Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hebu nipe uthibitisho wa hio point namba 2 with facts & figures kuwa ame arrive vipi katika hayo makusanyo?
Nani kakwambia? Kwani wewe ndiyo ulimleta? Kampeni uchwaraKama Taifa hebu tutafakari haya:
1. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayeweza kuongeza kwa mkupuo wanafunzi wapya elfu 29 kwenye HESLB,Simnakumbuka mtangulizi wake yeye ilimchukua miaka mitano ili kufikisha wanafunzi wapya elfu 32 kwenye HESLB,
2. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayekusanya kodi kwa haki kwa wastani wa TZS 1.72 Trilioni kwa mwezi bila ya kukimbiza wafanyabiashara wala kuwadhulumu chochote!!?.
3. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayewahurumia na kuwarejesha shuleni watoto wa masikini waliopata mimba wakiwa shuleni kwa kurubuniwa kwa chips na mserereko?!!
4. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayekuza uwekezaji wa nje FDIs mara sita zaidi kwa miezi sita tu yaani kutoka $510M hadi $3BL!!?.
5. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine kwa miezi saba tu ataongeza hifadhi yetu ya fedha za kigeni kwa TZS 4.4Trilion yaani kutoka $4.8BL mwezi March hadi $6.7BL mwezi September 2021!!?.
6. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayenunua ambulance 395 na magari 214 kwa mkupuo kwaajili ya chanjo wakati mtangulizi wake kwa miaka mitano alinunua ambulance 117 tu bila magari ya chanjo.
7. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayenunua CT SCAN kwenye kila mkoa,Wote mnakumbuka tangu uhuru zilikuwepo CT SCAN mbili tu Tanzania bara na visiwani.!!?
8. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayetununulia MRI kwenye kila hospitali ya kanda nchi nzima sina historia kama tuliwahi kuwa na MRI Machine yeyote kabla ya hizi mpya za mama Samia Suluhu Hassan,
9. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakaye tununulia "Water drilling holes machines " 25 toka mashine moja ya Halmashauri ya Tarime tuliyokuwa nayo,Huyu ni Rais anayekwenda kumaliza shida ya maji kwa vitendo Tanzania.
10. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayetujengea madarasa elfu 15 ya Sekondari na mengine elfu 3 ya Shule za Msingi shikizi, Hii ni Sawa na wastani wa kila shule moja ya sekondari ya Serikali kujengewa madarasa mapya manne (4).
11. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayewapanga Wamachinga wetu kwenye Permanent Premises ili watambulike na kupewa mikopo na huduma nyingine mbalimbali za kibiashara kama Semina na mafunzo kirahisi badala ya kuwatumia kama mtaji wa kisiasa na kuwaacha wakiogelea kwenye Umasikini toka mwaka mmoja wa Uchaguzi na mwingine.
12. Ni lini tena baada ya huyu Tanzania tutampata Samia mwingine atakayefuta wasiojulikana wote,walevi wa madaraka wote na kuwafanya watu waishi kwa Uhuru na kwakujiamini ndani ya nchi yao huku akilifungua Taifa kimataifa.
Nitaendelea na tafakuri yangu
Ngoja tuone hata sabaya alipingaLemma huo utabiri utamuhusu yeye mwenyewe,
CHADEMA mtapata shida sana, Hakuna kama Samia,Mungu aepushie mbali tusijepata tena kirusi kuongoza Taifa letu
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Chadema tena [emoji23][emoji23][emoji23] Unaweza kuwa na Mada Nzuri sana lakini ukiivika siasa unapoteza Uzuri wake [emoji125][emoji125][emoji125]CHADEMA mtapata shida sana, Hakuna kama Samia,
Ni mwanasiasa lakini ajenda za maendeleo ya Nchi hazitaki Siasa,ukanda na Dini hivyo vyote ni sumu kwenye maendeleoKwani Rais Samia sio mwanasiasa siku hizi?
Uko sahihi,Nadhani unajua katika yote uliyoyataja Samia hayupo huko,Ni mwanasiasa lakini ajenda za maendeleo ya Nchi hazitaki Siasa,ukanda na Dini hivyo vyote ni sumu kwenye maendeleo
Itatuchukua muda mrefu sana baada ya Samia kumpata Samia mwingine,Kwani Rais Samia sio mwanasiasa siku hizi?
Asante kwa kauli ya Kizalendo hii,Itatuchukua muda mrefu sana baada ya Samia kumpata Samia mwingine,
Unashida kubwa wewe jamaa,Yote ni upambe nuksi ila hilo namba 2 linastaajabisha na kushangaza!
CHADEMA mmeishiwa kila kituWacha kujichosha kwa hizi post za vichaa wa lumumba mkuu
Shekhee upewe pepsi ya baridi hapo kwa mangi nitalipa MimiNi lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais aliyeshindwa kukusanya kodi halali na kukimbilia kutengeneza tozo za ajabu ajabu?
Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais mpiga dili na mabeberu ambaye ameamua kuua mradi wa bwawa la nyerere?
Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais ambaye ndani ya miezi mitatu ya uongozi wake kumekuwa na mgao wa maji na umeme nchi nzima?
Ni lini baada ya huyu tutampata samia mwingine, Rais asiyeweza kuongoza serikali zaidi ya kudemka na kujilegeza (macho kurembua).
Atleast siishi kwa kulamba mataqo ya wakubwaUnashida kubwa wewe jamaa,
Kama Lumumba mlivyo kosa mwana na maji ya motoCHADEMA mmeishiwa kila kitu
Kama huyu lumumba?Atleast siishi kwa kulamba mataqo ya wakubwa