MoseKing
JF-Expert Member
- Jul 5, 2017
- 4,928
- 8,976
Na Mimi nimemuuliza, huko Kilimanjaro Hakuna MIJINI yeye alitaka hizo huduma.zisiwekwe zisubiri mpaka "MIJINI" ziwepo??Yeye anaongelea vijijin wewe unauliza mjini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Mimi nimemuuliza, huko Kilimanjaro Hakuna MIJINI yeye alitaka hizo huduma.zisiwekwe zisubiri mpaka "MIJINI" ziwepo??Yeye anaongelea vijijin wewe unauliza mjini
Kijiji gani hicho chenye kijana mmoja? japo kuna uhalizia.Ukienda mkoa wa Kilimanjaro utashangaa mambo yafuatayo haya matatizo hayako tu uchagani bali hata upareni yapo
Idadi ndogo ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, huku mikoa mingine wanafunzi wakiwa wengi na wengine wanakaa chini Hali ni tofauti mkoa wa Kilimanjaro idadi ya wanafunzi inazidi kushuka kila miaka inavyozidi kwenda Kuna shule inaandikisha darasa la kwanza wanafunzi 10, Kuna nyingine iliandikisha wa-nne
Nyumba nyingi kuwa empty hili ni tatizo lingine kubwa Kuna idadi kubwa sana ya nyumba hazina watu na ukienda vijijini Hali ndo mbaya Zaid nyumba nzuri nyingine gorofa Ila hazina watu na Hali inakua mbaya pale bibi na babu wakifariki sanasana utamkuta kijana mmoja tu ambaye Yuko kwa ajili ya kuziangalia, vijana kutoka Tanga hasa wasambaa, kutoka singida na manyara wambulu ndo utawakuta wanaangalia zile nyumba nyingi na kulimia migomba
Mfano ukienda upareni ni kawaida sana kuona nyumba imeachwa na kugeuka kuwa kichaka huku manyasi yakiwa yameota ndani huku nyumba ikiwa imebomoka bomoka
Vijiji mkoa wa Kilimanjaro havina watu kama umepanga kwenda kukaa week kwa Ile Hali ya vile vijiji vyao utajikuta umehairisha hakuna watu kabisa yaani in-short mkoa wa Kilimanjaro una ukiwa sio sawa na kipindi tunakua
Changamoto nyingine hakuna vijana Kuna kijiji nilienda kijiji kizima kijana ni mmoja ambaye ni bodaboda wengine waliobaki ni watu wa miaka 40 na kuendelea ni nadra sana kumuona kijana wa miaka 20's
Sawa Mmachame tumekuelewa mbee.Hapa ni moja ya vijiji vya mkoa wa Kilimanjaro, Kijiji cha Oria, Kata ya Kahe... Hapa ardhi hii hawauzi ila wanakodisha, tena kwa msimu, ambapo ekari moja ni sh laki nne... Watu wanajua umuhimu wa ardhi na pia ardhi ni ndogo hivyo hawawezi kuuza na kumnufaisha mwingine. View attachment 2430090View attachment 2430092
Labda hoja yako inaweza kuwa kweli, ila mimi pointi yangu ya mwanzo nilikuwa namjibu jamaa aliyesema Kilimanjaro kuna hali mbaya ya maendeleo ndio inayochangia watu kuhama,Kwasababu mikoa mingi Kuna MIJINI
Pia, Kilimanjaro ni ndogo sana, na udhaifu wa serikali ulivyo wanaofanya maamuzi hawana akili.
Mfano, Kilimanjaro Kuna shule nyingi na zahanati, lakini unashangaa pesa za mgawo wa UVIKO na TOZO wakalazimishwa wajenge Tena madarasa wakati yaliyopo tu hayatumiki yote.
Lakini wangewaacha huru, wangetumia hizo pesa kufanya ukarabati wa majengo mabovu.
Kwa Kilimanjaro, Wilaya moja tu mfano Rombo inalingana na Tarafa mkoa mwingine, kwahiyo usitarajie wakashindwa kuweka umeme mkoa mzima.
