Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Misri inatumia ile mbinu ya kijeshi ya "jasho jingi kabla ya Vita damu kidogo wakati wa Vita". Inapiga mkwara mwingi ili watu wakae mbali na maji hayo. Inafahamu kabisa kuwa hayo maji yanaweza Kutiwa sumu na maadui zake Kama Vita ya maji hayo itatokea, inafahamu kuwa vyanzo vya mto huo vinaweza kuharibiwa kabisa na maji kupungua Kama vile ilivyopungua barafu ya mlima Kilimanjaro, inafahamu kuwa hakuna taifa linaweza kufa kiu huku wakiyaangalia maji yanaelekea Egypt.
Nimependa hiyo point ya mwisho, eti unakufa kiu huku maji yanatiririka kwenda Egypt uyaangalie tu, sasa si bora ufe vitani kuliko kufa kiu?
 
Kutofungamana na upande wowote ilikuwa Ni with respect to Cold War, West vs East, Tena by defacto ilikuwa East

Kwenye hili la Egypt na Ethiopia sio cold War.
Hakuna nchi ambayo haina upande Duniani

Usikariri matukio. What matters is the concept and its application. Kama wewe ni lazima utake side, it is ni wewe lakini sisi Tanzania hatuna side. Ndiyo ilivyo.
 
utata upo hapo jinsi ya kulijaza hilo bwawa Ethiopia wanataka kulijaza kwa mkupuo yaani wachepusha maji mpaka bwawa lao lijae na ili hilo bwawa lijae linaweza kutumia miezi 6 mpaka mwaka 1

misri yeye anataka lijazwe kwa awamu kwamba maji kidogo yaelekezwe kwenye bwawa alafu mengi yaendelee to misri hii njia anayopendekeza misri itatumia miaka 3 au 5

all in all hawawezi kuingia vitani nadhani Ethiopia anatafuta tu kupewa offer nzuri na wamisri
Yaani mtu afanye uwekezaji mkubwa hivyo halafu alijaze bwawa kwa miaka mitano? Kwani si kuna maji mengine yanatokea Victoria? Watayamaliza kwa kunywa yote hayo? Either way, mtu chake, atumie anavyotaka!
 
Kutokuwa upande wowote hakumaanishi kupanga msururu. Ni fursa nzuri ya kusimamia uratibu wa kinachobishaniwa ili kuleta mtangamano sahihi wa haki kwa siyo pande zinazobishana tu, lakini pia na pande zingine zenye maslahi katika suala la aina ile ama lile lile.

Nilivyoelewa mimi, kama niko nje, nisahihishwe, Maana ya methali kwamba "mwenzio akinyolewa nywele zako tia maji", haina maana kwamba usubiri ujiandae kunyolewa. Bali ni tia maji kichwani ili usinyolewe!. Au vipi?
Kuweka maji kichwani kuna zuiaje usinyolewe? Maji huounguza tu maumivu ya kunyolewa
 
Usikariri matukio. What matters is the concept and its application. Kama wewe ni lazima utake side, it is ni wewe lakini sisi Tanzania hatuna side. Ndiyo ilivyo.
Lazima uwe na side Sababu lazima katika mtafaruku fulani lazima uwe na opinion unless uwe hujui chochote kuhusu kinachoendelea

, na ukiwa na opinion Katka side mbili lazima utakuwa unawaza hii side hii ndio ipo sahihi kuliko Ile, na kwa namna fulani uta support side ambayo unaona ipo sahihi japo unaweza usiwe direct

So hakuna mtu ambaye Hana side, labda awe ignorant ya mambo yanayotokea

Tanzania ime support causes mbalimbali za kisiasa tu, usijidanganye eti ipo neutral, ime support Biafra,ime support Western Sahara, ime support Palestine, hata wakati wa Vita baridi ime support China na Cuba..so hakuna kitu kinaitwa kutokufungamana labda usiwe concious
 
Lazima uwe na side Sababu lazima uwe na opinion, na ukiwa na opinion Katka side mbili lazima utakuwa unawaza hii side hii ndio ipo sahihi kuliko Ile, na kwa namna fulani uta support side ambayo unaona ipo sahihi japo unaweza usiwe direct
So hakuna mtu ambaye Hana side, labda awe ignorant ya mambo yanayotokea

Tanzania ime support causes mbalimbali za kisiasa tu, usijidanganye eti ipo neutral, ime support Biafra,ime support Western Sahara, ime support Palestine, hata wakati wa Vita baridi ime support China na ilikuwa karibu na mataifa ya Mashariki Kama Cuba..so hakuna kitu kinaitwa kutokufungamana labda usiwe concious

Ukiwa kwenye msingi wa mediation you are not supposed to take side. Kila upande (Nimesema mwanzoni kabisa) una pande zote. Hata hivyo hii wataelewa zaidi watu wa conflict resolutions, kazi aliyokuwa akifanya Mwl muda wote na baada ya uongozi.
 
