Tanzania hatujawahi kuwa na Marais au Mawaziri ambao kabla ya madaraka waliwahi kuendesha mradi wowote na wakafanikiwa

Umenena vyema.
 
Tumeshapita enzi za Mercantile Capitalism.
Kazi kubwa ya serikali sio kukusanya mapato, bali kutengeneza mazingira mazuri ya raia wake kufanikiwa. Makampuni binafsi ndio yaliyokuja ya kwanza kujitwalia makolini Africa, mashamba na migodi enzi za ukoloni ilikuwa inamilikiwa na watu binafsi ambao walikuwa wanalipa kodi tu kwa serikali za kikoloni. Watawala kazi yao ilikuwa kuhakikisha kuna mazingira mazuri ya hao watu kufanya mambo yao.
 
Makampuni yaliyo duniani kote sio ya Magharibi tu, yako ya Wachina, yako ya Waarabu kama DP World, Yako ya Singapore, Brazil, Vietnam, Russia, Korea Kusini n.k
 
Kutenganisha mapato ya serikali ni sawasawa na kuanza kubishana yai ma kuku nani ni nani...
Serikali inakutengenezea mazingira mazuri ili baadae ichukue kodi yake ikawaletee wananchi wengine maendeleo - Kutengeneza mazingira bora ya watu wakujiendeleza na kukusanya kodi kwa usahihi na ufasaha ni pande mbili za shilling
 
Serikali inaweza kukopa kujiendesha, inaweza kuuza maliasili zake, sio lazima ikusanye kodi, Serikali inaweza kukusanya kodi na isifanyie mambo ya maana. Lengo kubwa la uwepo wa serikali sio kodi.
 
Mtu yoyote mwenye uwezo wa kuongoza naye aongoze au kama vipi twende na meritocracy system kazi itakuwa nzito hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…