Tanzania ina waandishi wa habari wazuri sana, vyeti sio tatizo

Tanzania ina waandishi wa habari wazuri sana, vyeti sio tatizo

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Nimeona baadhi ya watu wakishangalia baada ya tetesi kwamba waandishi wa habari kadhaa wamepukutishwa kutoka vyombo kadhaa vya habari kwa madai ya kukosa vyeti vya taaluma, washangiliaji wanaowana waandishi wa habari wengi wa bongo kama machawa zaidi na watu wasio na weledi, hili jambo ni ujinga na kutoelewa chanzo cha tatizo.

Mwaka 2016 kurudi nyuma waandishi wengi wa Tanzania walikuwa wanaonekana mahiri sana kwa sababu ya mazingira ya ufanyaji kazi yao yalikuwa tofauti sana na kuanzia kipindi cha mwaka 2017 mpaka sasa. Tatizo la tasnia ya habari Tanzania sio waandishi bali mazingira ya ufanyaji kazi, wakina Kubenea walikuwa hawana vyeti vya darasani vya uandishi na walikuwa wanaandika vizuri tu, tatizo sio vyeti bali mazingira.
 
Tutalifanyia kazi ila Kwa Sasa bwana kitenge nenda katafute cheti
Screenshot_20240916-154459_1.jpg
 
Kama ni mazingira mkuu, unawazungumziaje waalimu na mazingira yao ya kazi?

Siku moja niko pale sentro, namsikia dada askari mmoja, pisi tu, kavaa nyeupe na daki bluu, analalamika..."akadhani ananikomoa, nikavua zangu mkanda na viatu, nikaingia..akaniweka mpaka usiku ndo akawaambia waniachie..."

Nikasema, kumbe ujanja mwingi kwa raia wema tu...haya mazingira nayo vipi?
 
Labda habari za udaku na umbea

Ova
 
Nimeona baadhi ya watu wakishangalia baada ya tetesi kwamba waandishi wa habari kadhaa wamepukutishwa kutoka vyombo kadhaa vya habari kwa madai ya kukosa vyeti vya taaluma, washangiliaji wanaowana waandishi wa habari wengi wa bongo kama machawa zaidi na watu wasio na weledi, hili jambo ni ujinga na kutoelewa chanzo cha tatizo.

Mwaka 2016 kurudi nyuma waandishi wengi wa Tanzania walikuwa wanaonekana mahiri sana kwa sababu ya mazingira ya ufanyaji kazi yao yalikuwa tofauti sana na kuanzia kipindi cha mwaka 2017 mpaka sasa. Tatizo la tasnia ya habari Tanzania sio waandishi bali mazingira ya ufanyaji kazi, wakina Kubenea walikuwa hawana vyeti vya darasani vya uandishi na walikuwa wanaandika vizuri tu, tatizo sio vyeti bali mazingira.
Kwenye List yangu

1. Sam Mahera
2.Spancer Lameki
3. Ansbert Ngurumo
4. Jenerali Ulimwengu
5. Pascal Mayalla
6. Chahali
7.Kubenea
8. Middle
9. Tido Mhando
10. Ayoub Rioba
 
Kuwa certificate tu si haba! Hii JAB ni upuuzi fulani ulioibuka na kuvuruga mambo. Eti wanataka diploma! kuwa na diploma ni hatua tu ya kusoma na hakuna mtu asiyependa kusoma yanayojiri kwenye taaluma yake kila uchao. Mtu anaweza kusoma zaidi na zaidi hata kama hatatunukiwa shahada lakini akawa na maarifa mengi kuweza kufanya kazi yake. Hakuna kazi ngumu duniani kama unaifanya kwa kuipenda
 
Naweza kuwa na weledi wa kufanya kazi fulani lakini nikawa sina hata cheti cha awali. Ishu hapa si cheti, diploma wala shahada bali ni kwa namna gani naweza kufanya kazi fulani ambayo najua condition na code zake. Haya mambo ya cheti ni upuuzi fulani wa kimapokeo tu unaozima ndoto za watu katika interest zao. Unataka cheti cha nini wakati naweza kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu?
 
Sasa hata nikikupa cheti, diploma na degree uone, kwani utanipa mshahara wa kunitajirisha mimi na kizazi changu? Upuuzi mtupu kuanza kutaka sifa za kijinga
 
Watu wamefanya kazi muda mrefu bila hata hizo sifa, anaibuka mchawi from no where anaanzisha ithibati kwenye taaluma pana kama hii, huu ni wendawazimu. Kama vipi wangechora mstari kuanzia sasa anayeingia kwenye taaluma hii lazima awe na diploma hapa ingekuwa sawa kuliko utaratibu huu wa ku sweep away watu waliofanya kazi hii kwa weledi bila kuwa na diploma
 
Walitoa muda wa kusoma tangu mwaka 2016. Hata kama mtu ni lasaba angekua alishamaliza hiyo Diploma kama kweli anania na kazi husika.
Taaluma nyingi zina udhibiti wake inawezekana kukawa na wanaofanya vizuri na wanaofanya vibaya lakini ni vizuri kuwa na udhibiti wa watu sahihi kwenye taaluma ingawa haiondoi kwamba wanaweza kuwepo watu wachache wazuri kwenye taaluma husika wasiokidhi vigezo.

