Tanzania inahitaji Rais Dikteta mwenye Maono ili iendelee

Tanzania inahitaji Rais Dikteta mwenye Maono ili iendelee

Libya ni Afrika sijui unaongelea Afrika ipi nyingine lakini hata kama iko ulaya kama unavyodhani basi natamani Tanzania ingepata angalau dikteta wa aina hiyo

Nikwambie labda upinzani hawana cha ziada cha kutusaidia upinzani ukishika hatamu huwenda mambo yakawa mabaya zaidi
Magufuli amewasanua watu kwamba ukiwa mamlakani unaweza kufanya lolote na hakuna wa kukufanya lolote hiyo ndiyo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi kwa sasa
Na itazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi huko mbele
Dawa siyo katiba mpya, katiba mpya itasaidia kwa uchache sana tofauti na matarajio ya wengi hii ni Afrika
Rais anashtakika lakini bado hutakuwa na hiyo power
Kinachotakiwa tumpate mtu kama Nyerere mwenye udikteta kiwango cha Magufuli
Umeongelea Libya kama mfano mzuri wa Maendeleo Afrika kwa sababu ya Udikteta wa Gaddafi,Je udikteta wa Gaddafi uliisaidiaje Tanzania na Bara nzima la Afrika kuanzia kijamii,kielimu,kisiasa,kiuchumi,kimiundombinu,kiteknolojia,kiutamaduni na mipango ya baadaye ?
 
Tatizo sio demokrasia kwani Rwanda wamefika wapi pamoja na udikiteta wake? Uganda je? What about Zimbabwe?
Sudani?
Demokrasi was not for African countries. Hasa hizi zetu zilizojaa Uswahili. Angalia nchi ambazo zilipata kukaliwa na waarabu. Zilizoendelea zimeendelea kwa mkono imara wa chuma not Demokrasia
 
Pindua then tawala wewe una uchungu Sana na Tanzania watawala waliopo au wapya wakiingia watakuja kukupa pesa bila kufanya Kazi?

Uongozi unatakiwa kuwa neutral sio udicteta au democracy.

Kiongozi anatakiwa kuwa neutral

Mwisho wa siku madicteta wote duniani wako wapi?

Amebaki Kim, Kagame na Putin hata mseveni kashaacha udicteta
Fata sheria, kuwa mwadilifu, tenda haki. Basi maendeleo wananchi wanajiletea wenyewe
 
Libya ni Afrika sijui unaongelea Afrika ipi nyingine lakini hata kama iko ulaya kama unavyodhani basi natamani Tanzania ingepata angalau dikteta wa aina hiyo

Nikwambie labda upinzani hawana cha ziada cha kutusaidia upinzani ukishika hatamu huwenda mambo yakawa mabaya zaidi
Magufuli amewasanua watu kwamba ukiwa mamlakani unaweza kufanya lolote na hakuna wa kukufanya lolote hiyo ndiyo imepelekea hali kuwa mbaya zaidi kwa sasa
Na itazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi huko mbele
Dawa siyo katiba mpya, katiba mpya itasaidia kwa uchache sana tofauti na matarajio ya wengi hii ni Afrika
Rais anashtakika lakini bado hutakuwa na hiyo power
Kinachotakiwa tumpate mtu kama Nyerere mwenye udikteta kiwango cha Magufuli
Libya ni Waarabu sio weusi, wapo Afrika kijiografia tu Ila kiasili ni Waarabu ndio maana hata Morocco walijitambua Kama Waarabu japokuwa wapo Africa

Na sijasema habari za upinzani Wala Katiba mpya hapa, nilichosema anatakiwa rais anayefuata Sheria.
Sheria hata zilizopo zikifuatwa vizuri ubadhirifu unaondoka kwa kiasi kikubwa
Madikteta ni matapeli tu wanaojifanya kuongea kwa kufoka ili waonekane wazalendo kumbe wezi na malaya
 
Hayo maendeleo yatakuwa ya nani Kama huyo dikteta ataua watu??, Unajua tafsiri halisi ya dikteta? Au ndio unaufananisha udikteta ucharwa wa awamu ya 5 kuwa ndio udikteta??. Acha kabisa kuombea kitu kinachoitwa udikteta!!.
 
Ni kwer kabisa, nashangaa watu ety ooh tunahtaji raisi mwenye utu mzalendo sjui anaejali watu wake ambae hajashiba madaraka😝😝hivi unazan kuwa na madarka kitu kirahisi mda huo kuna watu walkuwa viongozi drsn shule ya msingi na wakaona wamemaliza maisha sembuse nchi yote yakoo imagine uko na ka milioni 20 tu ndani hakana kazi huwa unajiskiaje?

Pesa na madaraka vina gharama zake hatuhitaji raisi mwenye huruma anatakiwa awe na akili bhan ata kam ni dekteta lkn tuone mafanikio watu wana relax makazini hawana ata hofu raisi anataka kuonekana mwema kwa watu

Hahitajiki rais katili, inahitaji katiba bora, hizi katiba zinasema rais hashitikiwi, sijui spika hashitikiwi akifanya makosa haziwezi kumaliza matatizo yetu zaidi ya kutuwekea walevi wa madaraka. Inatakiwa kila mtu awe chini ya sheria na sio mambo ya amri toka juu.
 
Hatuhitaji DIKTETA...

Tumeongozwa na Dikteta Magufuli tumeona alivyokuwa anaendesha nchi kwa kadiri atakavyoamka..

Ametengenezea watu wengi kesi za hovyo hovyo..

Tunahitaji katiba bora.. Kusiwe na muingiliano wa kimajukumu
 
Mkuu Chukua fomu mimi ntaunga Mkono Juhudi, JF kutoa Rais wa JMT inawezekana, wapo wengi humu wana uwezo wa kuliongoza Taifa hili, ILA SIO WEWE MKUU we unaonekana una KISIRANI
 
Hatuhitaji DIKTETA...

Tumeongozwa na Dikteta Magufuli tumeona alivyokuwa anaendesha nchi kwa kadiri atakavyoamka..

Ametengenezea watu wengi kesi za hovyo hovyo..

Tunahitaji katiba bora.. Kusiwe na muingiliano wa kimajukumu
Udiktekta upi wake,ulishawahi kulala saa 12 jioni

Ova
 
Udiktekta upi wake,ulishawahi kulala saa 12 jioni

Ova
Siongelei kulala saa 12 jioni..

Huyo mtu wenu alijiona anajua kila kitu mwenyewe na kukataa maagizo mengi ya wataalam...
Na ndio maana alikosana mno na Gavana Benno..

Huwezi kuwa na hiko cheo ukajidai unajua kila sekta.. Na ukajifanya eti wewe ni final
 
Back
Top Bottom