Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tatizo wanao takiwa kuidhibiti Misri ndio hao hao walio saini mkataba huo unao ipa haki Misri kuidhibiti huu mto ,nikimaanisha ni nchi za magharibi zenye uwezo wa kuidhibiti Misri.
Hakuna nchi ya kiafrika yenye ubavu wa kuidhibiti Misiri.
Sasa inapoelekea ikitokea vita basi itahusisha Misri, Ethiopia, Jamhuri ya Sudan, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania + (Rwanda na Burundi).

Tanzania yenye mchango mkubwa wa mto huo haitakiwi kukubali mkataba wa 1919's huko, Tanzania imepata uhuru 1961 na haikuingia mkataba huo, hata Ethiopia itumie hiki kigezo.

Unless, kila mtu atumie rasilimali zake katika mipaka yake, na hapo Ethiopia anamiliki Ziwa Tana na Blue Nile katika eneo lake.
 
Katika vita una judge nani atashinda kutokana na uhalisia uliopo kwa wakati huo. Una jeshi la namna gani na liko equiped kiasi gani na utayari lilionao kwa mafunzo. Hivi vyote vinaibeba Misri unapoilinganisha na Ethiopia. Labda kama kuna teknolojia ya haraka na gharama reasonable waliyonayo Ethiopia kubadili yale ma Boeing ya Ethiopia Airlines yawe heavy bombers labda wanaweza kuchukua hata round kwenye ring na Mafarao
 
Wakidundana, tutarajie USA kumpa msaada mkubwa Egypt.
 
Tatizo sio Misri na Ethiopia tena, hili suala litahusisha wote wenye mkono katika Nile na ikitoka hapo Misri atapata support ya Magharibi, maana nchi zote zilizobaki zinatafutwa sana na Magharibi wanatafuta sababu tu.
 
Mkuu ulikuwa serious kwamba Tanzania imchape Misri?
 
Kulisha watu zaidi ya milioni 100 kwa kutumia maji yaliyopitishwa kwenye hizo plants si pesa ndogo. Israel wanafanya hivyo kwakuwa hawana option zaidi ya hiyo.
 
Mnao ibeza Egypt kijeshi niwakumbushe tu kuna zile Mistral combat helicopter carrier Russia alikuwa ameweka oda kuzinunua Ufaransa baadae akazingua, aliekuja kuzinunua ni Egypt. Ni taifa linaweza kuprocure chochote wanachoweza mataifa makubwa. Sio nchi fulani ya kijima ambayo unahisi vitani na Ethiopia watapigana kwa mawe, matusi, uchawi na majini.
Kikubwa taasisi na mataifa asa ya Afrika yaongeze juhudi za kidplomasia ili huu mzozo uishe kibingwa maana sioni Tz tunafaidikaje na huu ugomvi
 
Ukiiambia Tanzania iache kutumia maji ya mito na ziwa yote ianze kutegemea tu maji ya bahari ya Hindi itakubali?
 
Maji yangu unipangie jinsi ya kuyatumia.

Misri wapumbavu sana.

Kama wanashida ya maji wageuze bahari chanzo chao cha maji.

Waache Waethiopia wafanye watakacho. Mto Nile ni baraka ya Mungu. Hatuna mwenye mamlaka na huo mto.
Nadhani wanachokosea Misri ni kutumia vitisho katika hili ila kiubinadam nadhani nchi zinatakiwa kumuelewa maana hamna kitu essential kwa uhai na usalama wa Taifa kama maji. Sasa em fikria Nile ndo chanzo cha maji baridi kwa wananchi wa Misri halafu leo usikie kuna mtu anafanya shughuli zake zinazoweza kuathiri negatively flow ya maji ya mto husika kuja kwako. Utajisikiaje? Ulishawahi kupigwa na jua halafu ukakosa maji ya kunywa! Ndo wanachokihisi wamisri unapoingilia flow ya mto Nile.
Tutangulize utu na ubinadamu kulihukumu hili
 
Kweli, utu na ubinadamu ndio uwe muongozo. Pia Misri anatakiwa kuacha vitisho akubali kukaa meza ya mazungumzo na Ethiopia.

Wote hao wakumbuke White Nile ndio yenye mchango wa asilia 72 katika kupatikana Great Nile.
 
sio silaha yoyote ambayo ni tishio kwa Ethiopia ambayo wanayo misri

mchakato hapa ni kuipiga Ethiopia na iwe koloni ili isijaze maji kwenye bwawa au watumie air force yao kushambulia bwawa (hit and run)

sioni ndege ambazo zinaweza kutekeleza hiyo mission bila kudunguliwa

alafu hawa Ethiopia army huwa wanafanya mazoezi kwa kudungua ndege za kenya in Somalia unajua kwa nn ?
 
misri alichelewa angeomba kuonewa huruma kabla bwawa halijajengwa au sasa hivi akubali kulipa gharama za ujenzi na atoe pesa ya nishati mbadala

walichokosea walionesha dharau tokea mwanzo
Kweli, utu na ubinadamu ndio uwe muongozo. Pia Misri anatakiwa kuacha vitisho akubali kukaa meza ya mazungumzo na Ethiopia.

Wote hao wakumbuke White Nile ndio yenye mchango wa asilia 72 katika kupatikana Great Nile.
 
Ata akimpatia, hautofikia msaada atakaopata Egypt, kuna UK nae yumo. Egypt ni very important ally wa western sasa ivi ili kuhakikisha usalama pale Israel.
UK na USA wanaipa supports misri ili kuihakikishia Israel usalama

na muda huohuo in deep Israel hawataki kuiona misri imara ili waendelee kuwa wababe wa middle East

in short haya mambo ni mapana saana
 
misri alichelewa angeomba kuonewa huruma kabla bwawa halijajengwa au sasa hivi akubali kulipa gharama za ujenzi na atoe pesa ya nishati mbadala

walichokosea walionesha dharau tokea mwanzo
Hakika,

Hili suala waongee wafikie tamati, either Misri ampatie mchango Ethiopia wa Bwawa na watapatiana umeme au alipe Ethiopia asimamishe na kuchukua umeme kutoka Aswan, Misri.

Yote kwa yote, wasilete vita maana Afrika wakimbizi wanafakiria Tanzania tu.
 
Yeye Misri ni nchi gani inayompangia masharti katika matumizi ya maji ya mto Nile?
Inatakiwa Nchi zote ambazo ni chanzo cha mto Nile zisimame kwa umoja wao kupinga ukoloni wa hao Mafarao.
Yaani huyu mwarabu alivyo na roho mbaya hata sisi huku tukinywa maji ya ziwa Victoria yeye roho inamuuma.
Nchi zote zisimame kwa pamoja kupinga huu ukoloni wa Misri, hili swala sio la Ethopia peke yake, maana wakishawadhibiti Wahabeshi wataleta tena chokochoko zao kwa nchi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…