ABC ZA 2025
JF-Expert Member
- May 2, 2018
- 1,299
- 832
Tutafika tuAgenda ya US$100B kwa nchi masikini baada ya Rais Samia kurejea nchini tutarajie chochote kutoka COP26?
"Hakuna kama Samia "
Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwawajumbe 197 wa baraza la 26 la Uhifadhi wa Mazingira duniani yaani COP26 lililoketi kwa kipindi cha Siku 12 Glasgow nchini Scotland chini ya Rais wake Alok Sharma kwa uenyeji wa UK,
Lengo kuu la mkutano huu wa 26 nililelile tangu mwaka 1994 ambalo ni kujadili kwa pamoja mpango wa EIA na namna ya kuendelea kuipunguza hewa ya ukaa ( Greenhouse gases) kwa 45% ifikapo 2030 ili kulileta Joto katika nyuzi joto 1.5'C za awali kabla ya ujio wa Viwanda kwa kuanzisha " zero carbon solution " ambayo hadi sasa imefikiwa kwa 25% tu duniani kote,
Greenhouse gases au hewa ya ukaa inatokana kwa kiasi kikubwa na kuungua kwa POPs kama Carbon na Sulphur ambazo mara nyingi hutolewa kutoka kwenye moshi wa Viwandani, kwenye magari moshi, magari ya kawaida,mashine mbalimbali za makaa ya mawe et el,
Gesi hii ikifika juu ya anga inaharibu lile blanketi la dunia|ozone layer ( O3 ) kwa kulitoboa matundu ambayo yanaifanya miali ya Jua ipenye kirahisi na kuifikia dunia na hivyo kupandisha Joto la dunia ambalo nalo hubadili karibu kila kitu chini ya uso wa dunia ndio tunasema "mabadiliko ya tabia ya nchi " au Global warming effects
Hoja ya dunia kwa sasa ni kuondoa au kupunguza matumizi ya nishati zote zinazotoa Carbon na Sulphur yakiwemo mafuta aina zote ili kuiepusha dunia na kiama, zaidi ya 50% ya hewa yote ya ukaa inatolewa na China na Marekani,
COP21 iliyofanyika Paris Ufaransa mwaka 2015 wajumbe wote walikubaliana nchi zilizoendelea au zenye kipato cha juu ambazo according to World Bank ziko 81 zitoe pesa kiasi cha $100B karibu TZS 230 trilioni kama LDCF kwa kila mwaka kwa nchi masikini kama Tanzania ili nazo ziweze kukabiliana na mabadiliko ya " Tabia nchi "
Tanzania tunamradi wa kujenga SGR au reli ya Umeme ( Zero carbon project) wa zaidi ya km 1,800 kama tutacheza vizuri na hizi $100BL kama tulivyocheza na zile TZS 1.3trilioni za COVID-19 tunaweza kupata sapoti hii kwani kwa hesabu ya hara karibu kila nchi masikini italamba $1BL au TZS 2.3trilioni za bure kwa kila mwaka kwaajili ya kupambana na mabadiliko ya tambia nchi ambayo SGR ni mradi kipenzi cha "Zero Carbon Solution " hakika Rais Samia ni akili kubwa,
Taarifa hii iwasaidie wasiojua kwanini Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan alikwenda mwenyewe Scotland,
View attachment 1994663
View attachment 1997302
View attachment 1997303
View attachment 1997304
View attachment 1997305
View attachment 1997306
View attachment 1997307
View attachment 1997308
View attachment 1997309