Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Tafsiri rahisi ya ongezeko la 23% maana yake serikali ina chanzo cha makusanyo ambacho kina zaidi ya 23% ili kukidhi kuhudumia mishahara, posho na malimbikizo ya mshahara toka kwa watumishi wa umma.

Swali, je uwezo wa watumishi wa umma umekuwa na tija kiasi cha ukipita ongezeko la ukuaji wa pato la serikali, unalazimu watumishi kupokea 23% ya kile wanachopokea sasa.

Je, hazina ina mkakati gani wa muda mfupi na muda wa kati ili kuchochea uzalishaji wa sekta binafsi ambapo ndipo kwenye upanuzi wa tax base. Ng'ombe (privately sector) ili atoe maziwa, kuna mazingira ya kulishwa quantitative and qualitative dietary ili atoe maziwa ya kutosha?

Kama ni nyasi kavu msimu wa kiangazi, mmh, tax base utaendelea kuwa finyu sana na tutaendelea kuwa na narrow scope kuwa na tozo chungu mzima kwenye petroli.

Basic assumptions kama ngano tunayoagiza toka Russia na inasafirishwa kwa meli mpaka Tz ni takribani 90% ya mahitaji ya soko la ndani, kwanini hazina na wazara ya kilimo tusiwekeze kwenye commercial farming ya ngano kwa soko la Tz na nchi 8 majirani, ili inapouzwa, say serikali itatoza sh 200 kwenye kila kg inayouzwa ndani na nje ya Tz (Congo, Zambia, Malawi, Uganda, Burundi, Rwanda Madagascar, Comoro)

Likewise, kwanini pamba, korosho, chai, kahawa, cocoa, katani zisiuzwe kama constables products kwa kuchochea industrial processing ili ku-tax kwenye sales ya funal products?

Vinginevyo, mama atapata sifa za kisiasa ila baada ya muda Serikali itashindwa kujiendesha.

Tax revenue ya 1.5tril-2.3 ni ndogo sana.

Lazima serikali iwe sehemu ya kujenga financial instruments/leverage ambazo zitapelekea kununua technology ambayo itaogenza tija na ufanisi kwenye uzalishaji ambako ndipo kwenye vyanzo vya Kodi na kuongeza mzunguko wa fedha.

Weekend njema.
 
Kwani hiyo miradi mikubwa magufuli alikua anatumia fedha za ndani au mikopo?
Ukikuta deni la nchi $42.1 billion na tumewekwa as moderate risks kwa zaidi ya miaka 10.

Ukalishusha deni ndani ya miaka mitatu mpaka $37.4 billion kupewa hadhi ya low risk.

Katika muda wako ukakopa labda $5 billion na ukalipa $5 billion na mpaka unafariki deni la nchi lipo $37.4 billion; maana yake ume maintain the level of debt.

Ni rahisi sana kuwaambia watu, jamaa alikuwa anakopa sana lakini awakwambii katika alichokopa alilipa kiasi gani ndani ya muda wake.

Kwenye uongozi wa Magufuli deni la taifa lilikuwa stable baada ya kulishusha na kuitoa nchi from moderate risk to low risk.

Mwaka mmoja wa maza tumerudi tena kwenye moderate sasa hayo maamuzi yakupanda au kushushwa yanaenda sambamba na dept payments to revenue collection ata wakiongopa makusanyo yameshuka, halafu bado wanajiongeza admin costs.

The nonsense is beyond hivi vitu huwa vinakuja kuumiza mbeleni uwezi vificha vikianza kuuma tupo hapa.
 

[emoji110] a reason ambayo JF itabaki kuwa JF, Ahsante mkuu kwa nondo
 
Ulikimbia hesabu shuleni, au ulipata mswaki (F), hizo number ni kubwa na inaonekana kichwa chako kidogo sana!
Sasa hivi serikali inalipa wafanyakazi wake 500bn kwa mwezi.

Tu assume serikali iwaongezee kila mfanyakazi wake 50% ya mshahara wake.

Hii ina maana wage bili itakuwa 750bn kwa mwezi.

Je serikali haiwezi kupata hiyo 250bn kwa mwezi?
 
Shida yenu kubwa ni kuona yake mlioshindwa kufanya mama anafanya. Roho mbaya sana. Hili la wafanyakazi mlifanya kwa kuwakomoa, mama anajua hiyo miradi bila wafanyakazi wenye ari hakuna kitu.
 
Ongezeko la 23.3% ya mishahara Tanzania linaongeza 2.8 billion za hela ya South Africa au Tanzania hii hii? Hizi hesabu umezitoa kichwani kwa nani mbona kunasikitisha.

