Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Ujerumani analitambua kama Ziwa Malawi (Milki ya Malawi).

Uingereza analitambua kama Ziwa Nyasa na Ziwa Malawi upande wa Malawi (Milki ya Tanzania na Malawi).
Kwa kawaida makoloni ya Uingereza yalikuwa yanagawana vyanzo vya maji nusu kwa nusu. Mkataba wa Heligoland wa mwanzo kabisa na ule wa pili sikumbuki ni wapi walisema ziwa Nyasa inamilikiwa na nchi mbili. Naamini ukiwaambia Malawi waoneshe ramani ya wakoloni wataonesha inayowatetea maana ipo.
 
Ujerumani analitambua kama Ziwa Malawi (Milki ya Malawi).

Uingereza analitambua kama Ziwa Nyasa na Ziwa Malawi upande wa Malawi (Milki ya Tanzania na Malawi).
Check this, hili ziwa kimataifa linatambulika ni la Malawi.
IMG_20200801_002534.jpg
 
Kwa kawaida makoloni ya Uingereza yalikuwa yanagawana vyanzo vya maji nusu kwa nusu. Mkataba wa Heligoland wa mwanzo kabisa na ule wa pili sikumbuki ni wapi walisema ziwa Nyasa inamilikiwa na nchi mbili. Naamini ukiwaambia Malawi waoneshe ramani ya wakoloni wataonesha inayowatetea maana ipo.
Ramani za hivi karibuni zinatumia dots kuwakilisha eneo lina mgogoro, chache ndio zenye kuonesha mpaka upo Kati, huku nyingine zikilalia Tanzania na Nyingine Malawi.
 
Conclusion yako ndio ambayo sijailewa
 
... pia kingine ni wakati muafaka kwa Misri kuwa na proper birth control kuhakikisha population yao ni proportional na resources ya (sio za) maji waliyo nayo - The Nile. Wanajua the only water source waliyo nayo ni hiyo for everything drinking, industrial, irrigation, etc. whatever you name halafu kwa kuzaliana hawajambo; I think third in Africa after Nigeria and Ethiopia. Wawe na mpango wa makusudi wa kudhibiti ongezeko la watu vinginevyo soon itakula kwao hata ya kunywa watayakosa wakifanya mchezo.

Mkuu RTI kasema Ethiopia wasijitoe ufahamu kujipima kifua na Misri ni kweli, Misri wako mbali kijeshi kuliko Ethiopia, lakini hata wakipigwa leo hawatalala nao watakuwa na mpango wa muda wa kati na mrefu 25, 50, 100 years kuja ku-retaliate. Ni kama China, Iran, NK leo wanavyotunishiana misuli na US wakati miaka michache iliyopita walikuwa si lolote.

So, in the long run, millitary approach might not be useful for Egypt, badala yake mipango madhubuti ya kuendana na resources zitakazokuwa zinapatikana by then. Of course hii inahusu nchi zote sio kufyatua fyatua ovyo wakati unajua resources za kulisha na kunywesha watu wako ni finyu.
Siku hizi kupigana vita ni ngumu sana na very expensive.

Angalia US anavyoyumba kiuchumi kisa vita zisizoisha.

Misri hana ubavu wa kuingia vitani sasa. Uchumi umeyumba sana.

Wataitana mezani na kuyaongea.

Ethiopia asipangiwe na mtu kutumia maji ya Nile.

Hata Magufuli naye avute maji mpaka Dodoma.
 
Unatumia vigezo gani kusema mlima Kilimanjaro uko kwenye mipaka ya Tanzania. Vigezo hivyo viliwekwa na nani?
Sheria zilezile zinazotambua Kili kuwa Tanzania ndizo kama hizo zinatambua maji ya Nile yasitumiwe nje ya mkataba. Sio mimi niliyesema, ni mabeberu.

Kama unadhani sina akili toka kwenye uzi huu anzisha uzi wako uni-tag.
Uko sahihi, ukiona sheria inabagua Basi inatakiwa kufutwa. Kuna watu wanalaani sheria ya mabeberu kuhusu matumizi ya mto Nile lakini wanawapongeza mabeberu haohao kwa sheria za mipaka ya nchi. Mfano, kwanini Rwanda au Djibouti ikilalamika kupunjwa nchi yao kuwa kadogo hakuna aliyetayari kuwasikiliza? Sababu ya kutowasikiliza Ni kwamba mipaka imeshawekwa na mabeberu.
 
