Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Hakika,

Hili suala waongee wafikie tamati, either Misri ampatie mchango Ethiopia wa Bwawa na watapatiana umeme au alipe Ethiopia asimamishe na kuchukua umeme kutoka Aswan, Misri.

Yote kwa yote, wasilete vita maana Afrika wakimbizi wanafakiria Tanzania tu.
... si tu Ethiopia anauhitaji huo umeme kwa matumizi ya nyumbani bali anauhita pia kibiashara kuuza mataifa jirani. Pagumu sana hapo.
 
Sijakuelewa labda unisahihishe umesema Ethiopia ni chanzo kikuu cha mto nile,kivp wakati tunajua souce kubwa ni ziwa victoria
... chanzo kikuu cha R. Nile ni milima ya Abyssinia (Ethiopia) ambayo huchangia karibu 85% kupitia Blue Nile wakati L. Victoria and other tributaries huchangia roughly 15%. L. Victoria ni kubwa tu in terms surface area not in terms of volume.

Hivi unajua L. Tanganyika ni la ngapi kwa ukubwa duniani kwa kuhifadhi maji baridi? Ni la pili; it is extremely huge by far in terms fresh water volume than L. Victoria which is very shallow while L. Tanganyika is so deep!
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?
Kwani sisi tunapotumia matrillion ya pesa kutunza mazingira ili mvua zinyeshe na hatimae kujaza huo mto, huwa wanatuconsider vipi wao misri kama misri, huwa wanatupa pesa ya carbon credit? Au wanasubiri maji tu bila kujua tunavyotaabika huku kutunza vyanzo vya maji? Wajinga nini?
 
Vita kwa ajili ya maji haiko mbali, chanzo halisi cha mto Nile ni Lake Victoria. Time will tell
... inategemea unamaanisha nini unaposema "chanzo halisi" but the fact is that Blue Nile originating from the Abyssinian Highlands (Ethiopia) contributes 85% of the Great Nile waters while White Nile (L. Victoria) only 15%. That's the fact.
 
Hata maji ya ziwa Victoria Kuna pahala yanakotoka, lakini Kuna white Nile na blue Nile ambayo inakutana pahala na kutengeneza Nile inayokwenda hadi Misri. Blue ndiyo inayochangia maji mengi kwenye Nile watanisahihisha Wana geography. Blue Nile inatoka Ethiopia/Eritrea huko
... uko sahihi; Blue Nile originating from the Abyssinian Highlands (Ethiopia) contributes 85% of the Great Nile waters.
 
Mama Tanzania hafungamani na pande yoyote ile.....
Huo ni ujinga, Misri alishwahi kutuzuia eti tusipeleke maji ya ziwa victoria kwa wananchi wa Tabora, hata sijui walipata wapi jeuri ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu, very arrogant, ila Lowassa aliwanyoosha, wakatulia
 
Endapo ikitokea vita basi hata Misri na Ethiopia watapigana pasipo sababu za msingi, na Tanzania katika vita hiyo inabidi iwachape wote.

Vyanzo vya mto Nile ni mkanganyiko mkubwa na watu wanachukulia kwa wepesi.

White Nile, inawezekana* chanzo chake ni Rwanda/Burundi, Mto Kagera au Ziwa Nyanza (Victoria).

Blue Nile kwa hakika chanzo ni Ziwa Tana, Ethiopia.

Great Nile the mixer of White and Blue Nile inaanzia Khartoum, Jamhuri ya Sudan baada ya White x Blue Nile kuungana na kuendelea Ardan, Cairo hadi Alexandria.

Sasa sijaelewa wanaenda kupigana sababu ya Greater Nile, White Nile au Blue Nile?

Kama wanapigana sababu ya Greater Nile basi Tanzania awaadhibu wote kwa kushirikiana na Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Sudan. Endapo chanzo cha mapigano ni Blue Nile basi Ethiopia ana haki ya kumpiga Misri na kwa White Nile bado Tanzania ana haki ya kuwachapa wote.
Hilo bwawa limejengwa along blue, white or the greater nile?
 
