Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Watu wa kulalamika kwa kila Jambo litendwalo na Serikali hataisha.Yaani Serikali imeamsha ari kwa wafanyakazi wake lakini BADO Kuna watu hawaoni jitihada hizi
 
Yaani Hadi tume iliyoundwa kukasimu nyongeza ya mshahara mnadhani haukuwa terms?Acheni Serikali ithamimi watumishi wake positively.Asingeongeza mngesema Serikali haijali wafanyakazi
 
Hakuna namna, either anakuja mwingine kama JPM kurekebisha mahesabu, kubana matumizi, kuweka vipaumbele sahihi kwa nguvu za kidikteta (hakuna mbadala) au tutauzwa jumla jumla.

Options nyingine ni kama ya watu wa Sri Lanka.
Yaani roho mbaya tu...waacheni watumishi nao waenjoy nchi Yao...mbona nyie mnapiga pesa ndefu na hatusemi?
 
Punguza kuwa nabii wa majanga (prophet of doom). SSH ameamua kuongeza mishahara ni suala zuri kuliko kuumiza mamilioni ya watu wakaishi kwa vinyongo wakati maisha haya ni mafupi.
Uko sahihi...yule dictator wao ambaye hakuongeza hata 10/- Yuko wapi Sasa hivi!?..acheni watumishi nao waenjoy nchi Yao
 
Mbona ww mshahara wako ni 1.2M take home ...Ila umekopa 20M halafu inabaki 300k take home na matumizi yako ni 500k kwa mwezi!! Lakini mbona watu wanaishi?
 

Ongezeko la bajeti kwa ujumla ni 19.51% maana yake ni nini?
 
Unauliza swali au umetoa hoja?
 
Ndani ya miaka saba maendeleo gani yalichochewa?

Acheni roho mbaya
 
Hesabu za kihasibu siku zote zina sura mbili, unapoongeza ni lazima uwe umepunguza au itapunguza mahali.
Ongezeko la 23.3% ambalo kwa vyovyote litagusa kima cha chini ni sharti liende sambamba na punguzo la 23.3% kutoka kwenye vipato vya watumishi wote wa ngazi za juu kwenye mihimili yote na hasa taasisi ya Urais.
 
NYUMA YA KILA MTUMISHI MMOJA KUNA WASIO WATUMISHI 8+
 
Mkuu
Mi Binafsi sioni tena kutangazwa bkwa miradi ile mikubwa ya kimkakati!
Sijui nini kumetokea hadi sasa!
NAJIULIZA
Mwenye majibu naomba!!
SGR haijamalizika, Stigler bwawa sijui Nyerere Hydropower haijamalizika, na miradi aliyoiacha mwendazake haijamalizika, unataka ianzishwe mingine? Tumalize hiyo kwanza
 
Yaani Hadi tume iliyoundwa kukasimu nyongeza ya mshahara mnadhani haukuwa terms?Acheni Serikali ithamimi watumishi wake positively.Asingeongeza mngesema Serikali haijali wafanyakazi
Uwe unajifunza kusoma na kuelewa mkuu, kuna mahali umenisoma napinga nyongeza ya mishahara au unakurupuka.
 
Hatutaki ujinga, kama kima cha chini ndicho kimeongezwa basi watu waelezwe ukweli bayana na siyo sifa za kijinga za akina Mwijaku!
Tanzania hatuna uwezo wa kuongeza Wage Bill yetu hata kwa 10% kwa sasa!
Mbona barua ya Ikulu imesema wazi kuwa hiyo asilimia iliyoongezwa ni kwa kima cha chini? Tatizo linaanzia wapi? Miaka yote mishahara inapoongezwa hutangazwa asilimia inayoongezwa kwa kima cha chini na inaenda inapungua kadri mshahara unavyokuwa mkubwa. What is the problem this time?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…