DOKEZO Tanzania Institute Of Education (TIE) does the textbooks business in a "cocaine style". Is that the core job of the institute?

DOKEZO Tanzania Institute Of Education (TIE) does the textbooks business in a "cocaine style". Is that the core job of the institute?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kiwahili Comprehensive Edition:
TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) INAFANYA BIASHARA YA ELIMU NA VITABU KWA MTINDO WA DAWA YA KULEVYA. BIASHARA YA VITABU (TEXTBOOKS) NDIYO KAZI YAO KWA KISHERIA YA TAASISI HII?

Kwanza kabisa TET imechanganyikiwa na kuvurugikiwa kimajukumu kiasi kwamba hakuna hata viongozi wanaotambulika kwa sheria ya bunge, hakuna kipaumbele, mwelekeo wa shighuli na hata tija. Matokeo yake ni kuwa kuna mitaala mibovu inayobadilika kila mara mheshimiwa mpya anapochukua madaraka. Mbaya zaidi, Taasisi hii HAIKO KISHERIA na inaendeshwa kama vile Behewa la Garimoshi kuvutwa na MBUZI. Hali hii inachochewa sana na kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi zinazomwangwa hapa na kutumika kifisadi kwa ushirika na viongozi wakubwa katika wizara ya elimu. Hali hii haina tofauti kubwa na uchakataji wa madawa ya kulevya kule Mexico wakati wa Pablo Escobar kwani sheria na maadili havihusiki ila pesa mbele.

Kwa mara ya mwisho Sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 1993 (TIE Act 1993) iliibadilisha taasisi hii kutoka Taasisi ya Ukuzaji Mitaala (Tanzania Institute of Curriculum Development) kuwa Taasisi ya Elimu Tanzania (Tanzania Institute of Education-TIE). Muundo wa kiutawala ulikuwa kwamba kuna Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi na waliofuata walikuwa ni wakuu wa idara 4. Bila sheria yoyote ya Bunge, Sasa kuna Mkurugenzi mkuu (Director General) mwenye madaraka makubwa hata akitaka kuiuza TIE kwa bei ya mchicha anaweza kufanya hivyo.

Kwa madaraka makubwa katika elimu ya watoto wa Tanzania iliyonayo TIE kwa sasa mambo mengi yameibuka na kundelea kufanyika kana kwamba Watanzania hatuoni na hata tukipewa mwanga wa koroboi tutembee nao mchana:

Kwa kutumia kawaraka ka elimu na. 14 ka mwaka 2014 ambao hakatokani na sheria ya bunge ila ni maamuzi tu ya waziri kwa maslahi yake (decision of administrative authority that not government policy that is supported by Act of Parliament), kazi zote za uandaaji, uandishi, Uhakiki, uchapishaji, uchapaji, uuzaji na usambazaji wa vitabu katika shule zote za Msingi, Sekondary na Vyuo vya ualimu TIE ikajijbebesha kama vile MBUZI Kuvuta behewa la gari moshi..!

Mwaka 2017 bila umakini wowote bali kupiga pesa, TIE walichapisha vitabu kwa shule zote na vyuo vya ualimu nchini kwa kiasi cha kama Tsh 15 bilioni. James Mbatia wakati huo akiwa Mbunge wa Vunjo akawasha moto Bungeni kuhusu ubovu wa vitabu vile. Baada ya malumbano makali bungeni vitabu vile vikakusanywa na kurudishwa TIE kimya kimya na hata sasa hatujui vilitupwa wapi ila najua karatasi hazitupwa bali hubadilishwa matumizi tu baada ya kuuzwa, na kazi ikaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.

