TANZANIA HATUJUI KUCHOMA NYAMA SABABU NYAMA YETU NI MBAYA

Kwangu mimi medium rare naona kama ni undercooked, mimi huwa sipendi kusikia ile shombo ya ubichi wa nyama hata kwa mbali, sawa sipendi ikauke napenda iwe juicy ila iive kabisa na iwe seasoned
 
Sehemu kubwa ya ufugaji wetu inategemea ng’ombe wanaozurura kutafuta malisho, badala ya proper beef production inayolenga kwa makusudi kuzalisha nyama yenye ulaini na ubora unaotabirika. UkiLinganisha nyama ya Kenya au SouthAfrica utaona utofauti mkubwa sana.. Ndio maana Arusha kuna baadhi ya ufugaji proper wa nyama ukibahatika kuipata ile nyama.
 
Nyama za mijini ndizo zimeingia shida kwasababu ya matibabu ya kisasa, ila nyama ya vijijini ni tamu kwakuwa mifugo inajitibu kwa aina za vyakula na wingi wa majani tiba ya maporini huko
 
Dah! Kwa hiyo kwenye huu uzi watu mnajadili jambo moja tu! Nyama choma! Nje ya hapo unaweza kufukuzwa kama mwizi!
 
tatizo uandaaji,,ilitakiwa waende course uturuki wajifunze vyenye nyama huchomwa
Mifugo imedumaa machinjioni, utatumia ufundi gani kuandaa nyama ngumu mpaka uichemshe kama maharage.
Tatizo linaanzia kwenye mfumo wa kukuza mfugo mpaka kumleta mezani kama mlo. Watunga sera wamelala uchumi umedorola, hii kitu ilitakiwa iongeze idadi ya watalii na ajira, Tanzania kuna mifugo mingi sana.
 
Nyama za mijini ndizo zimeingia shida kwasababu ya matibabu ya kisasa, ila nyama ya vijijini ni tamu kwakuwa mifugo inajitibu kwa aina za vyakula na wingi wa majani tiba ya maporini huko
sio kweli. Nyama ya mjini imedumaa kama matokeo ya kwenye mfumo mzima wa utunzaji hasa kwenye marisho na kuchagua mifugo iliozeeka sana.
 
HUNA LOLOTE SISI WAMASAI HATULI NYAMA CHAKULA CHETU.KIKUU TOKA ZAMA NI NYAMA NA MAZIWA IWE MBICHI IWE IMEIVA NI UTAMADUNI WETU.



USILETE UTAMADUNI WA WATU WENGINE WANAOJARIBU KUHARIBU MFUMO WETU NYAMA .

Nyama tunakula kwa kuchomwa au kupikwa acha kutuletea mambo ya brain wash hapa.

Beberu wewe !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…