Tanzania hatuna wachekeshaji bali tuna waropokaji, wengi ni kinyaa kuwatazama

Wachekeshaji wapo ila hii sanaa imevamiwa na watu wenye njaa kali lengo lao wapate vijitangazo vya kwenye Instagram wapate pesa ila hawana vichekesho vinavyo weza dumu miaka kadhaa mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
List yangu ya wachekeshaji (1)Msukuma akiwa bungeni(2)Muroto akiwahoji watuhumiwa na kuwahukumu live mbele ya wahandishi wa habari(3)Bashite akiangua kilio kanisani.
 
Bongo hatuna Burudani zenye hadhi ya ubora wa kimataifa kupitia waburudishaji wetu. na hii ni kwasababu hatupeendi kuvifuatilia tusivyovijua matokeo yake ubunifu imekua ziro.
in short commedy bongo bado ni kwaajili hasa ya watoto na wanawake wachache wasiokuwa na majukumu kamili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio uwezo walio nao na hapo ndipo walipofikia, sasa wafanyeje?
 
Kamtafute mtu anaitwa Deogratius wa cheka tu ndo utajua wapo au hawapo jamaa talented sana.
Huyo pipipili hamna kitu.

Mr Romantic

Pilipili ninachoona kazi yake ni kutusi watu na kujisifia kuwa ana PRADO basi. Deogratius namkubali sana. Wenzetu wa Kenya wapo mbali sana. Uganda yupo mmoja anaitwa Salvador huyo ni mkali sana.
 
Kuna Pastor kuria "Man Kushi", Mammito, profesa Hammo, Tricky Sana.... nawakubali sana jamaa wa churchil show
 
Kweli kabisa Kiongozi Jamaa wale ni talented sana halafu ni wabunifu sana..wametuletea ladha mpya ya komedi tofauti na ile tuliyozoea (mf. Bambo, Kingwendu, kiwewe n.k).Comedians wengi bongo ni wapiga zumari tu hamna kitu.
Hao jamaa wa Jambo na Vijambo wapo Chennel gani asee? Muda gani? Zamani nilikuwa nawaangalia EATV, Sasa siku hizi siwaoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafiki pembeni, wale jamaa wa "JAMBO NA VIJAMBO" Wanajua sana. Kibongobongo nawakubali sana wale raia.....Kwa malegendari, Joti yupo juu.

Kinachowabeba jamaa ni ubunifu pamoja na kipaji cha hali ya juu kila mtu akiuvaa uhusika fulani anaweza kuutendea kazi mfano jamaa wa maneno kumi akiwekwa avae uhusika wa utoto aisee utacheka utake usitake, bado cha uroho na jamaa mwenye misemo na misamiati anayeigiza mithiri ya Yesu. Hawakulazimishi kucheka ila utacheka tu. Na pia wamebeba maudhui ya kuelimisha jamii pia. Kwa Tanzania hawa jamaa wapo vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…