Tanzania inayotaka kujitegemea kiuchumi sasa inarudi zama za kutembeza bakuli ughaibuni

Tanzania inayotaka kujitegemea kiuchumi sasa inarudi zama za kutembeza bakuli ughaibuni

Mtetezi wa mama Samia, mkosoaji wa Magufuli. Rangi halisi haijifichagi sheikh.
Msgufulii lazima atakosolewa kwa nguvu zote maana aliwafunga watu midomo utadhani tupo nchi ya majilani zetu kumbe tupo nyumbani kwetu.
 
Sijaona hoja mkuu kukaribisha uwekezaji sio kutembeza bakuli.Nikukumbushe tu China imefika hapo ilipofika sio kwa fedha zake tu bali uwekezaji wa wafanyabiashara kutoka magharibi.Sema tu wenzetu ni wajanja sana kwe kuiba technolojia na kulinda soko lao.Ndio maana china waafrica ni rahisi kwao kununua bidhaa za china lakini ni ngumu sana Mwafrica kuingiza bidhaa china wanafanya hivyo ili sisi tubaki kuwa soko lao.Hiki ndicho kenya imekua ikiifanyia Tanzania.Nilipenda speech ya Rostam alipowaambia wakenya kua Tanzania haiwezi kukubali kubaki kuwa supplier wa Raw materials tu ni Lazima na wao wakubali uwekezaji toka Tanzania.
Rostam aliongea maono ya JPM, mama anatembelea biti za JK, kazi ipo.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Vita ya kiuchumi huwezi ipangua kwa kuwalamba watu miguu, kutembeza bakuli na ku compromise na kila kitu. Nchi yoyote yenye viongozi makini, huhakikisha wanatumia kila walichonacho +resources za nchi nyingine kujikwamua. Tulianza kupiga hatua, tukafika mpaka uchumi wa kati wa chini sio haba ila huko tuendako naona tunarudi tena kwenye group la nchi masikini kwa uzembe wa watawala wasio na maono. Inasikitisha Sana, endeleeni kupiga makofi na vigelegele.
Awamu yenu imeisha tulieni waachieni wenzenu nao wafanye yao.
Kosa tulilo lifanya kamwe hatutalirudia tena.
 
Vita ya kiuchumi huwezi ipangua kwa kuwalamba watu miguu, kutembeza bakuli na ku compromise na kila kitu. Nchi yoyote yenye viongozi makini, huhakikisha wanatumia kila walichonacho +resources za nchi nyingine kujikwamua. Tulianza kupiga hatua, tukafika mpaka uchumi wa kati wa chini sio haba ila huko tuendako naona tunarudi tena kwenye group la nchi masikini kwa uzembe wa watawala wasio na maono. Inasikitisha Sana, endeleeni kupiga makofi na vigelegele.
Vita vya kiuchumi mlikuwa mnashindana na nani?
Vita vya kiuchumi huku mnafisadi mabilioni.
 
Pamoja kiongozi,muda ni mwalimu mzuri ,ukifika wakati utaongea
Sukuma gang ni kipindi chenu mwacheni rais afanye kazi za kuiletea maendeleo nchi yetu iliyo haribiwa na utawala wenu.
 
Nimeshangaa kuambiwa mwendazake alichukua billion 120 kwenye akaunti ya wafanyabiashara mmoja ambaye analipa Jodi vizuri tuu
Eti wamechukua sababu jamaa anahela nyingi
 
Mabeberu tunajipanga kurudi ili ajira zirude ,na mzunguko wa hela urudi
Ilikuwa ndoto mbaya ile imepita............

1620420495634.png
 
Jiwe alikuwa anamkamua ng'ombe hadi anabakiza manyoya tu ili mradi apate sifa kuwa anakusanya kodi nyingi.

Pamoja na watu wake kugundua mapungufu kwenye ukusanyaji kodi kwa kutumia ubabe na vitisho na kufirisi watu.

