''...Tanzania haitakalika''

''...Tanzania haitakalika''

Well said,

Hii kusema tz haitakalika..kwa wanafunzi na mikopo..wanafunzi wa UD na % kidogo sana ya Watz wote..na ukiangalia watu wa kawaida wala hawawaungi mkono!

Hata maandamano yao..watu wa kawaida wanaona ni watoto tu..bado hawajakomaa...ndo maana maneno ya jazba kama Tz haitakalika huweza kutolewa.

Migogoro Tz imekuwa mingi..tangu 1961 na Tz ipo na watu wake hadi leo...kuna anayekumbuka wanafunzi UD kukataa kwenda JKT in mid 1960's- na Nyerere alichowaambia? Actually Mwalimu alikasirika hata akakaribia kuwachapa viboko!

Sii wanafunzi hawa hawa walikosa maji wakaenda kwa VC Luhanga wanampiga mlinzi..wakaenda UDASA wakawanywa bia..wakalewa..wakaenda Swiming pool..wakaogelea hadi bahati mbaya mmoja wao akafa? Kisa walikosa maji kwa siku kadhaa??

Ndo hawa hawa wanasema Tz haitakalika bila wote kupewa mikopo 100%?

Wanashindwa kusoma alama za nyakati!
 
Nilipewa dhaman ya kuwasajili hawa tukiwa na junior wenzangu kama 4. deadline ilipofika, hapo ndipo mwanzo wa picha nzima nilivyoipata.

Binti akiwa amevaa ushungi, mtoto mdogo amefaulu kutoka shule moja maarufi ya special school, akija ukweli akiwa anatoa machozi! alisema anasubiri wapewe mikopo na serikali, katika ule mkopo (posho ya chakula)atakaopewa ndio atakayokata alipe asilimia 40 anayodaiwa! mimi ni mtu mzima, na ndoa yangu changa, nilimwacha yule binti pale na kwenda chooni kutoa machozi kidogo. nikamuuliza sasa utakula nini? akasema sijui, kwao morogoro, dar hana ndugu, ila kuna watu anatoka nao kijiji kimoja, labda atakuwa akienda kwa katika nyakati za shida.

Nilimsikiliza wa pili,wa tatu, wa nne, mpaka wote 20. Moyo wangu ulijaa simanzi.

Waberoya,
Hii habari imenifanya leo siku nzima niwe na simanzi. Nafikiria kama angelikuwa ni dada yangu au mwanangu wa kike katika hiyo position. Uwezekano wa hawa mabinti kuingia katika biashara ya kujiuza ni kubwa sana. Na huko anaweza hata ishia kukwa magonjwa ya ajabu. Hii ni mbaya kuzidi hata JKT. Halafu utakuta vigogo haohao wanakwenda maeneo hayo jioni kuchukua vitoto vya watu.
Kuna watu hata uandike vipi, lazima wataona kuwa unachemka.

Ndugu yangu, endelea na moyo huo na utabarikiwa. Naona kwa nini Mungu kakupa hiyo kazi ya uwalimu. Mwalimu ni wito. (samahani kama wewe ni mtu ambaye haamini Mungu/Dini).
 
Kama leo kuna mtanzania yoyote bado anakubali ile kauli kuwa serikali haina uwezo wa kutosha basi huyo atakuwa anaishi kwenye dunia nyingine, yaani dunia ya ksadikika. Tunaweza kununua magari ya kifahari abayo hata serikali ya Japan yenyewe yanakotoka magari hayo hainunui, tunaweza kumpa kila waziri mashangingi mawili wakati waziri wa nchi kama Uingereza hawezi kutembelea gari kama hilo, sijui tunategemea nini. Tuna mdanganya nani tunapoema serikali haina uwezo wa kutosha, ni uwezo gani huo? Kama Mr Kagoda peke yake anaweza kukwapua mabilioni ya shilingi, nani anaweza kuamini kaul ya kuwa hatuna uwezo? Huu sio mwaka 84 au sio kipindi ch Mzee Ruksa ambapo serikali haikuwa na uwezo. Mkapa aliweka msingi mzuri wa kuifanya nchi iwe na pesa na inazo mpaka wenye uchu wanaiba Kwa hiyo ni lazima serikali i-invest kwenye elimu.
 
They have been telling us same stories for 40 years now since independence. tunashuhudia wana fedha nje ya nchi na kuishi maisha mazuri zaidi ya mawaziri wa nchi za dunia ya kwanza. hatuna sehemu ambayo tunajidai kuwa serikali inaweza AU MTETEZI WA SERIKALI TUMPE ASSIGNMENT ASEME NI LINI TUTEGEMEE SERIKALI ITAKUWA NA UWEZO?? LINI TUTEGEMEE UWEZO WA SERIKALI UTAKUWA "100%" if we ca not tell, yes tujue kuwa tuna viongozi bomu, wasio na vision.
 
