Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine
Imesisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo hilo ndilo walilotaka lakini halikutokea.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema: “Katika sera yetu ya mambo ya nje ni kutafuta muafaka, kutumia njia ya diplomasia, lakini hilo halikuwezekana ndiyo maana katika kupiga kura tukaamua kutofungamana na upande wowote.
“Lengo ni kutoa meseji kuwa sisi hatufungamani na upande wowote, hivyo kutopiga kura ni kuonyesha msimamo wa Tanzania.”
Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Ulaya (EU) utoe tamko kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi hadharani.
Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.
Source: TBC