Lkn wafuasi wake walikuwa wanakenua meno utadhani ni mazuzu tu .
Leo hii wengi wao ndiyo wanaanza kufunguka akili na kuanza kukosoa .
Maisha hayana ukamilifu. Kujifunza kupo dunia nzima.

Pia hatuongozwi na malaika wanaoshuka kutoka mbinguni, tunaongozwa na binadamu wanaosubiri kufa ili wakutane na hukumu ya Mungu.
 
Vita ya kiuchumi huwezi ipangua kwa kuwalamba watu miguu, kutembeza bakuli na ku compromise na kila kitu. Nchi yoyote yenye viongozi makini, huhakikisha wanatumia kila walichonacho +resources za nchi nyingine kujikwamua. Tulianza kupiga hatua, tukafika mpaka uchumi wa kati wa chini sio haba ila huko tuendako naona tunarudi tena kwenye group la nchi masikini kwa uzembe wa watawala wasio na maono. Inasikitisha Sana, endeleeni kupiga makofi na vigelegele.
Wapumbavu moo wengi sana
 
Kama ulikua unamsikiliza vizuri JPM hakuna sehemu aliyowahi kusema nchi isiingiliane kiuchumi na nchi nyingine. Alichokua anapinga ni wawekezaji wababaishaji ambao walizoea kuja kuchota rasilimali zetu na kupeleka kwao. Huyu mama anaturudisha kwenye sera za JK ambazo hazikuwahi kuinufaisha hii nchi.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Hivi unataka kuniambia sisi hatuna akili kabisa mpaka tuingie mikataba ya kinyonyaji? Kinachotakiwa ni kila upande ufaidike lakini kuacha eti kwa kuogopa tutaibiwa huu ni zaidi ya ujinga.
 
Dalili ya mvua ni mawingu, hali hii inatokana na matamshi na vision ya kiongozi aliyeko Madarakani.

Si kweli kwamba utaratibu wa uwekezaji nchini ni mbaya, nakataa hili kwa ushahidi kwa kupitia kauli ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini Rostom Aziz aliyoitoa akiwa ziarani Kenya aliyeambatana na Rais Samia.

Alisema, mfano kuna kampuni 530 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania,hebu lingania makampuni ya Tanzania nchini Kenya ,ambayo ni 30 tu, hivyo uwekezaji nchini kwetu ni rahisi kabisa, ispokuwa kuna machache ya kurekebisha kulingana na matakwa ya muda husika.

Hivyo sisi tumefungua fursa zaidi kuliko wenzetu, isipokuwa wenzetu wametugeuza sisi ndio raw materials producers wa viwanda vyao na wanahakikisha hatukui kwenye eneo la viwanda nchini. Hili Magufuli alilipinga kwa nguvu zote ndio maana akaja na sera ya viwanda.

Niseme tu hayati Magufuli alikuwa ni mtu ambaye Mara nyingi alifanya tafiti na kupata takwimu kabla ya Maamuzi magumu kutolewa, hii ilimfanya aheshimike sana duniani licha ya mahasimu wake kumshusha thamani.

Hayati Magufuli enzi ya utawala wake hakupenda kabisa ubabaishaji na hili lilimgharimu sana .ndicho kilichopelekea baadhi ya makampuni na wafanyabiashara matapeli kukimbia nchini, ambao Mama Samia kaenda kuwapigia Magoti.

Sasa naiona Tanzania inarudi ilipotoka, Tanzania inaenda kuwa nchi ya wachuuzi tena ,pamoja na raslimali lukuki ilizonazo,hii inaendana pia na kushuka kwa morali ya uwajibikaji wa baadhi ya viongozi wetu na kujiingiza kwenye rushwa.

Maneno aliyosema Rais Samia alipokutana na wafanyabiashara nchini Kenya ya kwamba anaenda kuifungua nchi. Je, ni lini nchi hii ilifunga mipaka yake?

