Tanzania: Hatukupiga kura sababu tulichotaka kati ya Urusi vs Ukraine hakikutokea!

Tanganyika hadi Tanzania haijawahi kuwa na msimamo tangu kuumbwa kwake.

Wewe Fikiria Mreno kapita, Mwarabu kapita, Mjerumani akafanya yake, Mwingereza akamalizia shughuli.

Haya kuna msimamo hapo?

Kwanza maskini anawezaje kuwa na msimamo?
 
Serikali ingetamka tu wazi kuwa tunalaai kitendo cha taifa lolote duniani kuvamia nchi ingine ambayo haijawavimia kijeshi iwe Russia au yeyote
 
Tanganyika hadi Tanzania haijawahi kuwa na msimamo tangu kuumbwa kwake. Wewe Fikiria Mreno kapita, Mwarabu kapita, Mjerumani akafanya yake, Mwingereza akamalizia shughuli. Haya kuna msimamo hapo?
Kwanza maskini anawezaje kuwa na msimamo?
Wakati Urusi ilipovamia Czechslovakia mwaka 1968 Tanzania chini ya Nyerere tulialaani kitendo hicho. Wakati Urusi ilipoivamia Afghanstan mwaka 1979, Tanzania chini ya Nyerere tuliaani kitendo kile; ni wakati huo huo ndipo Amini alipoivamia Tanzania, na bado pia tukalaani. Wakati Saddam alipoivamia Kuwait mwaka 1990, Tanzania chini ya Mwinyi tulilaani kitendo kile.

Wakati marekani ilipoivamia Iraq mwaka 2003, Tanzania chini ya Mkapa tulialaani kitendo hicho.

Kwa nini mwaka huu urusi imeivamia Ukraine na tukashindwa kulaani?
 
Kwa misaada tuliyokomba ni ngumu mno kuonyesha tupo upande gani
 
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine

Imesisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo hilo ndilo walilotaka lakini halikutokea.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema: “Katika sera yetu ya mambo ya nje ni kutafuta muafaka, kutumia njia ya diplomasia, lakini hilo halikuwezekana ndiyo maana katika kupiga kura tukaamua kutofungamana na upande wowote.

“Lengo ni kutoa meseji kuwa sisi hatufungamani na upande wowote, hivyo kutopiga kura ni kuonyesha msimamo wa Tanzania.”

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Ulaya (EU) utoe tamko kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi hadharani.

Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

View attachment 2161931

Source: TBC
Tanzania ya leo msimamo wao wa Aina yyt kuunga au kutounga mkono hauna athari yyt kwenye maamuzi ya kidunia..
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi. Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga. Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
Yaani huo unao wala wazir hahitaji kukufanya mjinga
 
Wakati Urusi ilipovamia Czechslovakia mwaka 1968 Tanzania chini ya Nyerere tulialaani kitendo hicho. Wakati Urusi ilipoivamia Afghanstan mwaka 1979, Tanzania chini ya Nyerere tuliaani kitendo kile; ni wakati huo huo ndipo Amini alipoivamia Tanzania, na bado pia tukalaani. Wakati Saddam alipoivamia Kuwait mwaka 1990, Tanzania chini ya Mwinyi tulilaani kitendo kile. Wakati marekani ilipoivamia Iraq mwaka 2003, Tanzania chini ya Mkapa tulialaani kitendo hicho.

Kwa nini mwaka huu urusi imeivamia Ukraine na tukashindwa kulaani?

Siasa ya kutofungama na upande wowote ilianzishwa na nani ili itumike wakati gani? Wakina Doctor Shika msitulazimishe kumuunga mkono Urusi.
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi. Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga. Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
Gharama kivipi mkuu. Acha uoga !!!!
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi. Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga. Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
Unaifahamu sera ya Tanzania dhidi ya hizi blocks mbili kubwa duniani?
 
Serikali iende mbele zaidi iombe Umoja wa Mataifa wairuhusu iwe msuluhishi wa huu mgogoro.

Mzee Kikwete aombwe aifanye hiyo kazi.
 
Ila sisi kama Tz, tunaamini katika dola na jamhuri, tunaamini kwamba tunatakiwa kujilinda na wavamizi wa nje, kwamba hatutakiwi kulazimishwa kufanya maamuzi haswa ya nchi, taasisi gani ujiunge nayo na ipi uiache.

Leo hii Uganda akisema Tz jitoe EAC unanitishia amani itamaanisha kwamba anaingilia sovereignty yetu na itabidi kujilinda.

Hicho ndicho anafanya Ukraine.

Leo anakwambia usijiunge hapo ukakubali, kesho atakuambia jitoe na huku, ukakubali, atarudi tena kukuambia naomba wanajeshi wakanisaidie kupigana so unakua kama subordinate wake badala ya nchi inayojisimamia.

Waziri anasema kwamba hatukupiga kura kwakua tulilolitaka la maridhiano halikutokea sasa kama lingetokea kungekua na haja ya kupiga kura? Si ingekua mambo yameisha? Hayajaisha na hayajafika kwenye maridhiano ndiyo maana kura imehitajika.

Natumaini ataona matundu ya hoja yake.
 
Siasa ya kutofungama na upande wowote ilianzishwa na nani ili itumike wakati gani? Wakina Doctor Shika msitulazimishe kumuunga mkono Urusi.
Inaelekea huelewi maana ya kutofungamana na upande wowote -Non Aligned Movement (NAM).