Tuwe waangalifu tunapoikataa mikataba iliyowekwa na wakoloni wakati ukoloni. Mkataba uliowapa Misri haki ya kwanza kwenye utumiaji wa maji ya mto Nile uliwekwa wakati wa ukoloni na wakoloni kwa manufaa ya wakoloni, sawa na mipaka ya nchi zetu iliyoko Sasa.

Je, nchi zetu ziko tayari kuachana na mipaka ya wakoloni ili tuligawe upya Bara la Africa? Iko nchi itakubali kuwa mipaka ya wakoloni haifai tuanze upya. Hata Misri kwenye hili inawezekana kuwa Ina hoja
Mikataba ambayo pande zote tunakubaliana nayo haina shida, especially mipaka, ila kwa amabayo hatukubaliani nayo, waingie vitani kama wako tayari, au la tukae chini tuzungumze, uamuzi ni wao hao Egypt, na kwakuwa Egypt anataka kutumia huo mkataba kukandamiza nchi zingine zote, basi awe tayari kupigana nazo zote vita, maana hata sisi tulishaletewa vikwazo wakati tunajenga mradi wa maji wa ziwa victoria kwenda mikoa ya kaskazini, the agreement defies logic, its nonsensical, tutaingia vitani au laa wakubali mazungumzo kuvunja huo mkataba
 
... hapo kwenye red; Ethiopia naye mbishi ameombwa mara kadhaa ila kwa kuwa anajua kashika mpini analeta ubishi. Mara kibao ameitwa kwenye meza ya mazungumzo haendi.

... hapo kwenye blue; hapana, mchango wa White Nile unaoanzia L. Victoria ni roughly 15% only; share kubwa ni Blue Nile (Ethiopia) about 85%. Katika jiografia enzi hizo nakumbuka kulikuwa na swali maarufu la "why floods occur in lower Nile (Egypt) in the months of August and September?" Because, rain season in Ethiopia is in June to August so by August and September the Blue Nile waters reach Egypt. Nakumbuka kujibu hili swali kwenye papers ya mchujo FII miaka hiyo! Nashukuru hili swali lilinitoa bila kuhitaji kukariri darasa; haha haha!
Uko sahihi, Namimi nilijuwa hivyo
 
Naungana na Misri kwa kuwa hawana chanzo kingine cha maji zaidi ya Nile. Wewe ungekuwa rais wa Misri ungekubali kuona watu wanakufa njaa kwa kukosa maji ya kutumia na kumwagilia mashambani?

Tatizo Ethiopia anataka ajaze maji kwa mkupuo na abadilishe mkondo wa maji. Misri anaomba mkondo wa maji usibadilike na muda wa kujaza bwawa uwe miaka kadhaa, sio mkupuo.
Wao wanapotoa hewa za ukaa viwandani na kutetea ukame Afrika na watu kufa njaa, huwa tunaenda kuwafungia viwanda vyao?!
 
Mikataba ambayo pande zote tunakubaliana nayo haina shida, especially mipaka, ila kwa amabayo hatukubaliani nayo, waingie vitani kama wako tayari, au la tukae chini tuzungumze, uamuzi ni wao hao Egypt, na kwakuwa Egypt anataka kutumia huo mkataba kukandamiza nchi zingine zote, basi awe tayari kupigana nazo zote vita, maana hata sisi tulishaletewa vikwazo wakati tunajenga mradi wa maji wa ziwa victoria kwenda mikoa ya kaskazini, the agreement defies logic, its nonsensical, tutaingia vitani au laa wakubali mazungumzo kuvunja huo mkataba
Kama Kuna kosa kubwa ambalo nchi za bonde la Nile watalifanya Ni kujifanya mzozo wa Ethiopia na Egypt hauwahusu. Kwavyovyote vile Vita ya Ethiopia dhidi ya Egypt kwaajili ya matumizi ya maji ya mto Nile lazima iwe yao wote. Vinginevyo itakuwa mwenzio akinyolewa tia zako maji. Tutapigwa mmoja baada ya mwingine kuhusu maji haya.
 
