Mtazamo mbaya wa Kitanganyika kwamba ukifanikiwa kwenye private sector wewe ni mwizi.
Marekani imewahi ongozwa majenerali wazuri wastaafu, wanasheria wakubwa, wafanyabiashara na hadi sasa Rais mteule ni mfanyabiashara, bondia kama Abraham Lincoln, mwigizaji wa filamu kama Ronald Reagan na hawa wote walifanikiwa kwenye fani zao.
Hufyatuki uko ukagombea Urais na hujawahi fanikiwa kwenye jambo lolote ulilofanya. Wala huji kugombea wakasema wewe ni tajiri hivyo ni mwizi, Rais Ford alikuwa billionaire na alifanya sera nyingi nzuri zinazohusiana na sheria za kazi. Hata sheria ya siku 5 za kazi, saa 8 za kazi, siku mbili za weekend aliianzisha yeye huku wakosoaji wakiipinga vikali.
Ford aliianzisha kwenye kiwanda chake, Ford akiwa mmiliki wafanyakazi wake waliweza jenga nyumba, miliki gari na kulea familia huku mama akiwa wa nyumbani. Wamefuata Marais hao unaoita sio wezi wakaharibu.
Israel viongozi wao hasa Waziri Mkuu aliwahi fanikiwa kwenye jambo lao kuu, ulinzi na usalama.
Sasa sisi mtu alikuwa UVCCM, mjumbe wa sijui nini, kaimu, mkuu wa wilaya, boom Waziri alafu leo Wizara ya Afya, kesho Wizara ya Michezo na kote uko hajui kitu.