Kiuhalisia hakuna uwezekano wa kutekeleza ongezeko la 23.3% unless kama tunataka hata kujenga vyoo vya shule tuendelee kusubiri ugonjwa utokee duniani kisha Benki ya Dunia itoe hela tujenge watoto wanye humo sisi tushangilie na tuandike mabango nyuma ya hivyo vyoo.

Tanzania ina viongozi wanaombea majanga duniani, janga likiisha wanakasirika wanatamani waendelee kulisingizia. Kwanini simenti imepanda ~ Ukraine
Mbona mafuta ya kupikia yapo juu ~ Ukraine
Vifaa vya ujenzi vimepanda ~ COVID-19
Mbona mafuta yamepanda kuliko hata nchi zinazoyasafirisha kupitia Tanzania ~ Ukraine, ila hata Marekani yamepanda
Bidhaa zote zipo juu ~ Ukraine, na zitaendelea kupanda
 
Inawezekana wale wanaopokea kimya Cha chini ndo wameongezewa izo asilimia ila kadri unavyopanda juu asilimia zinapungua
Tulishaambiwa nchi hii ni tajiri sana! We ni nani unayetaka kuturudisha kwenye nyimbo za "sisi ni maskini"?
Na jana tu waziri wa fedha amesisisiza bado tupo uchumi wa kati. Sasa!!??
 
Utakuwa ni mfaidika wa Royal tour,inaonyesha upepo umekujaa kichwa kizima unatamani kila kitu ufe nacho wewe.Kama.nchi haina uzalishaji ni matatizi ya tokea Uhuru.Kuongeza mshahara wala sio starehe
 
Naona mfanyishwa kazi unafurahia tangazo na unachukia ukweli wa tangazo.
Sasa sikiliza wewe mfanyishwa kazi, alichoeleza mleta mada ni kwamba ongezeko hilo haliwezekani. Maana pato jumla la mwezi ni dogo kuliko mahitaji jumla ya mwezi.
Uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana, ndo maana kwao ni rahisi sana kumwelewa Mrisho Mpoto au Mwijaku kuliko ninachomweleza hapa.
Mwisho wa mwezi atakapokuta ameongezwa elfu 30 kwenye Mshahara ndo atajuwa asilimia 23.3% ilikuwa ni kwenye kima cha chini ambacho yeye hayumo! Ila wanasiasa walishachukua political mileage.
Siku zote huwa naamini mtu akishaajiriwa ata kama alikuwa na akili sana,baada ya muda mrefu akili yake hupungua uwezo.
Ni sawa na kumsajili Messi kwenye timu na kumweka benchi kwa muda mrefu ni lazima uwezo ushuke.
 
Huwa hamkosekani 🤣🤣
 
JOHN POMBE MAGUFULI and others wake Wana shida sana naona hawa
(1) FUMADILU KALIMANZILA
(2) TULIA ACKSON
wanaonyesha bado wapo kimkakati wanafagia kaburi la marehemu JIWE.
 
Wewe hujui kitu, tulia ! Hata maana ya bilioni huijui!
Angalia kupunguza Tshs.29 tu ya bei ya Lita Moja ya petroli ambapo zitahitajika Tshs.bilioni 100 imebidi Serikali kuomba mkopo WB.
Sasa itakuja kuwa 250 bilioni kila mwezi!!!
Nasisitiza HUJUI KITU, TULIA!
Sasa hivi serikali inalipa wafanyakazi wake 500bn kwa mwezi.

Tu assume serikali iwaongezee kila mfanyakazi wake 50% ya mshahara wake.

Hii ina maana wage bili itakuwa 750bn kwa mwezi.

Je serikali haiwezi kupata hiyo 250bn kwa mwezi?
 
Huwa hamkosekani 🤣🤣
Akili ndogo,hapo unadhani sasa kwamba Mimi napinga nyie kuongezewa Mishahara! Utapata akili pale utakapokuta Mshahara wako umeongezewa elfu 10 na wewe kuchekelea asilimia 23.3% ambayo ni kwa kima cha chini ambacho wewe haumo!
UJINGA NI MZIGO MZITO SANA KWA BINADAMU!
 
Fomula ya kukokotoa asilimia 23 ya kima Cha mshahara ipo Hivi
Kima Cha chini Cha mshahara ni 300000.
23/100x300000=69,000/=
Hivyo 69000-18% ya makato yote utaona umeongezewa sh.ngapi?
18/100x69000=12420
Sasa 69000-12420=56580.
Hivyo Basi nyongeza ya mashahara ni 56580 kwa kila mtumishi.
Hivyo tutegemee nyongeza ya 56000 kwenye mshahara.
Ndugu zangu msije pigia 23%ya basic eti ndio nyongeza mtakuta Julai Ni tofauti kabisa.
Na Mchanganuo wa Makato Kodi 8% pesheni5%Bima3% Vyama vya wafanyakazi 2% total 18
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…