Nafikiri angesema hakusanyi kodi tena wawekezaji ruksa kufanyabiashara nchini bila masharti tungrmuelewa na jambo hilo halipo duniani, kodi ndio msingi wa maendeleo, serikali kama haikusanyi kodi haina uhalali wa kutawala.

Mwisho kataja bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda, tusikubali uharaka haraka wake kusaini hii mikataba bila ya kujiridhisha, bunge lihakikishe mikataba hii haisainiwi gizani kama alivyofanya kwenye hili bomba la kuuza gasi nchini Kenya.

Mambo haya yalifanyika sana enzi za awamu ya nne, na yameligharimu sana taifa baada ya hayati Magufuli kutaka kuinasua nchi kwenye ujinga huu, naona Mama Samia anataka kupita kulekule kulipotugharimu. Vinginevyo nchi hii tunaenda kugawana mbao, Magufuli kaondoka kawatoa watanzania tongotongo machoni.

mama kapiga U turn inaenda ku mcost sana

soon lile taifa linadorora, na wapinzania watarudia agenda zao
 
Maisha hayana ukamilifu. Kujifunza kupo dunia nzima.

Pia hatuongozwi na malaika wanaoshuka kutoka mbinguni, tunaongozwa na binadamu wanaosubiri kufa ili wakutane na hukumu ya Mungu.
Tatizo kulikuwa na wana ccm wenzenu kwa kujipendekeza kulio pitiliza walidiliki hata kumuita jiwe kuwa ni YESU.

wengine wakamfananisha na MALAIKA hiyo ni kufuru iliyo vuka mipaka.
 
mama kapiga U turn inaenda ku mcost sana

soon lile taifa linadorora, na wapinzania watarudia agenda zao
Hutaki jinyonge maana huna faida yoyote hapa nchini.

Haiwezekani uwe unapinga juhudi za rais za kusafisha nchi iliyojaa ukatili na udikiteeta.

Hongera zake nyingi mama yetu kwa kukyekeleeea hayo maujinga ukiwepo na wewe.
 
Tunawajua kundi lenu loote mnaojitahidi kumkwamisha mama Samia.

Mnajitahidi kubeza kila anachokifanya.

Hata hivyo hamtaweza maana tayari mshajulikana.

Niwashauri tu kuwa mnatakiwa mkubali kuwa mama Samia ndiye Rais wa JMT.
ila mtoa mada kaeleza vizuri tu. inakuaje kenya wawe na viwanda 534 Tz alafu useme nchi imefungwa, je kenya nao watafungua kama anavyofungua yeye. hizi hoja ni muhimu kabla hujaleta mapenzi mkuu
 
Kwa aina ya mateso tuliyopotia chini ya utawala wa Kayafa,mama hata akitaka kuiuza kigamboni kwa wakenya sawa tu
kwanini asiuze kile kijiji mkoa unaotoka unataja mkoa na eneo la wazaramo wenye eneo lao
 
ila mtoa mada kaeleza vizuri tu. inakuaje kenya wawe na viwanda 534 Tz alafu useme nchi imefungwa, je kenya nao watafungua kama anavyofungua yeye. hizi hoja ni muhimu kabla hujaleta mapenzi mkuu
Hakuna aliyewakataza kwenda kuwekeza wacheni kujifanya hamuelewi.
Serikali hiwezi kuwatia kamba wafanya biashara kuwalazimisha kwenda kuwekeza nchini Kenya?
 
Magufuli is dead and not coming back
Live with it!

Business and Investment environment during Magufuli regime was very bad, We are happy that Madam president is mitigating the situation

Above all Magufuli regime was characterised with gross human rights violation, including extortion, and taking farmers cashew nuts by force using the military.

Madam president is going to eliminate that nonsense and create confidence for businesses to flourish and investors to come.
andika kiswahili tu, maana engish mbovu sana
 
Back
Top Bottom