Tanzania inaongoza Afrika kwa kuwa na Walevi wengi."Kwa hali hii Maendeleo ni ndoto"

Tanzania inaongoza Afrika kwa kuwa na Walevi wengi."Kwa hali hii Maendeleo ni ndoto"

Hii imesababishwa na aina ya uongozi tulio nao toka uhuru.
Ni wazi kabisa roho lililo nyuma ya nchi yetu ni ya umasikini na kukata tamaa inayosukuma jamii kuwa ya walevi, wachawi, wanafiki ambayo ni kichocheo kikubwa cha magonjwa ya akili.
Msababishaji mkuu ni chama kinachotawala yaani ccm!
 
kwa unafiki kombe letu na nafasi ya pili had 10 wasiweke mtu iwe cc tu,hakuna kisiwa cha amani sema unafiki mwingi,
 
Hii ni hatari kama sio balaa.Wenzetu wanaongoza kwa mambo ya msingi,ni ajabu Tanzania yetu inaongoza Afrika kwa kuwa na wale wengi.

Si ajabu wanawake wanakosa wanaume na waliopo hawana nguvu za kiume na za mwili,hupigwa hovyo kwa sababu ya ulevi.

Kana kwamba haitoshi Tzn iko mingoni mwa nchi top ten Duniani zinazoongoza kwa uchawi.

Sasa kama sisi tunaongoza kwa mambo ya kipuuzi ni wazi swala la maendeleo litaendelea kuwa ndoto.[emoji116]

====

TOP 10 ALCOHOL CONSUMERS IN AFRICA (2019)

Drink Types: Beer, Wine, Spirits & Others Litres Consumed Per Capita

1. Tanzania 7.81

2. Eswatini 7.68

3. Burkina Faso 7.28

4. SA 7.21

5. Uganda 6.82

6. Gabon 6.47

7. Rwanda 6.35

8. Equatorial Guinea 6.11

9.Botswana 5.98

10.Angola 5.84
View attachment 2086200
Wanaotuponza na kutoa siri zetu sisi walevi na hawa watengenezaji wa hizi pombe yaani wenye viwanda,wamebweteka na pesa zetu hivi hawajui kwa umoja wetu wa walevi tukiamua kwa nguvu na umoja wetu HATUNYWI POMBE KWA ANGALAU WIKI MOJA TU,UNADHANI PATAKARIKA?Yaani yaani tukiamua kufanya mgomo wa kutokunywa,aisee aisee
Ila tukisemwa sana ipo siku na sisi tutafanya jambo mje muone miji inavofanana bila walevi kwn hamjawahi kuona.Waache kutoa siri zetu tumeishakubali limbwata lao ndo maana WALEVI hatuna umoja,
Pombe nayo ni maendeleo kwani imetoa ajira ya mamilioni na mamilioni ya Watanzania leo tukigoma nchi itazizima.
WALEVI tunachangia pato la taifa kwa kiwango cha juu sana
Tanzania ya viwanda,ebu hesabu viwanda vikubwa tena vya kimataifa vinavyotengeneza pombe Tanzania,ndo tugome kunywa hivyo utovisikia tena na uchumi utayumba ile mbaya
WEWE UNATAKA MAENDELEO YEPI
 
Acha wivu mtoa Mada, Sisi Ni wazalendo.. unajua Serikali unakusanya Kodi kiasi gani kupitia Pombe?? Tusingekunywa Barabara ya kwenda kwenu Mpanda utajenga wewe??
Namshangaa mtoa mada,wanatudharau jamani hawajui tukichomoa betri ni hatari hata kwake mnywa soda [emoji23][emoji23]
 
We unaona kila mlevi ana hela na maisha? Mbona wengi wako hoi kiuchumi?
Wewe unaongelea wanywa gongo,aisee wanywa pombe wanaojitambua wana maendeleo makubwa sana tena kuliko nyie wengi msiokunywa niamin ndugu yangu.Wanywa pombe wengi wana familia bora watoto wasoma shule za maana,ni wafanyakazi mahili make wasingekuwa mahili hata pesa ya kunywa wangeipata wapi,wanamiliki mali za maana nk. Ndo nikasema wewe unaongelea walevi wa gongo, gidi, ulazi nk.
Na wasiokunywa kuna mianya mingi sana wanakopotezea pesa tena kipumbavu klk hata wanywaji
 
Kwani hujui pombe ndio sehemu walio hoi huwa wanajifarijia? Pombe ziko za aina nyingi ,hata mbege na gongo ni pombe tofauti ni vifungashio.
Toa mbege kwenye huu upumbavu, Mbege n kinywaji cha asili Mbege haileweshi ukalewa ukawa Fala.
 
Tulikua busy kuwakomboa nchi zilizokua hazina Uhuru na vurugu zawao kwawao ,tumemaliza acheni yuenjoy kidogo
 
Back
Top Bottom