Pre GE2025 Tanzania huwezi kuwa maarufu kisiasa kama hupambani na CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kama unataka kuwa mwanasiasa maarufu Tanzania basi wewe onesha unapambana na CHADEMA.

Kuna wakati Mzee Wasira aliomba kura ndani ya CCM kwa hoja kwamba yeye ndiye mwenye uwezo wa kupambana na CHADEMA, akachaguliwa.

Leo baadhi ya Wana CCM wanamuona Samia Suluhu kama ni Mwenyekiti legelege kwa kuwa tu haoneshi kupambana na CHADEMA.

Tanzania kuna vyama vingi vya Siasa zaidi ya 18 lakini ni CHADEMA pekee ndiyo kila siku inazungumzia.

Hata chawa kikongwe johnthebaptist na mtafuta teuzi Lucas Mwashambwa na kaka yake Pascal Mayalla wanajua.

Kwa mtazamo wa kina CHADEMA ndiyo ramani ya siasa za Tanzania.
 
Anasema Luhanga ana hoja za kichademachadema na akasema kama Mpina Luhanga anataka kujua Magufuli alikufaje basi atoke CCM aende CHADEMA.

Lazima CHADEMA itajwe...😅😅😜

Hata hivyo Mengere hajawa maarufu
Mkuu yule Mengere hapa jijini ni maarufu sana na anasukuma ndinga za bei kali kwa sababu ya kazi yake ya kuwatafutia Mapedeshee pisi za maana na jamaa kazi anaifanya kwa weledi wa juu sana 😂😂😂
 
Kwa Ivo ni "team" mwijaku na baba levo. Unakuwa maarufu kwa mambo ya hovyo hovyo!!!
 
Kama unataka kuwa mwanasiasa maarufu Tanzania basi wewe onesha unapambana na CHADEMA.

Kuna wakati Mzee Wasira aliomba kura ndani ya CCM kwa hoja kwamba yeye ndiye mwenye uwezo wa kupambana na CHADEMA, akachaguliwa.

Leo baadhi ya Wana CCM wanamuona Samia Suluhu kama ni Mwenyekiti legelege kwa kuwa tu haoneshi kupambana na CHADEMA.

Tanzania kuna vyama vingi vya Siasa zaidi ya 18 lakini ni CHADEMA pekee ndiyo kila siku inazungumzia.

Hata chawa kikongwe johnthebaptist na mtafuta teuzi Lucas Mwashambwa na kaka yake Pascal Mayalla wanajua.

Kwa mtazamo wa kina CHADEMA ndiyo ramani ya Siasa za Tanzania.
Sasa sisi CCM tunapambana na yeyote anayeyaka kuleta machafuko ya kisiasa nchini,Hatupambani na chadema kwa sababu tunawaogopa,ccm inapambana kutunza Amani inayotaka kuvunjwa na masela wa chadema.
 
Kwa ivo vyama vingine kama kile cha Hashim Rungwe hamna haja navyo??

Umewahi kukaa muda gani bila ya kuizungumzia CHADEMA!??
 
Kumbe. Kwa kweli nchi hii upinzani ni chadema tu. Nami nawapongeza sana Chadema kwani wameandaa watu ambao sasa ndio lulu kwa CCM. Hata CCM inajua hilo kuwa vijana makini ni wale waliotengenezwa na Mbowe
 
Adui aliye karibu ndie tunapambana nae,chadema imejitahidi kufikia theluthi ya nguvu ya ccm ndio maana tunapambana nae asipate robo ya nguvu tuliyonayo.
Uzuri umekubali kuwa Chadema ina nguvu. Pambana sana ili wakuone upate kisemeo rasmi.
 
Back
Top Bottom