Sasa swali ulilopaswa kujiuliza wewe kama mwalimu ulioona wanafunzi wenye hali ngumu mpaka ukalia ni je, kwa nini wanafunzi wenye hali ngumu wanakubali kugoma kudai kila mwanafunzi apewe asilimia 100 wakati wanajua kuna wenzao wenye uwezo wa kujisomesha. Na kwanini hujiulizi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe kwanini wasiripoti hao wanafunzi walioandikwa kuwa wana asilimia 60 na kupewa asilimia 100??? Je kwanini wanafunzi wanaamini in the solidarity ambayo haipo? Kama kuna solidarity basi wale wenye uwezo wasingeenda hata kuomba huo mkopo, Kama kuna solidarity wale waliopewa mkopo mkubwa kuliko mahitaji yao wangeripoti, kama kuna solidarity basi wanaosaliti solidarity wangeshughulikiwa. Ukweli ni kwamba mtu mwenye hali ngumu kama uliyoelezea hapa hawezi kuwa kiongozi wa mgomo hata siku moja. Viongozi wa mgomo huwa ni watu wenye alternatives.

Kuna kijana ninamfahamu alikuwa ana fujo sana shuleni. Alikuwa anaorganise migomo na fujo nyingi tu. Huyu jamaa ni mtoto wa kiongozi wa juu serikalini. Baba yake alikuwa hataki akasome nje ya nchi, sasa jamaa alikuwa anatafuta mbinu za kufukuzwa mlimani ili apate sababu ya kupelekwa kusoma nje!!! Sasa vitu kama hivi ndio hawa wanafunzi wanapaswa kuvitambua. Mtoto wa masikini anapata wapi nguvu ya kukataa kujaza form ya kurudi chuo?? Kwanza ndugu zake watamuelewa?

Kuna jamaa mwingine alikuwa nachukua mkopo bodi na hataki baba yake ajue kama ameomba mkopo, kwa sababu baba yake pia anampa mahitaji yake yote ya chuo. Sasa ni akili gani mnayoitumia kutaka kila mtu apewe asilimia 100?? Wewe kama ni mtetezi wa wanyonge unapaswa kutetea wanyonge wapewe asilimia 100 na ili hilo litokee ni lazima idadi ya wanaopewa mkopo iendane na uwezo uliopo, the best way to cut the number ni kuwatoa wenye uwezo wa kujilipia kwenye mahesabu ya mkopo.

Swala la TV nimetumia kama mfano tu, samahani kama limekuoffend fellow.

Still you are analyising things that are not practical! huo si ubinadamu unachotaka ni kulazimisha! haipo hiyo go anywhere duniani. Si kweli kuwa wale wenye uwezo waseme kuwa hatutaki mkopo! that beyond humn nature as far as i know them, people always want to have more! situation ingekuwa worse kama usingekuwa mkopo. hawawezi kuwa punished kwa sababu wanazo! ningekuwa mimi ningewabana kurudisha na pengine hata kurudisha kwa interest. Mkuu nakatwa sh. 11,000 kila mwezi kulipa deni hili la chuo kwa miaka 10, kipato ninachopata kwa sasa ni kikubwa kiasi ambacho hata wakisema wakate with interest, hata wakondoa 20,000 kila mwezi no problem!!

Hayo matatizo mengi wanafunzi viongozi wameripoti na serikali inajua hivyo, wakiwa serious inabidi waunde tume wapitie nyarak zote kuhakiki! it is costful, the only way wape asilimia 100!

Kama nitakuwa upande wako ku-promote hili swala, maoni yangu ni kuwa we need critical thinkers wewe na mimi tusadiane katika hili swala, ebu angalia

1. Serikali ilitakiwa kujitayarisha katika hili swala, kujiyatarisha huko kuendane kubadilisha mfumo wa elimu ambao utemuwezesha mtanzania anayemaliza kidato cha sita, kujiajiri, kuwa trainable katika post mbalimbali kazini.

2. Kuondoa barrier ya kupata kazi kwa hawa wanafunzi, wenzetu ulaya hususan nchi kama canada niliyopata wahi soma, kuna kitu wanahita summer job, to my surpirise mpaka watoto wadogo utawakuta wakipiga kazi sehemu mbalimbali kuongeza kipato, because they ar education is good

3. Kujitayarisha kwa serikali kuendane na ku-promote vyuo vingi ambavyo vitazalisha wataalamu kwa bei nafuu, katika mikoa mbalimbali, this is possible, if we need to build our country na sio kurely tu kwenye university as if mtu pekee anayetakiwa makazini lazima atko mlimani!

4. Vyuo vyote vya elimu ya juu vinatakiwa viondoe kitu kiachoitwa disco, hii itamfanya mwanafunzi asome kama anatka kusoma, afanye kazi katika nyakati asizo na fedha. suprising canada kwa mfano wanatoa asilimia 100 ya mkopo , lakini wanafunzi wengi wanafanya kazi na wanajisomesha , HII INAPELEKEA BODI YA MKOPO HUKU KUTANGAZA KWENYE MA TV, NA REDIO KUWAVUTIA WATU WACHUKUE MKOPO!!!!!!

Hali ya sasa ya wanafunzi inapelekea kutegemea wazazi wao zaidi wengi maskini wa kutupwa ambayo nikianza kuwaelezea muda hautoshi.