Erick Shigongo amejiendeleza mpaka degree kutoka Lasaba, wengine kimewashinda nini haswa?

Miaka 9 ni mingi inatosha kabisa kupata sifa stahiki huenda labda wahusika walidhani Jambo hilo haliwezi kutekelezeka.
 
Ila CCM wanajiamini sana aisee ,yaani kuna mambo yanafanyika tena hadi ndani ya mwaka wa uchaguzi hadi mtu unajiuliza mbona hawa jamaa wanajiamini sana , wanategemea nini?

Wanabahati hawategemei kura za raia 😎 vinginevyo wangelikula walikopeleka mboga.
 
Nimeona baadhi ya watu wakishangalia baada ya tetesi kwamba waandishi wa habari kadhaa wamepukutishwa kutoka vyombo kadhaa vya habari kwa madai ya kukosa vyeti vya taaluma, washangiliaji wanaowana waandishi wa habari wengi wa bongo kama machawa zaidi na watu wasio na weledi, hili jambo ni ujinga na kutoelewa chanzo cha tatizo.

Mwaka 2016 kurudi nyuma waandishi wengi wa Tanzania walikuwa wanaonekana mahiri sana kwa sababu ya mazingira ya ufanyaji kazi yao yalikuwa tofauti sana na kuanzia kipindi cha mwaka 2017 mpaka sasa. Tatizo la tasnia ya habari Tanzania sio waandishi bali mazingira ya ufanyaji kazi, wakina Kubenea walikuwa hawana vyeti vya darasani vya uandishi na walikuwa wanaandika vizuri tu, tatizo sio vyeti bali mazingira.
Unatetea ujinga, watangazaji wengi wa redio binafsi hapa Bongo ni mazwazwa tu, hawajuwi chochote kuhusu ethics za utangazaji, mtu anaongea umbea siku nzima na kuchamba wenzake redioni as if yupo mtaani kiasi kwamba mpaka na wananchi nao wamekuwa wajinga, hawapendi habari za maana ila wanataka umbea tu ili nao wakae vijiweni waanze kujadili ili siku iende. Hii nchi inahitaji kunyooshwa haswa.
 
Habari za maana kwako ni kama za ipi??
 
Watu wamefanya kazi muda mrefu bila hata hizo sifa, anaibuka mchawi from no where anaanzisha ithibati kwenye taaluma pana kama hii, huu ni wendawazimu. Kama vipi wangechora mstari kuanzia sasa anayeingia kwenye taaluma hii lazima awe na diploma hapa ingekuwa sawa kuliko utaratibu huu wa ku sweep away watu waliofanya kazi hii kwa weledi bila kuwa na diploma
Hakika, huu ni wendawazimu.
 
Sina uhakika kama tunaishi dunia moja.

Unaweka udhibiti kupata leseni ya kuendesha gari, wakati wazalishaji wa magari wanazalisha yanayojiendesha yenyewe.

Leo sihitaji kupanga foleni kwa saa 4 ili kumuona daktari mwenye ithibati wakati picha ya echo nikiiweka kwenye chatgpt inatoa maelezo ya kina zaidi na kupendekeza suluhisho.

Huu uandishi wa kitanzania hauhitaji ithibati, tenkolojia inawaondoa katika aina ya uandishi na utangazaji wa kisasa.

Dunia ya leo kuhitaji mwenye kiwango fulani cha elimu huku hajawahi kufanya kitu ni kuwaza kikoloni.

Kwa kazi za sanaa kama uandishi, kuweka kigezo cha elimu ni kufikiri kinyumenyume.

Hivi waandishi kama Larry King na Jenerali ulimwengu walisomea wapi? Na nani aliwapa ithibati?

Tido mhando ndio mwenyekiti wa bodi hii, ulikuwa Bbc wakati Charles Hillary akijiunga nanyi, Nani alimpa ithibati? Kufanya kazi hiyo kwa weledi kwa miaka 20 kama kipanya unahitaji uende kufundishwa na mwalimu ambaye maisha yake hajawahi andika story yoyote na kuchapishwa kokote?

Kingine huyo new sherrif in town, kaimu mkurugenzi wa bodi aliwahi kukaa chumba chochote cha habari kujifunza kazi zinavyofanyika?
 
Back
Top Bottom