Hivi unafahamu kwamba mkataba lazima uwe na time limit as in validity yake katika kuanza na pia kuisha? Leo nikikuletea mkataba uliosainiwa enzi za Yesu au pengine kabla ya Yesu, maybe 150 B.C, utaukubali? Yaani mkataba uliosainiwa miaka 150 kabla Yesu hajazaliwa, utaukubali? Mataifa ya Kiafrika karibu yote and infact nadhani ni yote tumepata uhuru baada ya hiyo 1919, hivyo ni vyema mikataba yote ya nyuma ambayo haimake logical sense tukaijadili na kuitengua, ni kama ule unaosema eti maji ya nyasa yote ni ya Malawi, that is nonsense!!!
Kwani huo Ni mkataba au sheria? sheria anadumu hadi hapo itakapotenguliwa. Mfano, Kuna ipo sheria inayokataza baba kumuoa Binti yake, au kuzini au kusengenya. Inadumu tangu enzi na enzi. Leo hii ukimuoa Binti yako au mama yako unafungwa jela
 
... ni kosa baya kabisa kufanya hivyo! Atakuwa hapigani tena vita na Egypt but the world; at least majority. Kuna sheria kali kabisa zinazozuia uhalifu wa aina hiyo maana sumu inauwa kila kitu binadamu na bayo anuai yote all the way downstream and even far beyond to Europe (Mediterranean)! Yaani uwapelekee Ulaya sumu wakutizame tu kisa unamkomoa mbaya wako? Duh; stop thinking of that nonsense please!
Mzee kwani nuclear haiui kila kitu? Kwani hakuna biological weapons? Mbona sila hizo na zimetumika na hakuna aliyeshitakiwa?: Vita haina macho.
 
Siku hizi kupigana vita ni ngumu sana na very expensive.

Angalia US anavyoyumba kiuchumi kisa vita zisizoisha.

Misri hana ubavu wa kuingia vitani sasa. Uchumi umeyumba sana.

Wataitana mezani na kuyaongea.

Ethiopia asipangiwe na mtu kutumia maji ya Nile.

Hata Magufuli naye avute maji mpaka Dodoma.
Misri uchumi umeyumba kivipi wakati saivi niya pili Afrika
 
Haya mambo magumu sana aisee nasoma comments mdogo mdogo halafu nimejikuta napata swali

Wale wamisri wanaotujengea Nyerere hydro tumekubaliama nao nini??? Isije ikawa tumewaahidi kuwaunga mkono wakimbana Ethiopia
Hata Egypt anafahamu Tanzania ndio taifa lenye nguvu kubwa ya kijeshi katika ukanda huu, takwimu wanazo. Hivyo kusaidia ujenzi wa Nyerere hydro sio kwa bahati mbaya. Inawezekana Ni strategy kuelekea Ethiopia. Kihistoria Egypt Ni rafiki yetu zaidi kuliko Ethiopia
 
Ujenzi wa Nyerere Hydropower SIO MSAADA. Ule ni mradi ulioshindanisha tena na kupata mshindi.
Mradi ule tumekopa pesa na tunalipa.
Egypt kama wamelikoroga wenyewe shauri yao.

Tanzania hatuna uwezo kuyazuia maji yasitiririke mto Nile, ila tunaweza kusambaza maji ya ziwa Victoria kwenye maeneo yote jirani kwa matumizi ya nyumbani na hata kilimo, tungeweza tungepunguza kiasi kinacho tiririka mtoni.
 
Russia alienda kumsaidia Syria nchi njaa kali hamna mafuta wala nini just kwa kujimwambafai na swagger sababu alijua wa US anatajiingiza
Ethiopian akiongea vizuri na Putin na Xi
Mwarabu atapotezea ishu yote vita
 
Hata Egypt anafahamu Tanzania ndio taifa lenye nguvu kubwa ya kijeshi katika ukanda huu, takwimu wanazo. Hivyo kusaidia ujenzi wa Nyerere hydro sio kwa bahati mbaya. Inawezekana Ni strategy kuelekea Ethiopia. Kihistoria Egypt Ni rafiki yetu zaidi kuliko Ethiopia
Wakati wa vita ya Uganda,tulimjua rafiki wa kweli - Ethiopia!
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?