"" siri hapa ni kuwa hata kikwete hataki iwe hivi ila pressure za donors" na hii ilitakiwa kiongozi anayejali na kutetea watu wake. kwa kuwatayarisha kama nilivyoelezea hapo juu.

waberoya
 
Waberoyra,
Hapo Mlimani sii kuna kazi za usafi wa mazingira na mashirika kibao yanaajiri watu na kuwalipa 70,000 kwa kazi za kukatia fensi, kufagia, land scaping n.k kwa enoe la UD lilivyo kubwa hawa wafanyakazi ni zadi ya 1,000! Chuo hutenga pesa nyingi tu kila mwaka zetu sisi walipa kodi kufanya kazi hizo!

Je wanafunzi Watz hawawezi kufanya hizi kazi kama part time ili kujigharamia masomo..for 2-3 hours per day? Huwezi ukasema unatoka familia maskini alafu unachagua kazi!

Ni wakati pia wanafunzi wetu Watz tukafika mahali na kubadilika..tatizo sii kazi may be ni aina ya kazi! sasa mbona wazazi wetu hufanya kazi ya ukulima?
 
Last edited:
Still you are analyising things that are not practical! huo si ubinadamu unachotaka ni kulazimisha! haipo hiyo go anywhere duniani. Si kweli kuwa wale wenye uwezo waseme kuwa hatutaki mkopo! that beyond humn nature as far as i know them, people always want to have more! situation ingekuwa worse kama usingekuwa mkopo. hawawezi kuwa punished kwa sababu wanazo! ningekuwa mimi ningewabana kurudisha na pengine hata kurudisha kwa interest. Mkuu nakatwa sh. 11,000 kila mwezi kulipa deni hili la chuo kwa miaka 10, kipato ninachopata kwa sasa ni kikubwa kiasi ambacho hata wakisema wakate with interest, hata wakondoa 20,000 kila mwezi no problem!!

Hayo matatizo mengi wanafunzi viongozi wameripoti na serikali inajua hivyo, wakiwa serious inabidi waunde tume wapitie nyarak zote kuhakiki! it is costful, the only way wape asilimia 100!

Kama nitakuwa upande wako ku-promote hili swala, maoni yangu ni kuwa we need critical thinkers wewe na mimi tusadiane katika hili swala, ebu angalia

1. Serikali ilitakiwa kujitayarisha katika hili swala, kujiyatarisha huko kuendane kubadilisha mfumo wa elimu ambao utemuwezesha mtanzania anayemaliza kidato cha sita, kujiajiri, kuwa trainable katika post mbalimbali kazini.

2. Kuondoa barrier ya kupata kazi kwa hawa wanafunzi, wenzetu ulaya hususan nchi kama canada niliyopata wahi soma, kuna kitu wanahita summer job, to my surpirise mpaka watoto wadogo utawakuta wakipiga kazi sehemu mbalimbali kuongeza kipato, because they ar education is good

3. Kujitayarisha kwa serikali kuendane na ku-promote vyuo vingi ambavyo vitazalisha wataalamu kwa bei nafuu, katika mikoa mbalimbali, this is possible, if we need to build our country na sio kurely tu kwenye university as if mtu pekee anayetakiwa makazini lazima atko mlimani!

4. Vyuo vyote vya elimu ya juu vinatakiwa viondoe kitu kiachoitwa disco, hii itamfanya mwanafunzi asome kama anatka kusoma, afanye kazi katika nyakati asizo na fedha. suprising canada kwa mfano wanatoa asilimia 100 ya mkopo , lakini wanafunzi wengi wanafanya kazi na wanajisomesha , HII INAPELEKEA BODI YA MKOPO HUKU KUTANGAZA KWENYE MA TV, NA REDIO KUWAVUTIA WATU WACHUKUE MKOPO!!!!!!

Hali ya sasa ya wanafunzi inapelekea kutegemea wazazi wao zaidi wengi maskini wa kutupwa ambayo nikianza kuwaelezea muda hautoshi.

"" siri hapa ni kuwa hata kikwete hataki iwe hivi ila pressure za donors" na hii ilitakiwa kiongozi anayejali na kutetea watu wake. kwa kuwatayarisha kama nilivyoelezea hapo juu.

waberoya

Unaposema hali ya ubinadamu inakataa mtu kuacha ziada ili mwenziwe apate basics ni sawa na kusema kuwa hali ya ubinaadamu inakataa hiyo solidarity wanayoiamini wanafunzi wa UDSM!

ad 1. Mwanafunzi aliyemaliza form six anaweza kujiajiri. Nakumbuka mimi nilivyomaliza form six sikuwa kijiweni! nawafahamu wengi tu wanaofundisha tuition au kufanya business baada ya kumaliza form six. Siyo kwel kwamba mwanafunzi aliyemaliza form six hawezi kujiingizia kipato.

