Tanzania inahitaji Rais Dikteta mwenye Maono ili iendelee

Tanzania inahitaji Rais Dikteta mwenye Maono ili iendelee

Watanzania hatujielewi tupo hovyo sana mawazoni mwetu. JPM alikuja na huo udikteta tukaanza maongezi ya kwamba nchi hii inahitaji zaidi taasisi zinazofanya kazi.

Amekuja SSH na kusikiliza maombi ya hao wanaotaka taasisi na tumeanza tena kulia tukimdai rais dikteta!!. Tupo hovyo sana vichwani.
Watanzania hawajuwi wanataka nini

Ova
 
Hakuna dikteta asiye katili, hajawahi kuwepo. At some point lazma atawanyoosha wapuuzi puuzi
 
Hiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha! Tulivyokutwa na yale ya 2015-2021, bado tu kuna watu nchi hii wanaendelea kuutomasa-tomasa udikteta.
 
Upumbavu mtupu mnaongea nyie.
Huyo dikteta aliyepita alifanya nini cha maana zaidi ya visasi na kuua wapinzani?

Tanzania inahitaji viongozi watakaofuata sheria na wananchi wenye akili na ujasiri wa kuwawajibisha viongozi wasiofaa, sio dikteta, Uganda inaongozwa na Dikteta ina kipi cha maana?
Ikiwa mstari wa mwisho umeshindwa kuusoma
Huna hoja huu ni upumbavu zaidi
Huyo Museveni na Magufuli ni walewale mbona hutoi mfano angalau kwa Gadaffi
 
Demokrasi was not for African countries. Hasa hizi zetu zilizojaa Uswahili. Angalia nchi ambazo zilipata kukaliwa na waarabu. Zilizoendelea zimeendelea kwa mkono imara wa chuma not Demokrasia.

Angalia nchi za Kiarabu ambazo zimeendelea, zinatawaliwa kwa sheria kali sana. Nchi hii imeharibika kwa sababu tumeifanya siasa kuwa ni maneno maneno ya mipasho na utendaji zero.

Kuna watu unashangaa wanaogopwa. Wanaogopwa na serikali? Tumekuwa na maneno maneno kwa miaka mingi. Anatakiwa Rais shujaa mwenye maono ambaye ataipeleka nchi kwenye uelekeo sahihi.

Kuna watu unaambiwa wakiguswa nchi itayumba. Unawaza nchi itayumbaje? Mimi nawaambia nchi hii italiwa sana na wachache wengi wataendelea kuteseka. Mpaka apatikane Rais katili wa maendeleo ambaye hatoacha watu wajilie watakavyo.

Wavivu ni wengi asilimia 70 na hawa ndo ambao wanataka waishi kiujanja ujanja tu. Kiwizi wizi na kifisadi. Ukiwapa mazingira ya kuchapa kazi wanakuchukia. Imagine mtu hataki kusoma. Ila anataka aje apate kazi kwa cheti feki.

Ukimfukuza kazini anakuchukia anakuona wewe katili. Ila ukimwambia nenda shule anakuona wewe pia hufai unamletea Elimu za Kigeni zisizofaa kwake. Mtu huyo unamwachisha kazi. Humfungulii mashtaka bado anapata ujasili wa kudai alipwe mafao? Hii inatokea katika nchi ambazo ni shit holes tu. Hawa walipaswa wafunguliwe kesi.

Anyway, mtakuja wenyewe kujitetea mi nimesema yangu tayari. Nimepasua jipu.
Udikteta Afrika kwa sasa hauwezekani tena kwa sababu kwenye kipindi hiki resources za dunia nzima almost zimebaki Afrika tu na huko kwingine tayari tulisha-exhaust. Kwa hiyo unapokuwa tuseme unatawala Tanzania, mataifa ya magharibi nayo yanakuwa yanakuangalia pia kwa sababu na yenyewe yanakuwa yana mahitaji yake kutoka kwako. Unless uwe dikteta unayeshirikiana na mataifa yenye nguvu, na si kivyako vyako. Kwa sasa dunia haina resources sehemu zingine isipokuwa Afrika possibly na middle east
 
Sikubaliani na wanaoomba utawala Kama wa jiwe urudi. Hawa wana yao nyuma ya maombi yao.

Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba jiwe alikuwa full dictator wakati huyu aliyepo madarakani ni full laissez faire. Hatujapata mtu akaonesha uongozi.madhubuti kwa kufuata Sheria
Nadhani huyo mwenye misimamo ya katikati hawezi kupatikana kutokana na malengo ya kiuchumi ya wakati husika.

Huyu kaamua kuwa mpole ili asiwakere wafanya biashara na sifa ya TZ kimataifa iwe ni ile ile. Kumbuka huwa anasafiri na huko anataka taswira yetu kwa wao iwe ni ile ile yenye ustaarabu ndani yake.
 
Tanzania tunataka Rais anayefuata Sheria basi
Hakuna Cha dikteta Wala Nani, Dikteta anaweza kuwepo akawa Hana lolote, atafanya kuua na kufunga wapinzani wake kwa kisingizio Cha kupambana na rushwa huku akifuga mafisadi wake ambao anawaona ni loyal kwake
 
Mambo ya kiongozi mkali au mpole ni porojo tu za wanasiasa na akili duni. Nchi hij ina katiba na sheria, kiongozi anachopaswa kusimamia ni katiba na sheria za nchi kwa uaminifu bila double standards. Kuwa mkali au mpole haituhusu sana sisi raia kwani haongozi familia yake bali nchi.
Nadhani huyo mwenye misimamo ya katikati hawezi kupatikana kutokana na malengo ya kiuchumi ya wakati husika.

Huyu kaamua kuwa mpole ili asiwakere wafanya biashara na sifa ya TZ kimataifa iwe ni ile ile. Kumbuka huwa anasafiri na huko anataka taswira yetu kwa wao iwe ni ile ile yenye ustaarabu ndani yake.
 
Tunahitaji Rais mzalendo mwenye uchungu na nchi yake, asiwe kaburu awe mnyenyekevu Kwa Katiba aliyoapa kuilinda. Akikemea rushwa na ufisadi ukimuangalia usoni unasema yes huyu ndiye. Asiwe dikteta bali awe Rais wa vyama vyote.
Huwezi kuwadhibiti wabadhirifu/mafisadi bila kuonekana dikteta.
 
Tutampeleka course Marekani aone jinsi gani wabadhirifu na mafisadi wanadhibitiwa bila Rais kuonekana dikteta.
FBI, DEA, Justice department na taasisi nyingine zinafanya kazi zao vizuri kabisa bila hata maelekezo au jina la Biden kutajwa.
Huwezi kuwadhibiti wabadhirifu/mafisadi bila kuonekana dikteta.
 
Hivi mafuta kwa wingi duniani NATURALLY yanapatikana wapi, ukiacha yale ambayo yako yamehifadhuiwa kwenye stock tayari?
Kupatikana kwa mafuta hakukuletwa na madikteta bali watu wenye akili timamu ya kuendeleza dunia na nchi zao.
 
Gaddafi na Libya ni Waarabu, Kama ni mifano ya Africa tutor ya Africa,
Libya ni Afrika sijui unaongelea Afrika ipi nyingine lakini hata kama iko ulaya kama unavyodhani basi natamani Tanzania ingepata angalau dikteta wa aina hiyo

Nikwambie labda upinzani hawana cha ziada cha kutusaidia upinzani ukishika hatamu huwenda mambo yakawa mabaya zaidi
Magufuli amewasanua watu kwamba ukiwa mamlakani unaweza kufanya lolote na hakuna wa kukufanya lolote hiyo ndiyo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi kwa sasa
Na itazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi huko mbele
Dawa siyo katiba mpya, katiba mpya itasaidia kwa uchache sana tofauti na matarajio ya wengi hii ni Afrika
Rais anashtakika lakini bado hutakuwa na hiyo power
Kinachotakiwa tumpate mtu kama Nyerere mwenye udikteta kiwango cha Magufuli
 
Eti "tunahitaji dikteta" !! Nonsense !!

Nani anakwambia ni lazima dikteta awe na maono mazuri(vision for progress).

Kinachotakiwa ni KATIBA MPYA iliyoambatana na

1. Mipango mizuri ya maendeleo

2. Mfumo wa uwajibikaji
kama kwenye hizo nchi ambazo hata rais akifuja pesa za nchi anafilisiwa na kufungwa

3. Vyombo vya kutoa haki ambavyo havitamlinda mtu yeyote hata kama ni mkuu wa nchi. Yaani VISIWAJIBIKE KWA MKUU WA NCHI AU WAZIRI YEYOTE.

