Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Halafu mbaya sana wanajaribu kumufitinisha rais na wasukuma ambao ni wapiga kura walio wengi zaidi kuliko kabila lolote.
Ni kweli tuko wengi na pia wanatulazimisha tukae mkao wa kikabila,wakiendelea hv watashangaa 2025
 
Mama anatakiwa asome na kudadisi sana ili ajiridhishe kuwa wateule anaoletewa majina yao wanatosha kwa nafasi watakazopewa na pia kumsaidia yeye kutimiza malengo yake kama kiongozi mkuu. Ukweli usemwe tu, mtangulizi wake alimzidi hapo, kwenye kumakinika, kusoma na kukagua yale anayopelekewa kabla ya kutia kidole chake
 
Tatizo liko wapi? si ametengua kabla hajaapa? Na inawezekana hata anaweza akawa badilisha hata kabla hawaja apishwa SHIDA IKO WAPI Mkuu.
Shida siyo panga pangua, kateua yeye mwenyewe halafu kabla ya kuapisha mteule anatengua Tena!! Is this right?
 
naona tunazidi kuongezeka kwa kasi tuliposema hakuna rais hpo ...mimi siku ya kwanza tu baada ya jiwe kufariki niliamini hatuna rais sema sheria zetu tu ndizo zilizotupelekea kufika hpa tulipo
Ufarisayo huo
 
Mama anatakiwa asome na kudadisi sana ili ajiridhishe kuwa wateule anaoletewa majina yao wanatosha kwa nafasi watakazopewa na pia kumsaidia yeye kutimiza malengo yake kama kiongozi mkuu. Ukweli usemwe tu, mtangulizi wake alimzidi hapo, kwenye kumakinika, kusoma na kukagua yale anayopelekewa kabla ya kutia kidole chake
Kama kwenye korosho
 
Hizi teuzi hata wanaoteuliwa hawataamini kuwa wameteuliwa labda upite mwezi,kwa maana unateuliwa asubuhi na jioni unatenguliwa, kabla hata soda ya kujipongeza hujaimaliza mara unasikia radioni kuwa kuwa umetenguliwa, hata soda unaanza kuichukia.
 
Mleta mada nikuulize yule Mkuu wa wilaya aliyeteuliwa enzi za mwandazake akafika hadi ukumbini kwa ajili ya kula kiapo na muda mfupi akatolewa kwamba sio yeye je ulimwanzishia uzi? Au umeona kuwa sasa uko huru hata kutaja majina ya watu humu jukwaani tena kwa kijinasibu kuwa unajiamini? Leta hiyo thread humu nijue una msimamao tangu mwanzo.
Absolutely Rubbish....!!!!
 
Rais ana majukumu mengi hivyo kutimiza yote bila kuwa na wasaidizi wenye weredi kutakuwa hakuna tija ndio maana teuzi zipo na zinazingatia sheria zote

Kitendo cha kumsema mzee JK kuwa ndo anashika kalamu bila ushaidi huu ni uzandiki mkuu mbona kipindi Mzee JPM alipokuwa karibu sana na hayati BWM hukuja na uzi wa kumshauri? Leo Mama pia kafanya lile lile kama la JPM kuwa karibu na BWM yeye kawa karibu na Jk sasa ndo imekuwa udwazi?
Neno lako la 'Weredi' BAKITA wanalijua?
 
anzania ya sasa inahitaji Rais ambaye haishii tu kuwa Mchapakazi bali pia mwenye uwezo wa Kufuatilia Jambo, Kusoma sana, Kujiridhisha na kuwa na Timu ya Wasaidizi ( Washauri ) wenye Akili hasa na siyo Wapumbavu wenye ' Uchawa ' mwingi.
Sihitaji kusoma hadi huko chini.

Mada yako yote inaanzia na kuishia hapa, kwenye huo mstari mmoja na nusu.

Bila ya shaka yoyote ile, bado rais huyo hayupo kwa sasa hapa Tanzania, na wala sijui tutampata vipi!

Sasa basi, kwa vile tunaye huyu tuliye naye kwa sasa, ambaye najua hana sifa hizo kamwe, tumsihi atumie muda wake kwa mambo machache anayoyaweza vyema, mawili matatu kwa miaka minne inatosha kabisa.

Je, baada ya hapo atapatikana mwenye hayo yaliyopo kwenye mstari na nusu?
 
I'm very worried na uwezo wa mama wa kufuatilia mambo, kama wasaidizi wake watakuwa si wazalendo, mama atakuwa anaingizwa chaka several time.
MAMA SHOULD BE PAYING ATTENTION TO THE DETAILS, AKILI ZA KUAMBIWA ACHANGANYE NA ZAKE. JAKAYA NI JANGA LA KITAIFA, ALISABABISHA NCHI HII KUIBWA SANA.
Werevu tumekuelewa pakubwa mno tu.
 
Back
Top Bottom