Kutokana na mapesa yanayomwangwa TIE, biashara ya vitabu imekuwa in pango la walaji wenye meno mchongoko. Katika hali isiyo ya kawaida, utayarishaji mwa mswada wa kitabu tarajiwa (manuscript) kabla ya kupelekwa kwa Printer nje ya nchi kwa mtindo wa TIE gharama hufikia hadi Tsh milioni 40 wakati kwa publisher wa kawaida ni chini ya Tsh milioni 4. Kwa hali hiyo uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa vitabu vya TIE hauna tofauti kubwa na ile biashara ya cocaine kule Mxico wakati wa Pablo Escobar kwani hata bei ya kitabu haijulikani kwa inapangwaje (cover price determination). Twende kwa hisabati rahisi, katika catalogi ya bei ya vitabu vya TIE kwa msimu huu ambayo wala haiko wazi na haijulikani pa kuipata kuna vitabu 61 viko sokoni ambapo kama vilitayarishwa kwa mitindo pekee wa TIE ina maana Tsh 40 milioni zilitumika zidisha kwa 61 unapata kiasi cha Tsh 2,440,000,000/- zilitumika kabla ya kwenda kuchapisha nje ya nchi kwa pesa nyingine nyingi. Hapa ndipo palipo na utamu wa biashara ya vitabu kwa TIE. Wanang’ang’ania kwa mbinde na kusahau majukumu yao ya ukuzji wa mitaala na elimu bora kama jukumu lao kwa mujibu wa sheria.

Katika hali ya kushangaza, TIE wamejivika kazi ya kuidhinisha vitabu vya wachapishaji binafsi ambao watashindana na bidhaa za TIE sokoni! Kwanza TIE hakuna wataalamu huru wakufanya kazi ya kuidhinisha vitabu na kutoa idhibati (approval) na pia ni kinyume na haki ya asili (Natural Justice). Huwezi kuwa mwamuzi katika jambo linalokuhusu (You cannot be a Judge in your own cause). Yaani wazalishaji 2 wako sokoni na bidhaa shindani kwa wateja wale wale lakini huyu mmoja ni mkaguzi/muidhinishaji wa bidhaa za mshindani wake, maajabu haya siyo mpaka Prof. Shivji aseme!

Kwa hivyo basi, sekata ya elimu na vitabu kwa ujumla imepoteza dira na mwelekeo. Elimu, mitaala, vitabu na Dira ya Elimu havina mahusiano mema kwa faida ya elimu ya Watanzania kwa sasa na hata kesho yake haijulikani.

Textbooks publishing in Tanzania have gone hullaballoo since times before...
Edit op yako uongezee hii tafsiri ili mtu akifungua huu uzi akutane na Swahili version moja kwa moja.
 
Ndugu Midas Touch ,Mungu akubariki sana kwa kuliona hilo na kuliweka wazi.
Kongole sana kwa uzalendo.

Nina dada yangu mmoja ni Prof, alistaafu huko nnje akaja kupata contract hapo TET.

Aliwahi kuniambia kuwa hajawahi kuona madudu makubwa na ya kutisha yakifanyika kwenye taasisi ya umma, tena iliyopewa jukumu la kupika wataalamu wa kesho, kama hapo TET.

Hii elimu yetu inavyochezewa na watu walioaminiwa na kupewa dhamana ya kiuongozi, ni bomu ambalo lisipoteguliwa sasa, litakuja kuiangamiza Tanzania mazima.

Hivi na Tanzania Elimu Supply (TES) ilifia wapi na ilikufaje!!??
 
Ndugu Midas Touch ,Mungu akubariki sana kwa kuliona hilo na kuliweka wazi.
Kongole sana kwa uzalendo.

Nina dada yangu mmoja ni Prof, alistaafu huko nnje akaja kupata contract hapo TET.

Aliwahi kuniambia kuwa hajawahi kuona madudu makubwa na ya kutisha yakifanyika kwenye taasisi ya umma, tena iliyopewa jukumu la kupika wataalamu wa kesho, kama hapo TET.

Hii elimu yetu inavyochezewa na watu walioaminiwa na kupewa dhamana ya kiuongozi, ni bomu ambalo lisipoteguliwa sasa, litakuja kuiangamiza Tanzania mazima.

Hivi na Tanzania Elimu Supply (TES) ilifia wapi na ilikufaje!!??
TES ilikuwa ni agent wa serikali ktk kusambaza vifaa vya elimu pamoja na vitabu mashuleni, ilikufa siku nyingi sana ambapo TIE kazoa kazi za TES pamoja na Private publishers na Bookselers. Maajabu haya.
 
T. I. E walivyo wajanja maswali yote ya NECTA wanatoa kwenye vitabu vyao ili vitabu vinunuliwe Kwa wingi.
 
Back
Top Bottom