Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

... si tu Ethiopia anauhitaji huo umeme kwa matumizi ya nyumbani bali anauhita pia kibiashara kuuza mataifa jirani. Pagumu sana hapo.
 
Sijakuelewa labda unisahihishe umesema Ethiopia ni chanzo kikuu cha mto nile,kivp wakati tunajua souce kubwa ni ziwa victoria
... chanzo kikuu cha R. Nile ni milima ya Abyssinia (Ethiopia) ambayo huchangia karibu 85% kupitia Blue Nile wakati L. Victoria and other tributaries huchangia roughly 15%. L. Victoria ni kubwa tu in terms surface area not in terms of volume.

Hivi unajua L. Tanganyika ni la ngapi kwa ukubwa duniani kwa kuhifadhi maji baridi? Ni la pili; it is extremely huge by far in terms fresh water volume than L. Victoria which is very shallow while L. Tanganyika is so deep!
 
Kwani sisi tunapotumia matrillion ya pesa kutunza mazingira ili mvua zinyeshe na hatimae kujaza huo mto, huwa wanatuconsider vipi wao misri kama misri, huwa wanatupa pesa ya carbon credit? Au wanasubiri maji tu bila kujua tunavyotaabika huku kutunza vyanzo vya maji? Wajinga nini?
 
Vita kwa ajili ya maji haiko mbali, chanzo halisi cha mto Nile ni Lake Victoria. Time will tell
... inategemea unamaanisha nini unaposema "chanzo halisi" but the fact is that Blue Nile originating from the Abyssinian Highlands (Ethiopia) contributes 85% of the Great Nile waters while White Nile (L. Victoria) only 15%. That's the fact.
 
... uko sahihi; Blue Nile originating from the Abyssinian Highlands (Ethiopia) contributes 85% of the Great Nile waters.
 
Mama Tanzania hafungamani na pande yoyote ile.....
Huo ni ujinga, Misri alishwahi kutuzuia eti tusipeleke maji ya ziwa victoria kwa wananchi wa Tabora, hata sijui walipata wapi jeuri ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu, very arrogant, ila Lowassa aliwanyoosha, wakatulia
 
Hilo bwawa limejengwa along blue, white or the greater nile?
 
Mikataba ambayo pande zote tunakubaliana nayo haina shida, especially mipaka, ila kwa amabayo hatukubaliani nayo, waingie vitani kama wako tayari, au la tukae chini tuzungumze, uamuzi ni wao hao Egypt, na kwakuwa Egypt anataka kutumia huo mkataba kukandamiza nchi zingine zote, basi awe tayari kupigana nazo zote vita, maana hata sisi tulishaletewa vikwazo wakati tunajenga mradi wa maji wa ziwa victoria kwenda mikoa ya kaskazini, the agreement defies logic, its nonsensical, tutaingia vitani au laa wakubali mazungumzo kuvunja huo mkataba
 
Uko sahihi, Namimi nilijuwa hivyo
 
Wao wanapotoa hewa za ukaa viwandani na kutetea ukame Afrika na watu kufa njaa, huwa tunaenda kuwafungia viwanda vyao?!
 
Kama Kuna kosa kubwa ambalo nchi za bonde la Nile watalifanya Ni kujifanya mzozo wa Ethiopia na Egypt hauwahusu. Kwavyovyote vile Vita ya Ethiopia dhidi ya Egypt kwaajili ya matumizi ya maji ya mto Nile lazima iwe yao wote. Vinginevyo itakuwa mwenzio akinyolewa tia zako maji. Tutapigwa mmoja baada ya mwingine kuhusu maji haya.
 
Misri unajua wanabwawa mangapi ya kufua umeme?
 
Tanzania tukiacha Ethiopia waonewe, nasi zamu yetu inakuja, hivyo wakiigusa Ethiopia, wajue na Tanzania wameipiga
Mkuu Tz na nchi nyingine za kiafrika hazina uwezo wa kuisaidia Ethiopia hata kidogo .
Wenye uwezo wa kuibana Misri ni nchi za magharibi ambazo kimsingi wao ndio chanzo cha tatizo kwa sababu ndizo zilisaini mkataba huo unao ipa Misri nguvu ya kuimiliki mto naili.
Mkuu na kuhakikishia iwapo kutatokea vita Ethiopia itapigwa huku viongozi wa kiafrika wakitizama tu hakuna ataye jaribu kubweka.
 
Basi wacha wafe wote
 
Na ndiyo maana nimeitadharisha Ethiopia licha ya kuonekana iko upande wa haki lakini isije kujitoa ufahamu itakuja kukumbana na kipigo cha mbwa koko.
Arudia itapata kipigo cha mbwakoko.
Ni bora upigwe ijulikane moja, lakini sio kupokwa haki, kwenye uonevu hakuna amani ya kweli, ni kudanganyana tu
 
Lakini mm nisichokifahamu Ni kivipi bwawa hili la Ethiopia litawaathili watu wa Egypt. Nijuavyo mm baada ya bwawa hili kujaa maji yatarudi tena mto Nile na kuendelea na safari ya kuelekea Egypt tena, Kama Ni athali ni za muda tu wakati wa kulijaza.
 
Hakuna shida, Somalia akithubutu kuruhusu hiyo base, kabla haijawa established tunaichakaza Somali yote, total annihalation
 
Mkuu ninavyo wajua viongozi wetu wa kiafrika ,Ethiopia ata pigwa mpaka ata chakaa huku wakitizama na hakuna ataye jaribu kubweka.
Ndio maana nimetahadharisha hapo mwanzo ya kuwa Ethiopia isije kujiingiza kwenye vita na Misri kwa kutegemea ya kwamba waafrika wenzake watamsaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…