Tanzania inahitaji Rais Dikteta mwenye Maono ili iendelee

Umeongelea Libya kama mfano mzuri wa Maendeleo Afrika kwa sababu ya Udikteta wa Gaddafi,Je udikteta wa Gaddafi uliisaidiaje Tanzania na Bara nzima la Afrika kuanzia kijamii,kielimu,kisiasa,kiuchumi,kimiundombinu,kiteknolojia,kiutamaduni na mipango ya baadaye ?
 
Tatizo sio demokrasia kwani Rwanda wamefika wapi pamoja na udikiteta wake? Uganda je? What about Zimbabwe?
Sudani?
Demokrasi was not for African countries. Hasa hizi zetu zilizojaa Uswahili. Angalia nchi ambazo zilipata kukaliwa na waarabu. Zilizoendelea zimeendelea kwa mkono imara wa chuma not Demokrasia
 
Fata sheria, kuwa mwadilifu, tenda haki. Basi maendeleo wananchi wanajiletea wenyewe
 
Libya ni Waarabu sio weusi, wapo Afrika kijiografia tu Ila kiasili ni Waarabu ndio maana hata Morocco walijitambua Kama Waarabu japokuwa wapo Africa

Na sijasema habari za upinzani Wala Katiba mpya hapa, nilichosema anatakiwa rais anayefuata Sheria.
Sheria hata zilizopo zikifuatwa vizuri ubadhirifu unaondoka kwa kiasi kikubwa
Madikteta ni matapeli tu wanaojifanya kuongea kwa kufoka ili waonekane wazalendo kumbe wezi na malaya
 
Hayo maendeleo yatakuwa ya nani Kama huyo dikteta ataua watu??, Unajua tafsiri halisi ya dikteta? Au ndio unaufananisha udikteta ucharwa wa awamu ya 5 kuwa ndio udikteta??. Acha kabisa kuombea kitu kinachoitwa udikteta!!.
 

Hahitajiki rais katili, inahitaji katiba bora, hizi katiba zinasema rais hashitikiwi, sijui spika hashitikiwi akifanya makosa haziwezi kumaliza matatizo yetu zaidi ya kutuwekea walevi wa madaraka. Inatakiwa kila mtu awe chini ya sheria na sio mambo ya amri toka juu.
 
Hatuhitaji DIKTETA...

Tumeongozwa na Dikteta Magufuli tumeona alivyokuwa anaendesha nchi kwa kadiri atakavyoamka..

Ametengenezea watu wengi kesi za hovyo hovyo..

Tunahitaji katiba bora.. Kusiwe na muingiliano wa kimajukumu
 
Mkuu Chukua fomu mimi ntaunga Mkono Juhudi, JF kutoa Rais wa JMT inawezekana, wapo wengi humu wana uwezo wa kuliongoza Taifa hili, ILA SIO WEWE MKUU we unaonekana una KISIRANI
 
Hatuhitaji DIKTETA...

Tumeongozwa na Dikteta Magufuli tumeona alivyokuwa anaendesha nchi kwa kadiri atakavyoamka..

Ametengenezea watu wengi kesi za hovyo hovyo..

Tunahitaji katiba bora.. Kusiwe na muingiliano wa kimajukumu
Udiktekta upi wake,ulishawahi kulala saa 12 jioni

Ova
 
Udiktekta upi wake,ulishawahi kulala saa 12 jioni

Ova
Siongelei kulala saa 12 jioni..

Huyo mtu wenu alijiona anajua kila kitu mwenyewe na kukataa maagizo mengi ya wataalam...
Na ndio maana alikosana mno na Gavana Benno..

Huwezi kuwa na hiko cheo ukajidai unajua kila sekta.. Na ukajifanya eti wewe ni final
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…