Rombo unaweza kuzunguka na pikipiki masaa 6 ukaimaliza yote.
Lakini Wilaya Kama Geita au Mlimba Morogoro huo uwezo haupo leave muda mfupi.
Maendeleo ya kawaida ya kiserikali yapo sana, maana barabara kubwa Zina Rami, ndogo huwa zinalimwa mara kwa mara zipitike.Labda hoja yako inaweza kuwa kweli, ila mimi pointi yangu ya mwanzo nilikuwa namjibu jamaa aliyesema Kilimanjaro kuna hali mbaya ya maendeleo ndio inayochangia watu kuhama,
Ni kweli kijana aliyezaliwa dar hawezi kwenda kijijini kwao kwasababu wazazi wake wanaishi dar na wamejenga dar au mikoa mingine na huyo kijana utakuta kapata kazi mkoani uku wazazi wanaishi dar, kwaiyo kijana akipata likizo lazima ataenda dar sehemu ambayo kazaliwa na kakulia uko na wazazi wake wamejenga na kuishi dar.Hio ndo point yangu na wanapenda December ni wale waliozliwa kule lakin mtu amezaliwa na kukulia dar hauon umuhimu sana wa kwenda kule December wengi wanaenda kwa mkumbo hasa ambao hawajazaliwa kule
Wasukuma wao wana uziana wao kwa wao.Nimetembelea baadhi ya vijiji huko Kigoma, Katavi, Rukwa nk na kukutana na wasukuma wengi sana, vijiji vingine karibia 70 % ni wasukuma. Sasa wakati nawahoji hawa wasukuma nikagundua kwamba wanapotoka huko kwao wanauza kila kitu na kuhamia maeneo mengine, na sababu kuu wao wanasema huko kwao ardhi imechoka, ukame, uzalishaji mdogo nk hivyo kulazimika kukimbilia maeneo yenye mazingira mazuri. Sasa tofauti na watu wa Kilimanjaro ni kwamba wakati wasukuma wanauza miji/ardhi zao na kuhamia kwingine Kilimanjaro wao hawauzi maeneo yao na badala yake wanayaendeleza huku wakiwa nje ya mkoa wao.
Fursa za kiuchumi zipo nyingi tu, sema watu wa kule hawataki kubadilika, maisha yaleyale ya miaka ya 90 ndio wanataka kuishi vile vileMaendeleo ya kawaida ya kiserikali yapo sana, maana barabara kubwa Zina Rami, ndogo huwa zinalimwa mara kwa mara zipitike.
Umeme upo zaidi ya Kaya 90% na maji yapo, japo kiangazi ni mgawo.
Nyumba na ubora wa makazi yapo vizuri nadhani kwa 80%.
Kinachofanya watu wakimbie huku ni ugumu wa maisha, na ukosefu wa fursa za kiuchumi. Hata hao wengi wenye pesa na maendeleo binafsi hawatafutii huku.
Watalima wapi, ardhi kiduchu hiyo.Fursa za kiuchumi zipo nyingi tu, sema watu wa kule hawataki kubadilika, maisha yaleyale ya miaka ya 90 ndio wanataka kuishi vile vile
Mfano miti ya kawaha hadi leo unakuta ipo wanakomaa nayo wakati kahawa haina bei
Zao la parachichi ambalo ni deal siku hizi lina stawi sana kule lakini wachache sana ndio wamelima miche ya kisasa
Ndizi pia ni zao ka biashara lakini wapo na ndizi zile zile za miaka ya zamani
Mahindi pia pale wapo mipakani na Kenya wangelima soko lipo karibu tu
Watu wamehama ardhi nyingi ipo tupu, sema mambo yale yale ya ukale yanawarudisha nyuma, mimi kijijini kwetu majirani karibu 4 kati ya 6 wamehama na mashamba hayatumiki ila kuuza hawauzi wala kukodishaWatalima wapi, ardhi kiduchu hiyo.
Hata ukiweka wastani wa ekari 2 kwa kila mtu, bado haitoshi kilimo Cha biashara.
