Wengi wamekosa diplomasia ya uchumi sababu ya exposure.Mtembea bure si sawa na mkaa bure mtembeaji anapata exposure. Zambia wana bandari nyingi sana wanazotegemea sisi ndio tutakaoathirika.Wana bandari ya Angola, South Africa na ya Mozambique pia,hii yetu wanatumia sababu ya heshima ya Kaunda na Nyerere kama wanatuonea aibu vile.Kabla awamu ya kuzalisha masikini nchini haijaingia ni takribani truck elf 6 za watz zilikuwa zikivuka tunduma border kwa mwezi kati ya hizo ni truck 300 tu ndizo zilikuwa za wazambia na wacongo,watz walitengeneza faida nyingi sana kuanzia kodi,ajira,nk.Ilipoingia awamu ya kuwataka matajiri wawe masikini matajiri wengi sana watz sababu wana exposure yaani sio washamba wakuja wanalijua jiji walizihamishia truck zao na kuzisajilia nchini Zambia, Congo,Kenya,Malawi na Mozambique yaani waligoma kuishi kishetani msala wameachiwa wanyonge ndio wanalimia kucha kwa maana zile ajira za kwenye truck zilikufa zimeenda nchi za jirani sababu ukisajili truck kule lzm na madereva na matingo watoke kule.Truck nyingi zilizokuwa Tz ukienda Beira Mozambique unakutana nazo zinaenda Zambia,Congo,Zimbabwe kupitia njia ya Malawi.Hakuna mwanadamu yeyeto anaweza zuia riziki ya toka kwa Mungu wanasubiria awamu ya kuzalisha masikini ikipita watazirudisha tena bongo trucks zao ni kama ilivokuwa enzi za Nyerere alipotaka watu wawe masikini wachaga walihamishia pesa zao Kenya ,wahindi walihamia Canada,USA na UK wakaendelea kuwa matajiri alipoingia mzee ruksa wachaga wakazirudisha nchini ndio hao wakaanza kumiliki biashara za mabus,maguest,mahotel,mabar ,maduka nk ndipo wakaanza kuchomoza kina Mengi,Bakresa,nk enzi za Nyerere hawakuruhusiwa kuwa maarufu zaidi ya mwalimu. Masikini walifurahi sana matajiri wakishughulikiwa haswaa wakidhani watakuwa salama kumbe leo ndio hao wanalimia kucha baada ya hata meno kwisha.Matajiri wametulia tuli wanapokea check tu bizness zao nje zikinawiri.Tajiri kusomeshwa namba ni kaamua mwenyewe. Tumepoteza mapato na ajira sababu ya chuki na ubinafsi wa wasio na exposure, walidhani watawashusha matajiri kwa kuwasomesha namba kumbe namba wanazisoma wao sasa.