Tanzania inahitaji chama kipya cha upinzani chenye sera mbadala za kueleweka za kudumu kwa wananchi sio za matukio

Huna akili wewe
 
Kwa hiyo hakuna mzalendo alie upizani sasa.?
Maana dr slaa ni CCM
Nataka kujua ili Huyo mzalendo tumtumie kuazisha chama cha upizani km hakuna HIYO NDIO SABABU UPIZANI KUUMIZWA NCHI HII MAANA MZALENDO LAZIMA AWE CCM.
Baada ya chadema kuwa mafisadi, madalali na vibaraka uzalendo uliota mbawa
 
Jamaa jinga sijapata kuona...Badala ya kuongelea Tume huru unaleta utopolo...unajua Che alikufa natural death?pathetic
 
Nchi ina miaka 59 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, pesa za viwanda pesa za maendeleo pesa za walipa kodi zinatumika kudidimiza demokrasia kuwabambikia kesi uonevu unyanyasaji uchakachuaji na mambo ya hovyo yasiyo na tija kwa Taifa, CCM haitaki maendeleo kabsa hata tuvimaendeleo kiduchu twa SGR flyover bwawa la umeme tumejaa ufisadi mkubwa kama uliopo kwenye ununuzi wa Ndege mpaka kumtoa CAG kafara kukwepa aibu, CCM ni ile ile hakuna malaika wote wapo after money, ni vigumu Tanzania kupata maendeleo chini ya CCM kwani mda huu Tanzania ilipaswa iwe ni Nchi tajiri kuliko South Africa China America German India UK na mataifa yote tajiri, lakini chini ya CCM hakuna maendeleo zaidi ya kutumia pesa za walipa kodi kurejesha mfumo wa chama kimoja
 
Uzalendo wa CCM ni kuwabambikia kesi kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu

Tunataka rais wabunge na madiwani watakaokua wanawafanyia kazi watanzania... sio wa kuwafanyia kazi wabelgiji, wajerumani wala wamarekani
 
Ungesema tume huru ningekuelewa.au huoni Hilo??
 
Kwa hiyo hakuna mzalendo alie upizani sasa.?
Maana dr slaa ni CCM
Nataka kujua ili Huyo mzalendo tumtumie kuazisha chama cha upizani km hakuna HIYO NDIO SABABU UPIZANI KUUMIZWA NCHI HII MAANA MZALENDO LAZIMA AWE CCM.
Dr slaa alinunuliwa kwa dola milion mbili akawasaliti chadema hana Uzalendo wowote ni kizee fulani cha hovyo sana hakina mfano wa kuigwa hata mmoja
 
Reactions: lum
Tunataka rais wabunge na madiwani watakaokua wanawafanyia kazi watanzania... sio wa kuwafanyia kazi wabelgiji, wajerumani wala wamarekani
Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi angefikaje Belgium?
 

Nashukuru kwa kujua hilo la wazungu kuwa ni mabeberu ni propaganda za wachovu wa siasa. Ndio maana umeshindwa kuweka ubora wa wazalendo uchwara na hao wazungu.

Rais Magufuli hanangwi bali anapewa ukweli mchungu, ambao nje ya humu mitandaoni hakuna mtu anathubutu kufunguka. Akitoka madarakani hakuna mtu atakuwa na muda naye. Tatizo mmejiingiza kwenye kumsifia mpaka mkisikia anapewa ukweli mchungu mnaona kama ananangwa. Pale anapofanya vizuri hamtumsifii maana ni wajibu wake kwani analipwa mshahara na posho nene nene, lakini pale anapochemsha kama huu wizi wa kura alioagiza, mauaji na manyanyaso ya wapinzani tunampa kubwa yake mchana kweupe.
 
