Tanzania inahitaji chama kipya cha upinzani chenye sera mbadala za kueleweka za kudumu kwa wananchi sio za matukio.
Hivi vilivyopo hakuna hata kimoja chenye sera ya kudumu kinachoeleweka sera zake za kudumu hasa ni zipi.
Hivi vya kwetu havieleweki kabisa vinaenda na matukio tu.
Mfano CCM ikisema kila mtanzania lazima awe na shamba upinzani watakuja mbio kupinga na kutishia kuipeleka CCM Umoja wa Mataifa kwa kulazimisha kila mtu awe mkulima!!!
Lakini ukiwauliza vyama vya upinzani vyote kuwa hivi nyie sera zenu za kudumu ni zipi ambazo vyama vyenu vikitajwa tu mtu anajua yes hii ndio sera ya kudumu ya chama changu?
Ndugu Yehoyada kasema vema. Ni kweli Tanzania tunahitaji vyama vya Upinzani vilivyo madhubuti. Si kama hivi tulivyo navyo.
Binafsi sijaona. Ukiwachunguza kwa makini viongozi wa vyama vya upinzani, ni opportunists wachumia tumbo. Wajanja wajanja tu na wababaishaji. Bila shaka JPM kwa kuwatambua hivyo anawapiga mkwara ili kutekeleza visions zake, maana hawana jipya; Watampotezea muda bure.
Tulikwishawashauri mara nyingi tu; jamani ee, tengenezeni program kabambe ya kujenga na kuimarisha Chama; njooni vijijini, huko vijijini mnakojijenga zaidi, wanachama wenu wengi ni hawa wahuni wapiga debe na madili; wapiga kura tuko huku vijijini! Hawaelewi.
Tena kwa mfano mwaka huu 2020 ndiyo ulikuwa mwaka mwepeesi kuiondoa CCM kwa kupata madiwani na wabunge wengi mpaka JPM angechanganyikiwa. Sasa, Chadema, ACT, NCCR, hawako vijijini kuliko na wapiga kura wengi, kuliko na watanzania wengi wasiofaidi keki ya Taifa lao.
Nawashauri tengenezeni programu ya miaka angalau 20 kujenga na kuimarisha vyama vya upinzani vijijini kwa kuhakikisha mnawekeza ktk rasilimali watu, miundombinu ya ofisi na mawasiliano.
Ona Chadema na Ruzuku yote ile!
Epukeni siasa za ukabila na ukanda. Hamwoni CCM ilivyojijengea ngome vijijini; hamwoni nyinyi akina Mbatia? Nilikupigia simu siku moja kukupa a, b, c za kufanya; ukapuuzia!
CCM inavuna kura vijijini!
Freeman yeye nilikwishamkatia tamaa. Ni brotherman. Lifist mchumia-tumbo, egoist.
Kwa jumla kwa namna vyama hivi vilivyo, itachukuwa miaka mingi mno kuwa kama Marekani au Uingereza.
Namuunga mkono JPM kuvipiga mkwara vyama vya upinzani Tanzania kwani kwa jinsi vilivyo, ukiviendekeza Nchi haiwezi kupiga hatua ya maendeleo. Hovyo kabisa!