Kilimanjaro sehemu njingi hakuna mwingiliano wa watuKwahiyo Kilimanjaro hakuna Maisha?
Sensa ya mwaka 2012 Kilimanjaro ilikuwa na watu 1.6, mwaka 2022 wapo 1.8, watu laki mbili tu kwa miaka 10, 2032 itakuwa negativeNice topic, naona wengi wamechangia kwa mazuri, mabaya na changamoto zilizopo.
Kwanza ni declare interest, I am proudly chaga na nakubaliana na mitazamo mingi isipokuwa ile tu ambayo ipo negative na yenye wasiwasi kwa sababu zifuatazo kama ilivyo repotiwa kwenye matokeo yetu ya senza na makazi ya mwaka huu 2022:
1. MVUA: Wengi wameongelea Kilimo lakini takwimu zinaonesha kuwa mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo yenye mvua chache sana so sio rafiki kabisa kwa kilimo. Ukiangalia, Bukoba: 2245.2mm kwa mwaka, Dar es salaam 971.5mm lakini Kilimanjaro ni only 394.3mm kwa mwaka; kumbuka kilimo ndie mwajiri mkuu hapa Tanzania.
2. IDADI YA WATU: Wapo waliosema, idadi ya watu Kilimanjaro imepungua sana, unless kwa maneno machache lakini sensa inasema idadi ya watu inaongezeka kwa wastani mzuri, mwaka 2002 wakazi Kilimanjaro walikuwa 1.4m, 2012 wakawa 1.6m na mwaka huu 2022 sensa inasema wakazi Kilimanjaro ni 2.0m. Ongezeko hili la watu kwa Kilimanjaro ni la wastani at 2.3% (Tanzania 3.1%) hivyo mlio na wasiwasi tulieni na tuendelee kuonana December mgombani
3. UCHUMI: Pamoja na wale waliokuwa na wasiwasi kuhusu viwanda vya zamani kufa, hali ya uchumi kimkoa nayo ni nzuri at TZS 3.6m regional per capital GDP; hii ni hali ya utajiri wa mkoa gawanya kwa idadi ya watu - tukipitwa na mikoa 3 tu i.e. Dar, Ruvuma na Mbeya.
4. UHALIFU: Nimeshangaa tu hali ya uhalifu, ipo juu sana kufikia jumla ya visa 2981, tunapitwa na Ilala pamoja na Kinondoni pekee ambazo ni kama wilaya, tukifuatiwa na Morogoro kwa mbali.
Taarifa zote ni kutoka kwenye reports za TBS 2022
Nawasilisha
Hapana, ukichukulia kiwango cha wakazi waliohesabiwa kutoka mikoa mingine, hilo ongezeko ni very sustainable as wengi sana tumehesabiwa kutoka mikoa mingine kama Dar na MwanzaSensa ya mwaka 2012 Kilimanjaro ilikuwa na watu 1.6, mwaka 2022 wapo 1.8, watu laki mbili tu kwa miaka 10, 2032 itakuwa negative
Maisha Kilimanjaro shughuli kuyapata aise ule mkoa ni wakiume haswaHuko Kilimanjaro watu hawaendi kutafuta maisha
Mkuu mbona Zanzibar ina watu 1.8 na uchumi upo vizuri mzunguko wa pesa ni mkubwa tuSensa ya mwaka 2012 Kilimanjaro ilikuwa na watu 1.6, mwaka 2022 wapo 1.8, watu laki mbili tu kwa miaka 10, 2032 itakuwa negative
Ardhi ndio resource namba moja katika uchumi kusapoti shughuli zingine za kiuchumi ziende. Ukifika katika mji ambao wakazi wake wana masharti ya kichawi na ya ajabu ajabu juu ya ardhi ni ngumu sana kuvutia wawekezaji.Kutokana na utaratibu wa wachagga kutokuuza viwanja kama makabila mengine, maendeleo yamezorota maeneo mengi.
Ukibaki kijijini utaishia kuwa mlevi wa mbege