4. Mfumo wa kuwapa wapinzani uhuru wa kutoboa ukweli kuhusu mapungufu wanayoyaona

5. Mfumo wa tume ya uchaguzi ilio huru isiyosimamiwa na chama tawala

6. Bunge ambalo linapatikana kwa uchaguzi ulio huru na haki, na linaloweza kuwajibisha serikali

Tofauti na haya mambo yote niliyotaja, bado Tz itaendelea kuwa maskini pamoja na rasilimali zoooote tulizo nazo (ambazo zinatuwezesha kuwa DONA KANTRE)
 
Libya ni Afrika sijui unaongelea Afrika ipi nyingine lakini hata kama iko ulaya kama unavyodhani basi natamani Tanzania ingepata angalau dikteta wa aina hiyo

Nikwambie labda upinzani hawana cha ziada cha kutusaidia upinzani ukishika hatamu huwenda mambo yakawa mabaya zaidi
Magufuli amewasanua watu kwamba ukiwa mamlakani unaweza kufanya lolote na hakuna wa kukufanya lolote hiyo ndiyo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi kwa sasa
Na itazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi huko mbele
Dawa siyo katiba mpya, katiba mpya itasaidia kwa uchache sana tofauti na matarajio ya wengi hii ni Afrika
Rais anashtakika lakini bado hutakuwa na hiyo power
Kinachotakiwa tumpate mtu kama Nyerere mwenye udikteta kiwango cha Magufuli
Hivi upinzani walishawahi tawala Tanzania ukaona faida yake au hasara yake??Kwa nini mnaona upinzani kama adui wenu wa maendeleo Tanzania?Jaribu kufananisha maisha kabla ya 1992 na maisha ya sasa ambako kuna mfumo wa Vyama Vingi nini kimeongezeka au kupungua?
 
Demokrasi was not for African countries. Hasa hizi zetu zilizojaa Uswahili. Angalia nchi ambazo zilipata kukaliwa na waarabu. Zilizoendelea zimeendelea kwa mkono imara wa chuma not Demokrasia.

Angalia nchi za Kiarabu ambazo zimeendelea, zinatawaliwa kwa sheria kali sana. Nchi hii imeharibika kwa sababu tumeifanya siasa kuwa ni maneno maneno ya mipasho na utendaji zero.

Kuna watu unashangaa wanaogopwa. Wanaogopwa na serikali? Tumekuwa na maneno maneno kwa miaka mingi. Anatakiwa Rais shujaa mwenye maono ambaye ataipeleka nchi kwenye uelekeo sahihi.

Kuna watu unaambiwa wakiguswa nchi itayumba. Unawaza nchi itayumbaje? Mimi nawaambia nchi hii italiwa sana na wachache wengi wataendelea kuteseka. Mpaka apatikane Rais katili wa maendeleo ambaye hatoacha watu wajilie watakavyo.

Wavivu ni wengi asilimia 70 na hawa ndo ambao wanataka waishi kiujanja ujanja tu. Kiwizi wizi na kifisadi. Ukiwapa mazingira ya kuchapa kazi wanakuchukia. Imagine mtu hataki kusoma. Ila anataka aje apate kazi kwa cheti feki.

Ukimfukuza kazini anakuchukia anakuona wewe katili. Ila ukimwambia nenda shule anakuona wewe pia hufai unamletea Elimu za Kigeni zisizofaa kwake. Mtu huyo unamwachisha kazi. Humfungulii mashtaka bado anapata ujasili wa kudai alipwe mafao? Hii inatokea katika nchi ambazo ni shit holes tu. Hawa walipaswa wafunguliwe kesi.

Anyway, mtakuja wenyewe kujitetea mi nimesema yangu tayari. Nimepasua jipu.
Pindua then tawala wewe una uchungu Sana na Tanzania watawala waliopo au wapya wakiingia watakuja kukupa pesa bila kufanya Kazi?

Uongozi unatakiwa kuwa neutral sio udicteta au democracy.

Kiongozi anatakiwa kuwa neutral

Mwisho wa siku madicteta wote duniani wako wapi?

Amebaki Kim, Kagame na Putin hata mseveni kashaacha udicteta
 
Back
Top Bottom