ad 2. Hizo kazi za summer hutolewa na makampuni binafsi. Makampuni kama hayo Tanzania yapo na yanapenda kutoa kazi kwa wanafunzi, je wanafunzi wangapi hutafuta kazi wakati wa likizo? Huko Cadana na nchi nyingine zilizoendelea siyo serikali inayoandaa kazi za summer kwa wanafunzi. Huwa kuna recruitment agents ambao wanaunganisha wanaotafuta kazi na wanaotafuta wafanyakazi. Hivyo basi kutokuwepo kwa kampuni za aina hii Tanzania isilaumiwe serikali tu. Huu ni mwanya wa ujasiriamali kwa kila mtanzania, tusipofanya hivyo watakuja wa afrika kusini kufanya biashara hiyo.
Tusiegemee kwenye kulaumu tu!

ad 3. Ukipata fursa, tafadhali ipitie hotuba ya waziri wa Elimu kwenye bunge la bajeti. Huu ni mkakati ambao serikali inautekeleza kwa miaka kadhaa sasa. Mojawapo ya utekelezaji wake ni kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo binafsi pamoja na kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa vyuo hivyo.

ad 4. Unaposema kusiwe na Disco unahitajika kuspecify kuwa iwapo mwanafunzi atasoma kwa muda unaozidi standard study time basi hataendelea kupewa mkopo. kwa sababu utakapoamua kuwaacha wasome B. Com kwa miaka 10 huku ukiendelea kumpa huyu mtu mkopo, unatarajia lini mkopo huo uanze kulipwa na je waalimu wanatosha kuaccomodate wanafunzi wanaorudiarudia mwaka? Idea ya kuwaacha watu wasome kwa private programme kulingana na muda wao ni nzuri lakini iwapo wataendelea kusoma miaka yote hiyo kwa kutegemea mkopo wa serikali inakuwa haifai.

Kimsingi ninachojaribu kusema ni kwamba jitihada zinazofanywa na serikali kuwawezesha wananchi kupata elimu zinastahili kupongezwa. Utekelezaji wa jitihada hizo hauko perfect, una mapungufu kadhaa yanayowakwaza baadhi ya wadau. Hivyo basi ni vyema wadau wakawasilisha madai yao kwa lengo la kuuwezesha utekelezaji uwe more perfect. Hata hivyo ni muhimu kuwepo na subira, kwa sababu kumridhisha kila mtu kwa mpigo wakati mwingine huwa ni ngumu. Sasa hizi tabia za wanafunzi kusioridhika kuamua kuwa hakuna kitachoendelea chuoni mpaka yale wanayotaka wao yatekelezwe yanadhihirisha kutokukomaa kiakili.
 
"" siri hapa ni kuwa hata kikwete hataki iwe hivi ila pressure za donors" na hii ilitakiwa kiongozi anayejali na kutetea watu wake. kwa kuwatayarisha kama nilivyoelezea hapo juu. [/COLOR][/B]
waberoya

Swala la Kikwete kutaka wanafunzi wote wasomeshwe na serikali kwa asilimia 100 sio siri, na wala si Kikwete peke yake na wala si kwa wanfunzi peke yao. Watanzania wote wangependa wawezeshwe kwa asilimia 100 na serikali, kuanzia mwalimu mpaka askari, dereva mpaka mkulima, mfanyabiashara mpaka mwanamuziki, kila mmoja anapenda kusaidiwa kwa asilimia 100 na Kikwete kama Rais angependa hali iwezeshe kuwawezesha hawa wote kwa asilimia 100. Hii ni common sense, wala hakuna siri yoyote.
Ila unaposema kuwa sera ya kuchangia elimu ni pressure ya donors ndio unakosea. Zaidi ya nusu ya bajeti yetu inategemea donors. Pesa wanazotaka wanafunzi ni zaidi ya bajeti nzima ya wizara ya Elimu, sasa unadhani kwa bajeti iliyopo sasa kuna haja ya kungoja any pressure ili kujua kuwa serikali pesa hizo haina????
Ni ukweli kuwa tunaweza kuongeza uzalisha mpaka Tanzania ikawa na surplus. Lakini kwa hivi sasa tuna deficit. Sababu za kuwa na deficit zinaweza kuwa nyingi, zingine zinaudhi na kufedhehesha. Lakini wanafunzi wanapoamua kutokuingia darasani mpaka wapewe kitu ambacho kwa sasa hakipo (hata kama serikali ina uwezo wa kuipata fedha hiyo in the future, lakini kwa leo hii na bajeti ya mwaka huu haipo!!!) inakuwa ngumu kuelewa objectives zao.
 
Halafu symbolically haimake sense kwa mwanafunzi anayeishinikiza serikali kumsomesha kusema kuwa hataingia darasani!!! Sasa kweli mtu anayelilia ada anaweza kukataa kuingia darasani?
Ingeeleweka iwapo wanafunzi hawa wangesema watakaa darasani au maktaba bila kutoka, lakini sio kukataa kuingia darasani!
 
