Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Mlima Kilimanjaro upo ndani ya mipaka ya nchi gani? Ziwa Tana na blue nike ipo ndani ya mipaka ya nchi gani? Jaribu kutumia akili yako yote next time
Unatumia vigezo gani kusema mlima Kilimanjaro uko kwenye mipaka ya Tanzania. Vigezo hivyo viliwekwa na nani?
Sheria zilezile zinazotambua Kili kuwa Tanzania ndizo kama hizo zinatambua maji ya Nile yasitumiwe nje ya mkataba. Sio mimi niliyesema, ni mabeberu.

Kama unadhani sina akili toka kwenye uzi huu anzisha uzi wako uni-tag.
 
  • Thanks
Reactions: RTI
... pia kingine ni wakati muafaka kwa Misri kuwa na proper birth control kuhakikisha population yao ni proportional na resources ya (sio za) maji waliyo nayo - The Nile. Wanajua the only water source waliyo nayo ni hiyo for everything drinking, industrial, irrigation, etc. whatever you name halafu kwa kuzaliana hawajambo; I think third in Africa after Nigeria and Ethiopia. Wawe na mpango wa makusudi wa kudhibiti ongezeko la watu vinginevyo soon itakula kwao hata ya kunywa watayakosa wakifanya mchezo.

Mkuu RTI kasema Ethiopia wasijitoe ufahamu kujipima kifua na Misri ni kweli, Misri wako mbali kijeshi kuliko Ethiopia, lakini hata wakipigwa leo hawatalala nao watakuwa na mpango wa muda wa kati na mrefu 25, 50, 100 years kuja ku-retaliate. Ni kama China, Iran, NK leo wanavyotunishiana misuli na US wakati miaka michache iliyopita walikuwa si lolote.

So, in the long run, millitary approach might not be useful for Egypt, badala yake mipango madhubuti ya kuendana na resources zitakazokuwa zinapatikana by then. Of course hii inahusu nchi zote sio kufyatua fyatua ovyo wakati unajua resources za kulisha na kunywesha watu wako ni finyu.
Ethiopia acha afyatue, maji yako ndani ya mipaka yake, acha atumie rasilimali yake!!
 
Hakuna shida, Somaliland akithubutu kuruhusu hiyo base, kabla haijawa established tunaichakaza Somali yote, total annihalation
Somaliland aruhusu base ya Egypt wewe upeleke pua yako? Mbele ya Egypt unaenda kufanya nini, kutumia nini?
Unaenda pigana na Mig-35 kwa kutumia J-7G, Abrams kwa kutumia nini?

Then kuna ulazima gani wa kupigana na Somaliland kisa imeruhusu base ya Egypt? Au unadhani vita wanaamua tu kama movie zako za Rambo.
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?
Kusini🤣😂🤣!
 
Mkuu Tz na nchi nyingine za kiafrika hazina uwezo wa kuisaidia Ethiopia hata kidogo .
Wenye uwezo wa kuibana Misri ni nchi za magharibi ambazo kimsingi wao ndio chanzo cha tatizo kwa sababu ndizo zilisaini mkataba huo unao ipa Misri nguvu ya kuimiliki mto naili.
Mkuu na kuhakikishia iwapo kutatokea vita Ethiopia itapigwa huku viongozi wa kiafrika wakitizama tu hakuna ataye jaribu kubweka.
Inategemea unaposema haina ‘uwezo’ unamaanisha nini, kwamba yaani hatuwezi hata kidogo kuwasaidia? Tusiweze kivipi? Kwamba Tanzania ni nchi ya vilema pekee? Your statement is ‘Pure FALLACY,!!!
 