Kwani hayo matukio manne niliyotaja hapo juu kulikuwa hakuna sera hiyo ya kutofungamana na upande wowote? Nyerere mwenyewe aliyekuwa mjamaa bado alilaani kitendo cha urusi kuvamia Czechoslovakia na Afghanstan.

Wewe unaelekea kuimba siasa ya kutofungamana kwa mtazamo mfupi wa ama upande wa Urusi au upande wa Marekani, ambao ni mtazamo mfupi sana na hauna uhusiano wowote na tukio hili.

Kwa hiyo unapoona watu Ukraine wanauwawa bila makosa unachukulia hiyo ni sawa mradi hufungamani na Marekani?
 
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine

Imesisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo hilo ndilo walilotaka lakini halikutokea.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema: “Katika sera yetu ya mambo ya nje ni kutafuta muafaka, kutumia njia ya diplomasia, lakini hilo halikuwezekana ndiyo maana katika kupiga kura tukaamua kutofungamana na upande wowote.

“Lengo ni kutoa meseji kuwa sisi hatufungamani na upande wowote, hivyo kutopiga kura ni kuonyesha msimamo wa Tanzania.”

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Ulaya (EU) utoe tamko kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi hadharani.

Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

View attachment 2161931

Source: TBC
Sababu za kijinga.
 
Inaelekea huelewi maana ya kutofungamana na upande wowote -Non Aligned Movement (NAM).

Kwani hayo matukio manne niliyotaja hapo juu kulikuwa hakuna sera hiyo ya kutofungamana na upande wowote? Nyerere mwenyewe aliyekuwa mjamaa bado alilaani kitendo cha urusi kuvamia Czechoslovakia na Afghanstan. Wewe unaelekea kuimba siasa ya kutofungamana kwa mtazamo mfupi wa ama upande wa Urusi au upande wa Marekani, ambao ni mtazamo mfupi sana na hauna uhusiano wowote na tukio hili.

Kwa hiyo unapoona watu Ukraine wanauwawa bila makosa unachukulia hiyo ni sawa mradi hufungamani na Marekani?

Kwa nini Ukraine anataka kuvunja kiholela makubaliano na Urusi kwamba asijiunge NATO?
 
Sera yetu tokea enzi na enzi na hiyo, beberu Watuache!
Put-in atatuchamba Sana na bunduki Used hatotuuzia,

Wao wenyewe wanamgwaya Put-in, mkurungwa kaingia Kwa jirani, jirani hajarogwa kurusha japo kombora moja Moscow, hii inanifanya niwaone wale wa Houthi wa Yemen ni wababe, mikombora wamepiga mpaka Saudi!

Tutajadiliana Tu mitandaoni inatosha!

Hao mabalozi watuache mara chanjo mara kutugombanisha na rafiki zetu wanaogombana!
 
Wakati Urusi ilipovamia Czechslovakia mwaka 1968 Tanzania chini ya Nyerere tulialaani kitendo hicho. Wakati Urusi ilipoivamia Afghanstan mwaka 1979, Tanzania chini ya Nyerere tuliaani kitendo kile; ni wakati huo huo ndipo Amini alipoivamia Tanzania, na bado pia tukalaani. Wakati Saddam alipoivamia Kuwait mwaka 1990, Tanzania chini ya Mwinyi tulilaani kitendo kile. Wakati marekani ilipoivamia Iraq mwaka 2003, Tanzania chini ya Mkapa tulialaani kitendo hicho.

Kwa nini mwaka huu urusi imeivamia Ukraine na tukashindwa kulaani?
Wakati Idi Amin alipoivamia Tanzania, si kwamba tulilaani tu, bali tuliuomba ulimwengu ulaani kitendo hiki. Leo hii tunapata kigugumizi kuilaani Urusi.
 
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine

Imesisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo hilo ndilo walilotaka lakini halikutokea.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema: “Katika sera yetu ya mambo ya nje ni kutafuta muafaka, kutumia njia ya diplomasia, lakini hilo halikuwezekana ndiyo maana katika kupiga kura tukaamua kutofungamana na upande wowote.

“Lengo ni kutoa meseji kuwa sisi hatufungamani na upande wowote, hivyo kutopiga kura ni kuonyesha msimamo wa Tanzania.”

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Ulaya (EU) utoe tamko kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi hadharani.

Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

View attachment 2161931

Source: TBC
Hiyo kauli ya Waziri haina mantiki. Kama tunataka Urusi na Ukraine wamalize mgogoro kwa njia ya mazungumzo, je ni nani katika hizo nchi mbili iliyoamua kutumia nguvu?

Kama kweli tunataka mgogoro kati ya Ukraine na Urusi umalizwe kwa njia ya mazungumzo, tungetoa kauli ya kulaani kitendo cha uvamizi. Maana hizi nchi mbili, hazishambuliani.bali Urusi inaishambulia Ukraine.

Hii nchi yetu, kwa sasa naona imetoka kwenye misingi yake ya kitaifa ya kusimama na wanaoonewa.

Mwaka 1978, Ugamda ilipoivamia Tanzania, baadhi ya mataifa yalikaa kimya kama tulivyofanya sisi kwenye mgogoro huu wa Russia na Ukraine, Mwalimu Nyerere aliyalaani sana mataifa yaliyokaa kimya. Akasema, 'hatuhitaji watusaidie, lakini angalao watoe kauli tu ya kumlaani Idd Amin kwa kuivamia Tanzania'.

Hii nchi yetu kwa sasa imekuwa isiyoeleweka siyo kwa sababu nchi imekuwa hovyo, bali aina ya watu wanaoiwakilisha Tanzania kimataifa, hawajitambui.
 
Back
Top Bottom