Ukitaka kujua kichwa chako kimejaa funza jijibu maswali haya
1.) Ethiopia ilikuwa ni Koloni la nani? Au ilikuwa ni taifa huru lenye maamuzi yake juu ya mambo yake?
2.) Kwenye huo mkataba , Ethiopia alisaini?
Britain hakuwa na haki ya kugawa maji mto Abbay (Blue nile) kwa sababu yeyote ile iwe ya kupeana zawadi au kulipana madeni, kwa sababu hakuwa na mandate katika himaya ya wahabeshi at the time of the agreement, waEthiopia wenyewe ndio walipaswa watoe hiyo ridhaa kwa wamisri kuwapa hayo maji, hilo halikutokea, hivyo wamisri walipewa maji toka kwenye makoloni ya Britain (Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan), lakini maji toka Ethiopia hayapaswi kuhusishwa kwenye huo mkataba.
kuhusu mipaka, Ethiopia au taifa lolote lile halikuwepo kabla ya mipaka, kwa kuwa mabishano ni baina ya nchi na nchi zenye mipaka, tuna assume wote tumekubaliana juu ya mipaka na hilo halina mjadala.
(kukushibisha tu zaidi, Hiyo Kenya na Tanzania unayotolea mfano ilikuwa under british rule, hao Egypt na Sudan walikuwa under british rule)