Sasa swali ulilopaswa kujiuliza wewe kama mwalimu ulioona wanafunzi wenye hali ngumu mpaka ukalia ni je, kwa nini wanafunzi wenye hali ngumu wanakubali kugoma kudai kila mwanafunzi apewe asilimia 100 wakati wanajua kuna wenzao wenye uwezo wa kujisomesha. Na kwanini hujiulizi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe kwanini wasiripoti hao wanafunzi walioandikwa kuwa wana asilimia 60 na kupewa asilimia 100??? Je kwanini wanafunzi wanaamini in the solidarity ambayo haipo? Kama kuna solidarity basi wale wenye uwezo wasingeenda hata kuomba huo mkopo, Kama kuna solidarity wale waliopewa mkopo mkubwa kuliko mahitaji yao wangeripoti, kama kuna solidarity basi wanaosaliti solidarity wangeshughulikiwa. Ukweli ni kwamba mtu mwenye hali ngumu kama uliyoelezea hapa hawezi kuwa kiongozi wa mgomo hata siku moja. Viongozi wa mgomo huwa ni watu wenye alternatives.

Kuna kijana ninamfahamu alikuwa ana fujo sana shuleni. Alikuwa anaorganise migomo na fujo nyingi tu. Huyu jamaa ni mtoto wa kiongozi wa juu serikalini. Baba yake alikuwa hataki akasome nje ya nchi, sasa jamaa alikuwa anatafuta mbinu za kufukuzwa mlimani ili apate sababu ya kupelekwa kusoma nje!!! Sasa vitu kama hivi ndio hawa wanafunzi wanapaswa kuvitambua. Mtoto wa masikini anapata wapi nguvu ya kukataa kujaza form ya kurudi chuo?? Kwanza ndugu zake watamuelewa?

Kuna jamaa mwingine alikuwa nachukua mkopo bodi na hataki baba yake ajue kama ameomba mkopo, kwa sababu baba yake pia anampa mahitaji yake yote ya chuo. Sasa ni akili gani mnayoitumia kutaka kila mtu apewe asilimia 100?? Wewe kama ni mtetezi wa wanyonge unapaswa kutetea wanyonge wapewe asilimia 100 na ili hilo litokee ni lazima idadi ya wanaopewa mkopo iendane na uwezo uliopo, the best way to cut the number ni kuwatoa wenye uwezo wa kujilipia kwenye mahesabu ya mkopo.

Swala la TV nimetumia kama mfano tu, samahani kama limekuoffend fellow.

Aisee! Hata ueleweshwe vipi hutakaa uelewe. Kama kwa hoja zote zilizokwishatolewa bado unadhani serikali imefanya 'the best it could have done' (hii ni namna ninavyoweza kuelewa hoja zako) basi kweli Tanzania haitakalika.
 
1. Mwanafunzi aliyemaliza form six anaweza kujiajiri. Nakumbuka mimi nilivyomaliza form six sikuwa kijiweni! nawafahamu wengi tu wanaofundisha tuition au kufanya business baada ya kumaliza form six. Siyo kwel kwamba mwanafunzi aliyemaliza form six hawezi kujiingizia kipato.
Kijana sijui unaingelea zama zipi ulizomaliza from six.....i think ni 90's au mwanzoni mwa 2000...mkuu hii ni Tanzania njoo ujionee na sio kusoma kwenye blogs na Jf peke yake....Kama degree holder mwenye proffesional anakosa ajira hata ya 70k kwa mwezi iweje kijana wa form 6 HGL apate ajira....

Niambie mfano wewe umaliza from 6 leo hii 2008...umekosa nafasi ya kuingia chuo chopchote tanzania.....unatafuta kipato(kujiajiri) utaanzaje????? Nisaidie mkuu

2. Hizo kazi za summer hutolewa na makampuni binafsi. Makampuni kama hayo Tanzania yapo na yanapenda kutoa kazi kwa wanafunzi, je wanafunzi wangapi hutafuta kazi wakati wa likizo? Huko Cadana na nchi nyingine zilizoendelea siyo serikali inayoandaa kazi za summer kwa wanafunzi. Huwa kuna recruitment agents ambao wanaunganisha wanaotafuta kazi na wanaotafuta wafanyakazi. Hivyo basi kutokuwepo kwa kampuni za aina hii Tanzania isilaumiwe serikali tu. Huu ni mwanya wa ujasiriamali kwa kila mtanzania, tusipofanya hivyo watakuja wa afrika kusini kufanya biashara hiyo.
Tusiegemee kwenye kulaumu tu!
Mkuu unanisikitisha kweli kweli......niambie makampuni gani tanzania yanayotoa kazi za summer?? na kama yapo nakuapia hawawezi kuajili watu wasiokuwa na ujuzi.....
mkuu unalinganisha Canada na Tanzania????
Anyway wewe kama Mtanzania hebu ishauri basi serikali na wajasiriamali wengine maana unasema serikali isilaumiwe......

ad 3. Ukipata fursa, tafadhali ipitie hotuba ya waziri wa Elimu kwenye bunge la bajeti. Huu ni mkakati ambao serikali inautekeleza kwa miaka kadhaa sasa. Mojawapo ya utekelezaji wake ni kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo binafsi pamoja na kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa vyuo hivyo.
Mkuu hebu tafuta data kwanza....vyuo vingapi vya binafsi na wanafunzi wangapi wamepata mikopo...hizo ni piga domo za serikali ya tanzania tumezoea mara ngapi wanasema mkakati mkakati mkakati toka enzi ya nyerere mpaka leo vikao vya mikakati..lini itatekelezwa??

