Mtu kufia hospitali haimaanishi kuwa ni lazima kwamba mwili wake uhifadhiwe hapo. Bado mnaweza kufanya taratibu mkaondoka na mwili na kisha kwenda kuuhifadhi kwenye a private mortuary kama mkitaka hivyo. Ila pia mkuu, kuna watu wengi tu wanafia kwenye hospitali/vituo vya afya ambavyo havina mortuary, hii pia huwa inatokea. Au mtu anafia hospitali yenye mortuary ila mnaambiwa kwa wakati huo imejaa, kwa hiyo mnaambiwa mchukue mwili labda muuepeleka mortuary ya Muhimbili au mortuary ya hospitali nyingine yoyote kubwa. Hapa sasa pia mnaweza kuamua kuupeleka mwili private mortuary.
Changamoto ambayo naiona itabidi kupambana nayo ni namna ya kuitangaza au kuifanya ijulikane... Maana kwa response niliyoiona hapa inaonekana Watanzania wengi wako so negative about this. Ila, mtu akianzisha na akapata namna tu ambayo ikafanya ikajulikana (mfano kwa kuestablish links na hospitali/vituo vya afya binafsi ambavyo havina mortuary, au kuingia mkataba nazo kwamba ikitokea mgonjwa amefariki, basi wanamleta kumhifadhi hapo kwako then wao wanapata percent fulani na wewe unapata percent fulani kulingana na makubaliano mtakayofikia, etc), kutusua ni rahisi.