Binafsi natamani sana Yanga atolewe, tena atolewe kwa goli si chini ya 3.
Tatizo ni kwamba Yanga wamekuwa na kikosi chenye motisha ya hali ya juu na wameshafanya maajabu yasiyotegemewa si mara moja.
Kufika fainali shirikisho, kumpiga CRB 4, Kutoa droo na Sundown si mambo tuliyoyategemea.
Tuwaombee mabaya hawa vyura wapigwe baraaa baraaa hiyo ijumaa ila tujiandae na kelele iwapo maombi hayatatimia na wakapita.
Ukijiaminisha hawapiti halafu wakapita unaweza taniwa kawaida tu na mzee mwenzako mwanayanga ukajikuta umetoa lugha chafu mbele ya vijana wadogo wanaokuheshimu.