Hata hivyo ni muhimu kuwepo na subira, kwa sababu kumridhisha kila mtu kwa mpigo wakati mwingine huwa ni ngumu. Sasa hizi tabia za wanafunzi kusioridhika kuamua kuwa hakuna kitachoendelea chuoni mpaka yale wanayotaka wao yatekelezwe yanadhihirisha kutokukomaa kiakili.
Nimegundua wengi humu mmesoam majuu au mnaishi majuu mnakuja bongo krisimasi na mwaka mpaya mnatimua......mkuu hali ya bongo unaisoma Ippmedia na JF tu.....hiyo subira unayosema ilianza lini kusubiriwa??
Kusbiri gani huko kama hao wanaosema tuwasubiri wananunua gari la mil 100 4WD kwa matumizi ya Dar....
wawasubiri vipoi wakati hao hao wanajilimbikizia bilions of money nje na wanaviita vijisenti....
wawasubiri vioi hao hao....shit!

mkuu jiulize kwanini katika EA Tanzania inatoa wahitimu wachache?
Yes tanzania haitakalika
 
Hivi tunategemea kupata great people among watu ambao wanaona ni bora kununua TV kuuuubwa kuliko kujilipia ada? Hivi kuna haja gani kila mwanafunzi awe na TV yake pale mlimani. Je, TV Moja haitoshi kwa block nzima ya wanafunzi ambao wanaclaim kuwa ni masikini???
ngrrrrrrrrrrrrrr nachoka kabaisa.......this is too low
 
Kijana sijui unaingelea zama zipi ulizomaliza from six.....i think ni 90's au mwanzoni mwa 2000...mkuu hii ni Tanzania njoo ujionee na sio kusoma kwenye blogs na Jf peke yake....Kama degree holder mwenye proffesional anakosa ajira hata ya 70k kwa mwezi iweje kijana wa form 6 HGL apate ajira....

Niambie mfano wewe umaliza from 6 leo hii 2008...umekosa nafasi ya kuingia chuo chopchote tanzania.....unatafuta kipato(kujiajiri) utaanzaje????? Nisaidie mkuu

Mkuu unanisikitisha kweli kweli......niambie makampuni gani tanzania yanayotoa kazi za summer?? na kama yapo nakuapia hawawezi kuajili watu wasiokuwa na ujuzi.....
mkuu unalinganisha Canada na Tanzania????
Anyway wewe kama Mtanzania hebu ishauri basi serikali na wajasiriamali wengine maana unasema serikali isilaumiwe......

Mkuu hebu tafuta data kwanza....vyuo vingapi vya binafsi na wanafunzi wangapi wamepata mikopo...hizo ni piga domo za serikali ya tanzania tumezoea mara ngapi wanasema mkakati mkakati mkakati toka enzi ya nyerere mpaka leo vikao vya mikakati..lini itatekelezwa??

Nimegundua wengi humu mmesoam majuu au mnaishi majuu mnakuja bongo krisimasi na mwaka mpaya mnatimua......mkuu hali ya bongo unaisoma Ippmedia na JF tu.....hiyo subira unayosema ilianza lini kusubiriwa??
Kusbiri gani huko kama hao wanaosema tuwasubiri wananunua gari la mil 100 4WD kwa matumizi ya Dar....
wawasubiri vipoi wakati hao hao wanajilimbikizia bilions of money nje na wanaviita vijisenti....
wawasubiri vioi hao hao....shit!

mkuu jiulize kwanini katika EA Tanzania inatoa wahitimu wachache?
Yes tanzania haitakalika

Hivi bado hujajua kuwa utaratibu mpya wa kutoa mikopo ndio uliokiwezesha chuo cha Tumaini kuongeza idadi ya wanafunzi wake toka 200 mwaka 1997 hadi 8000 mwaka huu? Je hizi sio jitihada zinazostahili pongezi?

Wanafunzi ninaokwambia wanajiajiri kwa tuition etc. ninawajua live na sizungumzii hadithi. Hivi kuna watu wangapi wenye elimu chini ya form six dar es salaam lakini wanashughuli zinazowaingizia kipato? Elimu waliopata wao ina tofauti gani na ya wanafunzi wa UDSM mpaka imfanye mwanafunzi wa UDSM ashindwe na yule wa mtaani aweze kujitafutia kipato?

Hiyo ya kufananisha Tanzania na Canada, soma vizuri utaelewa kuwa hilo ni jibu la mchangiaji aliyefananisha Tanzania na Canada ambako alisoma. Hakikisha unasoma vizuri kabla ya kukosoa.

Tanzania imekuwa ikitoa graduates wachache kwa sababu vyuo vikuu vilikuwa vichache, sasa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi idadi ya vyuo inaongezeka na kama unafuatilia statistics utagundua kuwa we are improving kwa mwendo mzuri. Iwapo tutaacha kuwawezesha wanafunzi wa vyuo binafsi kama wanavyotaka wanafunzi wabinafsi wa UDSM basi hatutaweza kufikisha idadi inayolingana na nchi tulizo nazo jirani.

