Nimeshawahi kuliongea hili siku za nyuma, na hapa narudia kuongea mawazo yangu yale yale yenye elements za Kibeberu, ambayo naamini hata ndugu yangu
Kataskopos sometimes huwa anajiuliza "hivi huyu blaza sometimes huwa ankulaga ule mmea?"
The answer is YES, sometimes nakulaga ule mmea, na ndio maana bila aibu wala soni hapa narudia tena kwamba tunatakiwa kumuunga mkono Egypt na sio Ethiopia!!
Sio unamuunga mkono wazi wazi bali tunajifanya ni namna gani Tanzania tulivyo binadamu; na ni namna gani tunatakiwa kutanguliza ubinadamu kwa Egypt ambao hawana chanzo chochote cha maji cha uhakika zaidi ya Mto Nile!
Hapa tunajifanya kulia ni namna gani maisha ya Wamisri yanavyoweza kuvurugika pasipo na Mto Nile wenye maji ya kutosha!!
Kwamba, ujenzi wa Grand Ethiopian Renaissance Dam utaiathiri sana Blue Nile na hivyo kuleta janga kubwa kwa Egypt inayotegemea tu Nile! Sio tu itaathiri Egypt Livelihood bali pia inaweza kuathiri mazingira!!!
Tukifanya hayo kwa uchungu usiomithirika:-
Dunia itatushangilia kwa "ubinadamu" wetu!
Wanamazingira watatushangilia kwa jinsi tunavyojali mazingira!!
Waarabu na wenyewe watatushangilia kwa jinsi tunavyosimama na Warabu wenzao;
Kumbe:-
Deep inside tunalenga tu kuhujumu ufanisi wa Grand Ethiopian Renaissance Dam!!
How come tuchekelee tu kumuona Ethiopia anajenga mbwawa mkubwa kama ule ambao kimsingi lengo lake ni kutaka kuuza umeme kwa nchi za Afrika Mashariki?!
Kule Lindi na Mtwara kuna gesi ya kumwaga ambayo na tukipata Visionary Leaders, itatuwezesha kuwa wauzaji wakubwa wa nishati ukanda huu wa Afrika!!!
Grand Ethiopian Renaissance Dam ni threat kwa hiyo fursa, kwahiyo mawazo ya kibeberu yanahitajika kuwahujumu Wahabeshi!!
Hapa hapa nilishauri "tuwaunge mkono" ndugu zetu Wakenya baada ya kuzuka taarifa kwamba Wachina wanataka kupokonya Bandari ya Mombasa ili kufidia deni lao!!
Kwamba tupinge uharamia huo wa Uchina wa kutaka kuwanyang'anya ndugu zetu Wakenya Bandari waliyoirithi toka kwa Mababu wa Mababu zao!!!!
Watu hawakunielewa! Hawakunielewa kwa sababu hawawezi kuelewa what would happen kwa Dar es salaam Port endapo Mchina atakuwa ndie operator wa Mombasa Port!!
Na kwahiyo sitashangaa na hapa tena nisipoeleweka kwa sababu si kazi ndogo kuelewa what will happen endapo Ethiopia anakuwa ndie Energy Giant kwenye ukanda huu wa Afrika!!
Energy can be used as a weapon in geopolitics!!
Leo KE anatufungia tu mpaka kwa sababu anaamini hatuwezi kumbabaisha!!
Kinyume chake, hata kama ONLY 10% ya Mombasa and Nairobi Residents depend on energy from Tanzania; hapo KE kabla hawajatufanyia unyang'au wowote watakuwa kwanza wanajiuliza "...lakini na hii mijamaa haitafunga zile valves zinazoleta gas Nairobi and Mombasa?!"
Tuwaunge mkono Misri!
Misri ni ndugu zetu! Ni ndugu zetu kwa sababu ni Waarabu! Waarabu ni ndugu zetu kwa sababu Zanzibar pia kuna Waarabu! Hata huku Tandika pia tunaishi na Waarabu lakini hakuna Mhabeshi hata mmoja!
NIMEMALIZA!!!!