Tanzania haitakiwi kuegemea upande wowote zaidi ijikite kushawishi nchi mbili hizi kufikia makubaliano mazuri namna ya matumizi ya Maji. Wanayogombania. Sema Misri ni watata sana kwenye Suala la kutumia maji ya mto Nile .
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?

Chonde Chonde Chote. Naomba katika hili tuweke records sawa. TANZANIA SIASA YETU NI YA KUTOKUFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE . Tusije tukaacha reli bali tusimamie nafasi yetu ya upatanishi kwa kuona haki, changamoto na udhaifu wa kila upande ili kusadifu miafaka isiyo hila wala unafiki. HII NDIYO TANZANIA HALISI.
 
Hao ulowataja wote, watakuwa wanaongea tu, action zikiwa sifuri. Sudan mwenyewe alikubaliana na Egypt ET wasijenge hilo bwawa. Kama sikosei katika huo mkataba Sudan na Egypt waliwekwa kundi moja la kumilikishwa Nile. Kikubwa nchi ulizotaja zitajikita kwenye diplomacy rather than confrontation. Ila USA, UK na wenzao, watajikita kwenye supplies za military. Although sio kwamba USA na allies wake watapeleka majeshi yao, lakini wataipa silaha Egypt za uhakika katika kumpiga Ethiopia ikibidi.
Kitakachomponza Ethiopia kwenye hilo Ni ukaribu wake na nchi za kijamaa
 
Kumpiga mhabeshi misri itamchukua siku tatu tu ashaweka kambi somaliland na jibuti halafu misri wana mfumo wa kuzuia makombora wa thad na S 3000 unategemea nini
Hata USA walidhani hivyo pale kwa Asad, Syria lakini hadi Sasa imeshindikana.
 
Nimesoma comments nyingi za members humu na kugundua kuwa wengi hawafahamu historia na chanzo cha jeuri ya Misri kupata 'mandate' ya kuingilia mambo ya nchi nyingine wanufaika wa maji hayo.

Ingawa mleta mada katutaka wachangiaji tujigawe makundi ili kushabikia upande ambao tunaona wana haki katika mgogoro huo, ama jinsi tu mtu anavojisikia bila kuuangalia mgogoro wenyewe, mimi nimetofautiana kidogo!

Tungeangalia kwanza chanzo cha mto Nile kwa ujumla wake, wanufaika wake, sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu matumizi ya maji ya mto huo pamoja na mito mingine, maziwa na bahari zinazokuwemo, kugusa, kugawa nchi na nchi, kupitia katika jiografia za nchi mbali mbali husika duniani na si kushabikia .

Chanzo cha mto Nile kimejumuisha mataifa mengi na wote ni wanufaika wa maji hayo, ilitakiwa sasa mataifa yote yenye chanzo na wanaopitiwa mto Nile walione suala hili si la Ethiopia pekee, ni la wote.

Anachokifanya Ethiopia sasa kwa mfano, ndicho alichokifanya Uganda kujenga kituo cha kufulia umeme kwenye maporomoko ya Owen pale mjini Jinja unapoanzia mto Nile.

Nionavyo mimi, alifanya hivyo kwa kuwa ana haki ya matumizi ya mto huo pamoja na nchi zingine ambazo ni chanzo ama ni mapitio ya mto huo wanayo haki ya matumizi sahihi ya maji hayo.

Jambo la kujiuliza; hivi mabwawa ya kufulia umeme yanazuia maji kuendelea na safari yake kwenye uelekeo wake wa asili yakiisha kutumika kuendesha mitambo?

Jambo hili si la Ethiopia na Misri pekee, ni la mataifa yote ambayo ni chanzo, pamoja na wanaopitiwa na mto Nile tukiwemo sisi Tanzania, kukaa na kutafakari kiini cha mgogoro huu kwa kuwa wote ni wanufaika na unatuhusu.
 
Misri uchumi umeyumba kivipi wakati saivi niya pili Afrika
Kuwa wa kwanza au wa pili hakumaanishi uchumi haujayumba.

Wengine hizo bajeti mpaka sasa wanakopa na kupokea misaada.

Vita ni gharama sana, hakuna nchi Afrika yenye hiyo bajeti kwa sasa maana hata huduma muhimu hatuwezi kuzisambaza.
 
Back
Top Bottom