Mojawapo ya vitu vinavyochelewesha maendeleo Tanzania ni tabia ya watanzania kutokuwa tayari kujifunza kutoka kwa watanzania wenzao waliopata experience tofauti toka nje ya nchi. Sikilizeni na myaheshimu mawazo mbalimbali toka sehemu mbalimbali, hii itawawezesha kupata utatuzi mpya wa matatizo yanayo wakabili.Kama kila siku mtaendelea na migomomigomo tu hamtapata ufumbuzi mpya, mkumbukeni Obama wakati anatoa definition ya neno insane -''doing the same thing again and again, and then somehow expect different results.''
 
Wanafunzi ninaokwambia wanajiajiri kwa tuition etc. ninawajua live na sizungumzii hadithi. Hivi kuna watu wangapi wenye elimu chini ya form six dar es salaam lakini wanashughuli zinazowaingizia kipato? Elimu waliopata wao ina tofauti gani na ya wanafunzi wa UDSM mpaka imfanye mwanafunzi wa UDSM ashindwe na yule wa mtaani aweze kujitafutia kipato?
Hizo tuition kumbe ndio unazosemea?
kwa muda upi ataweza kupata darasa la kufundisha tuition?
Na pesa ngapi utapata?
Na ni location gani unayoisema? dar nafikiri.....

alafu mkuu tuzungumzie wanafunzi wote sio udsm peke yao.......

Suala la nyie wa nje msikilizwe ni jema sana na si kosa la watanzania ni kosa la viongozi wenu mliowapa dhamana ya kutawala....nenda leo useme una degree ya ulaya na unaweza kazi uone kama hutarogwa au kuundiwa skendo na kupotezwa mazima kazini...
 
Tanzania imekuwa ikitoa graduates wachache kwa sababu vyuo vikuu vilikuwa vichache, sasa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi idadi ya vyuo inaongezeka na kama unafuatilia statistics utagundua kuwa we are improving kwa mwendo mzuri. Iwapo tutaacha kuwawezesha wanafunzi wa vyuo binafsi kama wanavyotaka wanafunzi wabinafsi wa UDSM basi hatutaweza kufikisha idadi inayolingana na nchi tulizo nazo jirani.
mkuu unafahamu wanafunzi wangapi waanaacha masomo kwa kukosa hiyo %? nina ushahidi kwa hili
Iwapo tutaacha kuwawezesha wanafunzi wa vyuo binafsi kama wanavyotaka wanafunzi wabinafsi wa UDSM basi hatutaweza kufikisha idadi inayolingana na nchi tulizo nazo jirani.
Hivi wanafunziw a udsm hawataki wanafunzi wa vyuo binafsi????? sikujua
 
Hizo tuition kumbe ndio unazosemea?
kwa muda upi ataweza kupata darasa la kufundisha tuition?
Na pesa ngapi utapata?
Na ni location gani unayoisema? dar nafikiri.....

alafu mkuu tuzungumzie wanafunzi wote sio udsm peke yao.......

Suala la nyie wa nje msikilizwe ni jema sana na si kosa la watanzania ni kosa la viongozi wenu mliowapa dhamana ya kutawala....nenda leo useme una degree ya ulaya na unaweza kazi uone kama hutarogwa au kuundiwa skendo na kupotezwa mazima kazini...

Yaani unataka kusema wanafunzi wa Tanzania wana ratiba ngumu kuliko wanafunzi wote duniani wanaopata muda wa kufanya vijikazi??? Sidhani kama muda unakosekana iwapo kuna marengo.

Pesa wanayopata wanaofundisha tuition ni kubwa kuliko watu walioajiriwa na wizara. Ukiwa na wanafunzi kumi, kila topic unapata zaidi ya sh. laki moja. Hii ni asimilimia 10 ya ada kwa UDSM. Ndugu yangu amesoma hapo na amekuwa anafundisha at the same time, sasa amemaliza chuo na anaendelea na masters kwa mtindo huo huo so kusema kuwa haiwezekani sio ukweli. Yeye hajaajiriwa na ameoa mke! I have seen that it is possible from my own family.

Hivi sasa tunajadili mgomo wa UDSM ndio maana natoa mifano ya UDSM.
 
Unatania au upo serious!!!!!!!!!? Hahahahahahaaaa
Mkuu kwenye swala la tuition umechemka kabisa tena haufahamu tuition ni kiasi gani. Nikiwa TZ, tena mwakajana nimefundisha (Advance maths & Basic maths) tuition hapo DAR, jamaa zangu wapo mwenge, makumbusho, kumbukumbu mwembeni n.k huwa tunawasiliana. Hiyo laki moja unaipata kama unafundisha door to door kwa watoto wa waheshimiwa/wakubwa/mafisadi. Tembea DAR yote, hiyo hela haipo.
Unakazania tuition, wewe umeshawai fanya tuition? Unajuwa ni masomo gani zaid yanapewa kipaumbele na School candidates na Private candidate?

Samahani mkuu, kwa swala la tuition, umechemka. nakupa 1 out of 100. Huifahamu tuition ya laki moja per topic. Eti nifundishe Set (Form two -maths) kwa laki moja; Tanzania au ????
 