Ukisema hivyo unakosea mkuu, sheria za kidunia haziruhusu kufanya chochote kwenye chanzo cha maji kumbuka Mbowe mashamba yake yariharibiwa kisa kuwa karibu na chanzo cha maji sasa misri wanatumia sheria hiyohiyo iliyotumika kumuharibia mbowe mashamba, ingawa mimi sioungi mkono hii sheria maana haiwezekani ziwa lote lile turuhusiwe kuvua samaki tu bila kunywa yale maji
Misri unajua wanabwawa mangapi ya kufua umeme?
 
Tanzania tukiacha Ethiopia waonewe, nasi zamu yetu inakuja, hivyo wakiigusa Ethiopia, wajue na Tanzania wameipiga
Mkuu Tz na nchi nyingine za kiafrika hazina uwezo wa kuisaidia Ethiopia hata kidogo .
Wenye uwezo wa kuibana Misri ni nchi za magharibi ambazo kimsingi wao ndio chanzo cha tatizo kwa sababu ndizo zilisaini mkataba huo unao ipa Misri nguvu ya kuimiliki mto naili.
Mkuu na kuhakikishia iwapo kutatokea vita Ethiopia itapigwa huku viongozi wa kiafrika wakitizama tu hakuna ataye jaribu kubweka.
 
Kwa Wamisri maji ya mto Nile ndio roho yao pekee. Hawana mbadala, Ni ama wafe wote au wapone wote kutetea maji hayo.

Sema tu Misri na sudani lazima walazimishwe kuchangia gharama za utunzaji wa vyanzo vya maji hayo nakusaidia upatikanaji wa maji na nguvu za umeme kwenye nchi za bonde la mto Nile ili zisishiawishike kutumia maji ya Nile kwa matumizi ya nyumbani, umeme na kilimo. Maana Ni upuuzi Mwanza wafe kiu lakini ziwa Victoria lipo kwaajili ya Misri
Basi wacha wafe wote
 
Na ndiyo maana nimeitadharisha Ethiopia licha ya kuonekana iko upande wa haki lakini isije kujitoa ufahamu itakuja kukumbana na kipigo cha mbwa koko.
Arudia itapata kipigo cha mbwakoko.
Ni bora upigwe ijulikane moja, lakini sio kupokwa haki, kwenye uonevu hakuna amani ya kweli, ni kudanganyana tu
 
Lakini mm nisichokifahamu Ni kivipi bwawa hili la Ethiopia litawaathili watu wa Egypt. Nijuavyo mm baada ya bwawa hili kujaa maji yatarudi tena mto Nile na kuendelea na safari ya kuelekea Egypt tena, Kama Ni athali ni za muda tu wakati wa kulijaza.
 
Hayo ni maji ya chumvi. Gharama za kuyatreat na teknolojia yake ngumu wanayotumia Israel haipatikani Misri. Hata hivyo mkataba wa mabeberu uliwapa haki hiyo, kama hawatokubaliana mezani lolote litatokea. Wiki hii kuna delegation ya Misri ilikuwa Somaliland wakizungumza possible military base, Somaliland na Ethiopia wanapakana.
Hakuna shida, Somalia akithubutu kuruhusu hiyo base, kabla haijawa established tunaichakaza Somali yote, total annihalation
 
Kama Kuna kosa kubwa ambalo nchi za bonde la Nile watalifanya Ni kujifanya mzozo wa Ethiopia na Egypt hauwahusu. Kwavyovyote vile Vita ya Ethiopia dhidi ya Egypt kwaajili ya matumizi ya maji ya mto Nile lazima iwe yao wote. Vinginevyo itakuwa mwenzio akinyolewa tia zako maji. Tutapigwa mmoja baada ya mwingine kuhusu maji haya.
Mkuu ninavyo wajua viongozi wetu wa kiafrika ,Ethiopia ata pigwa mpaka ata chakaa huku wakitizama na hakuna ataye jaribu kubweka.
Ndio maana nimetahadharisha hapo mwanzo ya kuwa Ethiopia isije kujiingiza kwenye vita na Misri kwa kutegemea ya kwamba waafrika wenzake watamsaidia.
 
Back
Top Bottom