Tanzania haitasita kuizuia Zambia kupitishia mizigo yao hapa nchini

Tanzania haitasita kuizuia Zambia kupitishia mizigo yao hapa nchini

Zambia hawalimi Mahindi?
Capitalist Economy, Free market economy tushindane kibiashara kwa diplomasia maana tukizuia shaba kupita pia tutakosa pesa pia.

Mbona simple 2 wauzie mahindi Zambia nao wauze congo maana Zambia nao hawalimi mahindi wanayatoa Tanzania kwa njia za magendo.

Imagine kama mfano msumbiji wakitaka kuuza mahindi kenya mtawaruhusu kirahi rahisi kupitisha apa kwetu?

Tatizo utawala wa Magufuli wamekosa diplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu ya mahindi tu muwaze kuwazuia wazambia kutumia bandari ya Dar.?

Hii serikali inapaswa iwe inatembea tembea nje kujifunza maana ya mahusiano.

Hivi anajua Zambia inachangia kiasi gani kwenye pato la nchi hii, hivi anajua ndani Zambia kuna maelfu ya Watanzania wanavuna tu huko na kuleta Tanzania..

Hizi kauli zingine bora kukaa kimya tu kuliko kuropoka namna hii.!

Huu udhaifu wa wanaccm kushindwa kushindana umeingia mpaka kwenye mahusiano ya nchi, wakiona mahali wanazidiwa wanakimbilia kwenye figisu.
 
Waziri wa biashara mh Bashunga amesema Zambia inafanya faulo katika biashara ya mahindi kwenye soko la DRC.

Mh Bashunga amesema kama Zambia wataendelea na faulo zao japo wote tuko kwenye SADC basi serikali haitasita kuizuia kupitishia mizigo yao hapa nchini.

Source ITV habari!
Mku Port Beira ya Mozambiq na hapa Dar wapi mbali ndugu.
Zambia hawapotezi ni kitu ila wanakuja Dar kwa mazoea tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wanajua Nyerere na Kaunda walikotokea wajaribu kuzuia kama mzimu wa Nyerere hautawazukia na matamko yao yasiyo na tija kwa Taifa.
 
Kabla Mheshimiwa Waziri hajatoa tamko lake aangalie critically prons and cons, na aone kuwa hakuna namna nyingine, hata ya mazungumzi, ndipo afanye maamuzi, au ashauri hilo lifanyike,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wao (serikali) wanavyofanya foul kuendelea kuwanyenyekea wachina na wanaingia nchini utafikiri kijana sharobaro anavyoingia na kutoka chumbani kwa sugar mamy.... God save us from COVID-19
 
Back
Top Bottom