Mkuu; hivi unajuwa ratiba ya masomo mfano UDSM?
Kabla ya UDSM hawajapunguza miaka ya kusoma ualimu, iliwezekana kuwa na kufanya part-time ukiwa mwaka wa nne. Kwa miaka 3, inakuwa ngumu. Sababu kuu ni uwingi wa kozi hivyo kumfanya mtu kukonsentrati na masomo. Ninaafikiana na jamaa aliesema muda. Kuna baadhi ya wanafunzi, wanaosoma miaka 3, huwa na part-time. Waulize wana sapu ngapi. Ninayoongea sio kutoka hewani ((kama wewe ulivyosema mtu anapata laki per topic (Hahahahahaaaaaaaaaaa). Nimecheka sana, tena mpaka jamaa tulienae hapa kaniambia eti mimi mbea)).
Chukua idara ya maths mwaka 2006/2007. Madogo wa miaka 3 (Huwa tunawaida voda fasta) walifeli sana analysis, na waliofeli zaid ni wale ambao wanatution. Uzuri ni kwamba watu wa Maths tulikuwa wachache, tunafahamiana. Kwahiyo kutokana na muda na idadi ya kozi, part-time unatakiwa uwe makini. Jalibu kubisha kitu ambacho unauhakika, pia usilazimishe mambo mkuu. ****Mimi nimesoma UDSM, nimemaliza mwaka jana 2008 (Education, major maths)-4years, June*** na bahati nzuri nimepata nafasi ya masters nje ya TZ. Nimeona huku ratiba zao na kozi zao kwa undergraduate zipoje. Katika thread hii nimewai andika kuwa usi -judge kulingana na ulivyo wewe au ulipo wewe. Jaribu kumuuliza Yo Yo nadhani anaweza kukusaidia kama upo nje ya DAR. Nikisoma alichoandika Yo Yo kinaukweli zaidi tena perfect. Inaonekana Yo Yo anayajuwa mazingira.

Mkuu usikurupuke

Samahani mkuu, part-time kwa Tanzania inakuwa ngumu kutokana na Education system, the way course is assessed, contents of the course w.r.t time
 
Unatania au upo serious!!!!!!!!!? Hahahahahahaaaa
Mkuu kwenye swala la tuition umechemka kabisa tena haufahamu tuition ni kiasi gani. Nikiwa TZ, tena mwakajana nimefundisha (Advance maths & Basic maths) tuition hapo DAR, jamaa zangu wapo mwenge, makumbusho, kumbukumbu mwembeni n.k huwa tunawasiliana. Hiyo laki moja unaipata kama unafundisha door to door kwa watoto wa waheshimiwa/wakubwa/mafisadi. Tembea DAR yote, hiyo hela haipo.
Unakazania tuition, wewe umeshawai fanya tuition? Unajuwa ni masomo gani zaid yanapewa kipaumbele na School candidates na Private candidate?

Samahani mkuu, kwa swala la tuition, umechemka. nakupa 1 out of 100. Huifahamu tuition ya laki moja per topic. Eti nifundishe Set (Form two -maths) kwa laki moja; Tanzania au ????

Unajua bei ya huduma uamuliwa na mtoa huduma, ndio maana soda mlimani city ni sh. elfu moja wakati mtaani ni sh. 400.
Ninajua wanaofundisha topic kwa sh. elfu 20 ndio maana nimesema wanafunzi watano unapata laki kwa topic. Hata kwa wanaoamua kujifanya cheaper wanaweza kupata hiyo elfu 30, haiko mbaya.
Halafu kumbuka kuwa tuition ni mfano tu, kazi za kufanya ni nyingi. kuna aliyetoa mfano wa kusafisha bustani za chuo etc. Hili kuna siku niliwashauri wanafunzi wa muhimbili, wakaniambia hawawezi kusafisha muhimbili watajiaibisha! Well, hii ndio attitude ya wanafunzi wa chuo kikuu Tanzania unfortunately.
Kuna wanaoweza kupika, wangeweza kuanzisha huduma ya ''dada ntilie'' etc.
Yaani shughuli ziko nyingi. Iwapo kuna watu darasa la saba town wanaishi fresh, huwezi kuilaumu elimu eti imeshindwa kukuwezesha kujitegemea.
 
Ulichoongea nikweli kabisa, kuwa tuition huchajiwa kulingana na quality of the teacher. Nilipokuwa TZ Nimewai kuwafundisha watoto wa mkuu wa mkoa x, nilikuwa ninalipwa 70,000 per month per head. Walikuwa wanne. Mkuu kuzipata hizi ni nadra sana.
Kuhusu part-time zingine, ebwana ni kampuni gani la usafi ambalo linaweza kumpa part-time mwanachuo? The way companies are run, hayapendi part-time.

Kwa wanafunzi, kama wewe wajiona huna uwezo wa kupata 20% percent ya ada yako usichangue kazi. Fanya, by the way kazi ni kazi. Hii tabia ya ubrazamen au usisita duu si nzuri. Ni ujinga kukataa kazi ya kusafisha eti kisa wewe ni mwanafunzi. Not good at all.
 
Back
Top Bottom