Tanzania haiwezi kuendelea kwa sababu Makanisa na Misikiti ni Mingi sana kuliko idadi ya Viwanda, Hospital na Shule

Nchi hizo zinazopiga marufuku dini ni wajinga sana,hawana akili.Dini ni uchumi.Kilq mwaka ukiwa na mahujaj laki 4 tu,wanaosafiri kwenda Hija,nchi inapata kodi kubwa ya kuanzia usafiri wa ndani,mahotel,chakula na huduma nyingine na tiketi za ndege na kodi za viwanja vya ndege.Kwenda na kurudi,ni pesa nyingi tu.Ni mjinga peke yake ndio atqkayezikataa pesa hizi za kodi na za kuongeza ajira.
 
Hujamuelewa mtoa hoja. Yupo sahihi
 
Uongo huuuuuu.
 
Sa itakuaje??
Sijasoma upuuzi alioandika ila Vijana wa sasa wana shida sana. Wanashindia kubet, umalaya na Uchawa alafu wanalaumu misikiti na kanisa. Wanaona Mabar, Madanguro, sehemu za kubet na Maguruguru ni sawa na zinaleta Maendeleo ila misikiti na kanisa ndio kikwazo.

Wanashindwa kupambana kwa ajili ya kujiletea maendeleo ila wanalaumu Makanisa na misikiti. Mi nimetoka Kanisani asubuhi hii, sasa naenda kupambana. Sasa hapo Kanisa limeninyimaje maendeleo.
 
Tanzania haiwezi kuendelea kwa sababu ya elimu mbovu.... Yaliyobaki ni matokeo ya elimu mbovu.
Elimu mbovu ndio inaleta viongozi wabovu wenye PhDs lakini kichwani hakuna kitu.
Elimu mbovu ndio inafanya wananchi wasijue haki zao na kuona viongozi Mungu watu
Elimu mbovu ndio inaleta mipango mibovu
Elimu mbovu ndio inafanya watu waamini miujiza huko kwenye nyumba za ibada.
Tatizo Tanzania ni elimu elimu elimu
 
Kwani makanisa na misikiti inasaidia Nini?


Kila siku inaongezeka ila IDADI ya uhalifu na matukio ya hovyo yanazidi kuongezeka!


Huyo mungu hawezi kuiokoa jamii Hadi ajengewe majumba ya kutupigia kelele!
 
Mwekezaji inatakiwa uwe wewe kichekoh na siyo mzungu aliyetoka Ulaya au Amerika... Fikirisha akili kidogo kaka
 
Yupoje sahihi? Makanisa na misikiti inazuiaje Maendeleo ya nchi na Maendeleo yako Binafsi?
Kwa mfano ukichukulia umbali wa msikiti mmoja mpaka mwingine ulipojengwa au kanisa moja mpaka lingine lilipojengwa. Unakuta wangejenga kanisa moja hiyo hela nyingine wangejenga kiwanda kidogo kitoe ajira kwa vijana. Hata hizo hospital zinazoota kama uyoga kila Mahali watu hawaumwi mzee. Watu wanastress za maisha zinazowaletea magonjwa. Gharama ya kujenga hospital kwa mfano ile ya tegeta pale. Unaweza kujenga kiwanda kikubwa tu ukawapunguzia watu pressure za maisha.
 
Huo mstali wa mwisho umekosea na umeharibu maana nzima ya maoni yako, swala ni kwanini nguvu kubwa inawekwa kwenye ujenzi wa nyumba za ibada kuliko huduma za kijamiii kama vile hospitali nyumba za walimu vyuo vya ufundi n.k
 
Sa itakuaje??

Itakuwa raha sana. Kila mtu asubuhi anaamkia kiwandani kufanya kazi. Hakuna kushinda vijiweni kubishana mambo ya simba na yanga. Kwenu wadada pia Ndoa zitakuwa nyingi maana kipato kinaleta ndoa imara. Bila ajira wanaume wengi hawaoi wanakunywa visungura tu kutwa nzima
 
Tukijenga viwanda ndio tutaendelea.

Ushauri wangu Makanisa na misikiti yote igeuzwe viwanda.

Kila kata kubaki na msikiti mmoja tu na kanisa moja tu la kuzugia
Wenzako hawataki hivyo wanataka muendelee kuzozania Simba na Mlandege huku wao wanapiga Pesa kwenye biashara ya siasa, ukileta habari za viwanda usiwaguse wao na Ajira zao za siasa wewe njoo na kiwanda chako watakusaidia kuja kukata utepe
 
Usukumani wapi kwenye umasikini unaonuka we **** nini
 
Ardhi ya akiba IPO ya kutosha njoo na kiwanda chako tunakupeleka Kimanzichana au Mkuranga kuna maeneo ya viwanda yapo tu unapewa unafungua kiwanda chako ya kusafirisha matunda nje ya Nchi Safi kabisa

Siku hizi misikiti na makanisa yanafuata watu sio watu wanafuata makanisa na misikiti zamani nakumbuka watu ndio waliokua wanafuata misikiti au makanisa yaan kanisa linajengwa mbali sana na makazi ya watu hata msikiti hivyo hivyo Ila siku hizi kila ukipiga kona kanisa hujamaliza kona msikiti huu hapa
 
[emoji1] diamond mwijaku kafanyaje
Wema sijui vp Wolper yuko nani
Twende tukaione nyumba ya mwijaku

Ova
 
[emoji1] diamond mwijaku kafanyaje
Wema sijui vp Wolper yuko nani
Twende tukaione nyumba ya mwijaku

Ova

Hizo zote sababu watu hawana kazi za kufanya.. hakuna viwanda. Watu hawana pa kwenda zaidi ya misikitini na makanisani tu. Lazima waangaike na kina mwijaku
 
Wajenge kiwanda kwa ajili ya nini? We umejenga kiwanda gani zaidi ya kubet na ufuska tu. Pumbau wahead wewe. Fanya kazi acha kujiita Afisa Ubashiri alafu ulalamike eti makanisa ndio chanzo.
 
Naunga mkono hoja hasa kwa haya makanisa na misikiti saccos , maana ni mali ya wachungaji na maimamu na ni mahsusi kwa ajili ya kujitafutia pesa tu wala hakuna kitu kingine, watu wanakusanya swadaka kama hawana akili nzuri kwa kuuza tuvitu twa ajabu ajabu kama mafuta udongo nywele , keki na kadhalika. UKO SAHIHI SANA MLETA MADA.
 
Pesa tunazochangishwa kwa ajiri ya ujenzi wa makanisa na misikiti ingetumiwa kwa kujenga viwanda tungekuwa mbali Sana kiuchumi.
Usitupangie matumizi ya hela zetu. Tunaishi dunia huru. Wewe jenga kiwanda, Sisi tutanenga nyumba za ibada. Jasho langu alafu unanipangia matumizi. Mbona bar zipo kila Kona hamsemi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…