Ndugu Yehoyada kasema vema. Ni kweli Tanzania tunahitaji vyama vya Upinzani vilivyo madhubuti. Si kama hivi tulivyo navyo.
Binafsi sijaona. Ukiwachunguza kwa makini viongozi wa vyama vya upinzani, ni opportunists wachumia tumbo. Wajanja wajanja tu na wababaishaji. Bila shaka JPM kwa kuwatambua hivyo anawapiga mkwara ili kutekeleza visions zake, maana hawana jipya; Watampotezea muda bure.
Tulikwishawashauri mara nyingi tu; jamani ee, tengenezeni program kabambe ya kujenga na kuimarisha Chama; njooni vijijini, huko vijijini mnakojijenga zaidi, wanachama wenu wengi ni hawa wahuni wapiga debe na madili; wapiga kura tuko huku vijijini! Hawaelewi.
Tena kwa mfano mwaka huu 2020 ndiyo ulikuwa mwaka mwepeesi kuiondoa CCM kwa kupata madiwani na wabunge wengi mpaka JPM angechanganyikiwa. Sasa, Chadema, ACT, NCCR, hawako vijijini kuliko na wapiga kura wengi, kuliko na watanzania wengi wasiofaidi keki ya Taifa lao.
Nawashauri tengenezeni programu ya miaka angalau 20 kujenga na kuimarisha vyama vya upinzani vijijini kwa kuhakikisha mnawekeza ktk rasilimali watu, miundombinu ya ofisi na mawasiliano.
Ona Chadema na Ruzuku yote ile!
Epukeni siasa za ukabila na ukanda. Hamwoni CCM ilivyojijengea ngome vijijini; hamwoni nyinyi akina Mbatia? Nilikupigia simu siku moja kukupa a, b, c za kufanya; ukapuuzia!
CCM inavuna kura vijijini!
Freeman yeye nilikwishamkatia tamaa. Ni brotherman. Lifist mchumia-tumbo, egoist.
Kwa jumla kwa namna vyama hivi vilivyo, itachukuwa miaka mingi mno kuwa kama Marekani au Uingereza.
Namuunga mkono JPM kuvipiga mkwara vyama vya upinzani Tanzania kwani kwa jinsi vilivyo, ukiviendekeza Nchi haiwezi kupiga hatua ya maendeleo. Hovyo kabisa!
 

Mkuu na wasiwasi kama ulinipata vizuri, CCM kwasasa ni tasisi zote nilizozitaja na ndio zinaipa madaraka, hata ikimaanisha kuptia “uchafuzi

kinachohitajika ni mfumo utakao toa uhuru na haki sawa kwa vyama vyote halali vya kisiasa.

Swala la sera kufaa au kutofaa litapata jibu kutoka kwa wananchi kwa kupitia sanduku za kura zitakazoratibiwa na TUME HURU na ya HAKi ya uchaguzi.

kwa maneno mengine huwezi jua nguvu ya sera za chama chochote cha siasa kwa wananchi kupitia sanduku la kura bila ya kuwa na tume huru na ya haki ya uchaguzi.
 
Hupati uteuzi ng’oo kwa kuandika huu ujinga wenu, kama wapinzani ni Dhaifu iweje CCM kuwabambikia kesi kesi kuwapiga risasi uonevu unyanyasaji uovu mateso manyanyaso kibao kwa wapinzani? Wewe ndiyo hovyo kabsa maendeleo gani yanaletwa na CCM kwa kudidimiza demokrasia?
 
CCM bila Polisiccm bila Tumeccm bila mahakamaccm bila wakurugenziccm bila Msajiliccm ni weupe sana


Ulisahau bila jeshi la kukodi kutoka Burundi ni weupe sana
 
Wananchi wanazielewa sera za wapinzani ndiyo maana wamewachagua kwa kuwapa kura nyingi lakini CCM kwa kutumia Polisiccm NECCCM Tumeccm na wakurugenziccm imepora haki zao na kuisimika CCM ikulu kienyeji pasipo idhini ridhaa ya wapiga kura
 


CCM inavuna kura vijijini kwa hali hii ??


Your browser is not able to display this video.
 
Hicho chama mwanzilishi wake awe nani.? Au ni hawa hawa wapinzani tulionao.?
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…