TANZANIA HATUJUI KUCHOMA NYAMA SABABU NYAMA YETU NI MBAYA

Ed edd n eddy

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2016
Posts
263
Reaction score
345
Utamaduni wetu wa nyama choma hapa Tanzania kwa ujumla ni wakishamba sana. Ukiagiza nyama choma matarajio ya watu wengi ni nyama iive mpaka ndani iwe imekauka kabisa. Ukiomba medium rare au rare, unaweza kuangaliwa kana kwamba umeagiza nyama mbichi kutoka machinjioni.

Tatizo letu ni kwamba tumefundishwa kuamini kuwa nyama ikiwa na rangi ya pinki katikati, basi haijaiva. Nyama inakauka mpaka inakosa juisi yakw

Katika nchi zenye kujua nyama watu wanafurahia steak ya medium rare kwa sababu wanathamini ulaini na ladha halisi ya nyama. Hapa kwetu, mara nyingi tunaichoma mpaka inakuwa ngumu kutafuna, halafu tunaifunika kwa pilipili, chumvi nyingi na viungo ili angalau iweze kuliwa.

Pia mi naona huenda wengi wetu hatujapata nafasi ya kutosha kuonja nyama bora iliyotayarishwa kwa mbinu tofauti. Nyama yenye ubora mzuri, ikipikwa au kuchomwa vizuri inaweza kuwa na ladha nzuri bila kuhitaji kuchomwa mpaka ikauke. Wakati mwingine, kuichoma kupita kiasi kunaficha ladha na ubora wake badala ya kuviendeleza.
 
ok.🐒
 
Running cost ni kubwa chakula cha kuku wa nyama ununue laki moja kwa mfuko halafu huyo kuku uje umuuze 5k?
mchawi ni bei ya mbolea tu,ingekua chini,uzalishaji nafaka ungekua mkubwa kwa gharama ndogo,kupelekea bei ya chakuka cha mifugo kuwa chini na kupelekea overproduction ya mifugo,na so bei ingeshuka juu ya oversupply
 
Daah umenikumbusha niliagiza nyama ya kuku beach flan Dar broiler kafanyia seasoning mpk radha ya kuku hamna ni maviungo tu asee ,so sikuping mzee
 
Unakutana na nyama ngumu, nyeusi tii mpana unajiuliza kama huyu ng'ombe alikuwa mzima wa afya je angekuwa mgonjwa nyama ingekuwaje 😂
 
Back
Top Bottom