Kwa nini Ukraine anataka kuvunja kiholela makubaliano na Urusi kwamba asijiunge NATO?
Hakukuwa na makubaliono yoyote ya namna hiyo. Soma historia ya jambo hilo kwa ukamilifu wake, usikimbilie kumeza maneno ya Putin ambayo ni uwongo mtupu.
Mwaka 1949 baada ya vita iliyokuwa imeanzishwa na na Ujerumani, dunia ilikuwa imegawanyika makundi mawili, moja lilikuwa linaongozwa na muungano wa nchi za Urusi, na la pili lilikuwa linaongozwa na muungano wa nchi za magharibi. Kwa vile Ujerumani ndiyo iliyokuwa imeanaisha vita ile, ilivunjwa vipande viwili, kimoja kikawa chini ya muungano wa Magharibi, na kingine kikawa chinia ya muungano wa Urusi. Nchi kadhaa za Magharibi (siyo zote) zilingia mktaba wa
kushirikiana iwapo mmoja wao atashambuliwa, mkataba huo ndio unaoitwa
NATO leo, vile vile nchi saba za mashariki zikaingia mkataba wao wa kuwa na
ulinzi wa pamoja ulioitwa
Warsaw Pact ambazo zilikuwa zinatawaliwa kikomunist
. Nchi kadhaa za Ulaya hazikutaka kuingia mktaba wowote kati ya hiyo miwili: nchi hizo ni pamoja na Austria, Cyprus, Finland, Ireland, Malta, na Sweden.
Miaka 40 tangu ya kuanzishwa kwa NATO na WP, nchi zilizokuwa chini ya NATO ziliendelea sana kiuchumi wakati zile zilizokuwa chini ya WP zikirudi nyuma sana kiuchumi na maisha kuwa magumu kila siku. Mwaka 1987 Gorbachev akiwa Katibu Mkuu wa chama cha kikomunist alihimiza mabadiliko ya kiuchumi ya Perestroika, ambapo pamoja na mambo mengine alihimiza nchi wanachama wa USSR na wale wa WP kufanya maamuzi yao ya kiuchumi wenyewe badala ya kusubiri kuamuliwa na viongozi wa juu (Perestroika) na kutaka serikali ziongoze kwa
ukweli na uwazi (glasnost). Hiyo ilisababisha nchi zilizokuwa chini ya WP kuanza kuachana na uchumi wa kikomunist, hali iliyopelekea kuanguka kwa tawala za kikomunist katika nchi zote za WP ambapo kule Romania rais wa nchi ile pamoja na mke wake walinyongwa hadharani. Mabadiliko hayo yakazikumba hata nchi za Afrika ambapo Msumbiji waasi wa Renamo wakaanza kupambana na utawala wa kikomunist wa Frelimo, serikali ya kikomunist ya Haile Mariam huko Ethiopia nayo ilipinduliwa na hata China kukawa na Maaandamano ya Tianamen Square kupinga utawala wa kikomunist.
Kutokana na mabadiliko hayo nchi za Ujerumani Magharibi na Mashariki zikaonyesha nia ya kuungana tena kuwa nchi moja, na katika mchakato huo kukawa na tatizo kuwa kwa vile Ujerumani Magaribi iko chini ya NATO, na Ujerumani Mashariki bado iko chini ya WP, itakuwaje zikiungana. Kulikuwa na alternative mbili: ama zote ziachane na mikataba hiyo, au zote ziwe chini ya mkataba mmoja. Waziri Mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher hakutaka ziungane, Rais Reagan wa Marekana akasema iwapo zitaungana basi ziwe chini ya NATO, Chancellor wa Ujeruman Helmut Kohr naye alitaka ziwe chini ya NATO. Hivyo mazungumzo yakafanyika kati ya Reagan, Kohr na Gorbachev aliyekuwa anaongoza WP wakati huo kuhusu swala hilo. Gorbachev alitaka iwapo zitaungana basi zijitoe katika mikataba hiyo. Hata hivyo baadaye Reagan na Kohr walimshawishi
Gorbschev akakubali Ujerumani iungane na kuwa nchi moja chini ya NATO lakini baada ya muungano huo, NATO isichukue nchi nyingine yoyote ya WP, na pande zote tatu zikakubaliana hivyo.
Mwaka 1991,
Muungano wa Soviets (USSR) ulivunjika, jambo lililosababaisha hata Mkataba wa WP nao kufa. Kufuatia hali hiyo nchi zilizokuwa chini ya USSR zikaanzisha mkataba wao wa ulinzi ulioitwa Collective Security Treaty Organization (CSTO) ambao ulianza na nchi za Armenia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Urusi, Tajikistan na Uzbekistan, baadaye zikafuatiwa na Georgia pamoja na Belarus. Ukraine haukujiunga na CSTO kabisa. Baadaye nchi za Azerbaijan, Georgia and Uzbekistan zilijitoa kwenye hiyo CSTO, na badala yake zikaunda kundi lao la GUAM (Georgia, Ukraine, Azerbaijan and Moldova) ambalo halikutaka kuingiliwa na Urusi kwa namna yoyote; na hata lugha yao ya mikutano walikataa kutumia kirusi bali wakawa wanatumia kiingereza. Hatua hiyo ya nchi hizo kukataa kuwa chini ya influence ya Urusi ndicho kilichoiudhi Urusi, siyo kwa sababu ya NATO hata kidogo. Serikali ya Urusi ilipoanza kuwa hostile kwa nchi hizo za GUAM vitisho vya namna hiyo vikazifanya nchi hizo na nyingine zinazopakana na Urusi kutafuta uanachama wa NATO. Utaona kuwa Urusi ilishazishambaulia nchi hizo za GUAM moja baada ya nyingine lakini haikuwahi kuzishambulia Latvia, Lithuania au Estonia zilipoomba kuwa wanachama wa NATO na baada ya muda wakakubaliwa. Ilishaishambulia Georgia, Azerbaijan (kupitia Armenia), Ukraine kwa mara tatu sasa na kwenye plani yao ya vita iliyovujishwa na rais wa Belarus ilionyesha kuwa walikuwa pia na mpango wa kusihambulia Modova; yaani nchi zote za GUAM!
Hiyo ndiyo historia halisi kwa ufupi, usilishwe propaganda za Putin nawe ukaona ni haki watu wa Ukraine kuuwawa bila hatia yoyote. Baada ya USSR kufa, WP nayo ilikufa, hivyo hakuna mkataba wowote au makubaliano yoyote yaliyosema kuwa nchi zilizokuwa chni ya WP zisikubaliwe kuwa chini ya NATO; in fact ni nchi zenyewe zinazoomba kuwa wanachama, hawalazimishiwi na NATO. Makubaliano baina ya Gorbachev na Reagan/Kohr yalikuwa ni kati ya NATO na WP ambayo haipo tena leo hii.