Mafarao walikuwa weusi, hao ni wakimbizi toka wanakokujua wenyewe, probably Arabia, tumia akili yako yote
Umetumia probably halafu unataka niamini unachokisema! Toa nyaya na ma switch uliyojaza kichwani weka ubongo tuanze kukutofautisha na roboti
 
Lakini mm nisichokifahamu Ni kivipi bwawa hili la Ethiopia litawaathili watu wa Egypt. Nijuavyo mm baada ya bwawa hili kujaa maji yatarudi tena mto Nile na kuendelea na safari ya kuelekea Egypt tena, Kama Ni athali ni za muda tu wakati wa kulijaza.
At the back of my mind, hili ndilo linaloniumiza kichwa, maana bwawa la kufua umeme haliconsume maji, bali hurusu yaoite kuendelea na safari yake, kinachovunwa ni ile potential energy ya maji na kugeuzwa kuwa umeme, so hata mimi niko puzzled
 
Mzee nahisi hujanielewa, misri hayuko kwenye chanzo cha maji, sheria inakataza kuchepusha maji kutokea kwenye chanzo
Sijakuelewa, kwamba unahitaji kuchepusha maji ili kuzalisha umeme, kwani ni kilimo cha umwagiliaji wanachojenga?
 
Mkuu ninavyo wajua viongozi wetu wa kiafrika ,Ethiopia ata pigwa mpaka ata chakaa huku wakitizama na hakuna ataye jaribu kubweka.
Ndio maana nimetahadharisha hapo mwanzo ya kuwa Ethiopia isije kujiingiza kwenye vita na Misri kwa kutegemea ya kwamba waafrika wenzake watamsaidia.
Endelea kusali na kuomba, ila haonewi mtu hapa, yaani mwenzetu anyolewe halafu sisi kazi kuweka maji kwenye nywele zetu?! No way!!!
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?
Tunapaswa kuwa referee.
 
Huu ugomvi wa maliasili ni mgumu sana.

Huwa nafikiria (theoretically tu) hivi Misri akitutaka tuzuie maji kutoka Victoria yasitiririke kwenda kwake, tutayapeleka wapi? Au tunachimba mto yaende Tanga? Baharini?
Yeye ndio ayazuie, kama anaweza
 
Inategemea unaposema haina ‘uwezo’ unamaanisha nini, kwamba yaani hatuwezi hata kidogo kuwasaidia? Tusiweze kivipi? Kwamba Tanzania ni nchi ya vilema pekee? Your statement is ‘Pure FALLACY,!!!
Kwa hiyo kama sio vilema mtapiga mbizi kufika Misri kuipiga. Au mtatumia mitumbwi kwenda Suez canal?
Misri ina wanajeshi active zaidi ya laki moja. Rais wao wa sasa ni Field Marshall, anatumia sana budget kwenye jeshi. Misri kamdindia Turkey pale Libya na yupo anajiandaa kupeleka majeshi ndo huyuhuyu unataka tumchangie.

Vita hautatumia mapanga na mishale mnayotumia uko kwenu Tarime.
 
Akileta ujinga maji yatakuwa poisoned yeye ashambulie na ndege zake tu ila asiyatumie kabisa
... ni kosa baya kabisa kufanya hivyo! Atakuwa hapigani tena vita na Egypt but the world; at least majority. Kuna sheria kali kabisa zinazozuia uhalifu wa aina hiyo maana sumu inauwa kila kitu binadamu na bayo anuai yote all the way downstream and even far beyond to Europe (Mediterranean)! Yaani uwapelekee Ulaya sumu wakutizame tu kisa unamkomoa mbaya wako? Duh; stop thinking of that nonsense please!
 
Akileta ujinga maji yatakuwa poisoned yeye ashambulie na ndege zake tu ila asiyatumie kabisa
Akionyesha dalili za kutaka kushambulia tu, tunajaza sumu ya panya maji yote kutoka mpaka wa Ethiopia kwenda mbele, tukose wote, akijitoa akili na sisi tunajinyofoa ubongo kabisa, liwalo na liwe!!
 
... ni kosa baya kabisa kufanya hivyo! Atakuwa hapigani tena vita na Egypt but the world; at least majority. Kuna sheria kali kabisa zinazozuia uhalifu wa aina hiyo maana sumu inauwa kila kitu binadamu na bayo anuai yote all the way downstream and even far beyond to Europe (Mediterranean)! Yaani uwapelekee Ulaya sumu wakutizame tu kisa unamkomoa mbaya wako? Duh; stop thinking of that nonsense please!
Liwalo na liwe, walikuwa wapi wakati Misri anafanya huo uonevu dhidi ya sovereign state?!
 
Back
Top Bottom