Kwani Tz imeshaingia kwenye mediation kwenye huu mgogoro?
We ulichosema sera yetu Ni kutofungamana na upande wowote, ndio nikajibu, in practice Tz imefungamana sanaa
 
Tutauza wapi? Gesi yetu tunaiuza wapi?
Gesi hatuwezi kuuza nje wakati umeme uliopo hatujitoshelezi. Mkoa Kagera nakumbuka walikua wanatumia umeme kutokea Jinja Uganda na Sina uhakika Kama wameshaungwa kwenye grid ya taifa ya umeme. Ila bwawa la mwl Nyerere liloko Rufiji likiwa tayari, tutakuwa na surplus production of energy source jambo litakalopelekea kuuza nje umeme wa ziada hasa kwa nchi jirani.
 
Hivi unagombaniaje mali iliyo ndani ya mipaka ya mwenzio, hapo hakuna kugombania, hapo ni kuporana, tofautisha
Tatizo Ni kuwa wao wamepewa hiyo haki ya kuyamiliki maji ya Nile sawa na Tanzania ilivyopewa haki ya kuumiliki mlima Kilimanjaro wote hata Kama unaona mpaka umepindishwa kwa makusudi ili mlima wote ubakie Tanzania.
Wakoloni waliyafanya haya yote wakiwa na akili timamu kwa maslahi yao. Wakati mwingine walikuwa wanalipana madeni kwenye Mali zetu. Mfano, ujerumani inaweza kugawiwa kaeneo kadogo (e.g. Rwanda) huku East Africa na kulipwa kaeneo kengine au kitu chochote huko Asia. Ukiuliza sababu ya kwanini nchi nyingine zilifanywa kuwa kubwa na nyingine ndogo sana unaweza kupandwa na hasira. Kwa bahati dunia imekubaliana na hili kila nchi Leo inailinda mipaka ya nchi yake iliyowekwa na wakoloni na haitaki kuachia mtu hata futi moja; kisa nimepewa na mkoloni. Kwahiyo siishangai Egypt kudai maji ya Nile Ni yake pia. Dialogue ndiyo solution.
 
Ntarudi.....
Ni matumaini yangu ukipata muda siku yoyote, utakuja kututendea haki wana-JF! I know hili ni eneo lako la kujidai... sie wengine hili sio eneo letu, na kwahiyo tunasukumwa sana na economic idiology kuliko diplomacy!! Sie wengine kwetu ni kama kule ambako ndugu yangu residentura alini-tag wiki kadhaa zilizopita, lakini nimetafuta ile tag hadi nimechoka!

Residentura, hivi unaweza kunijuza ile thread ya Mafuta, Gas, TPDC iliandikwa na nani ili iwe rahisi kuitafuta ile thread?
 
Ukitaka kujua kichwa chako kimejaa funza jijibu maswali haya
1.) Ethiopia ilikuwa ni Koloni la nani? Au ilikuwa ni taifa huru lenye maamuzi yake juu ya mambo yake?
2.) Kwenye huo mkataba , Ethiopia alisaini?

Britain hakuwa na haki ya kugawa maji mto Abbay (Blue nile) kwa sababu yeyote ile iwe ya kupeana zawadi au kulipana madeni, kwa sababu hakuwa na mandate katika himaya ya wahabeshi at the time of the agreement, waEthiopia wenyewe ndio walipaswa watoe hiyo ridhaa kwa wamisri kuwapa hayo maji, hilo halikutokea, hivyo wamisri walipewa maji toka kwenye makoloni ya Britain (Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan), lakini maji toka Ethiopia hayapaswi kuhusishwa kwenye huo mkataba.

kuhusu mipaka, Ethiopia au taifa lolote lile halikuwepo kabla ya mipaka, kwa kuwa mabishano ni baina ya nchi na nchi zenye mipaka, tuna assume wote tumekubaliana juu ya mipaka na hilo halina mjadala.

(kukushibisha tu zaidi, Hiyo Kenya na Tanzania unayotolea mfano ilikuwa under british rule, hao Egypt na Sudan walikuwa under british rule)
 
Eti eneo langu la kujidai!!!! Tuombe uzima kaka, kichwa kipoe moto ntajitahidi kuchangia!
Maana hapa akili inafanya TIKTOK, TIKTOK nivumilie tu ndugu yangu!
 
Ukitaka kujua kichwa chako kimejaa funza jijibu maswali haya
1.) Ethiopia ilikuwa ni Koloni la nani? Au ilikuwa ni taifa huru lenye maamuzi yake juu ya mambo yake?
2.) Kwenye huo mkataba , Ethiopia alisaini?

Britain hakuwa na haki ya kugawa maji mto Abbay (Blue nile) kwa sababu yeyote ile iwe ya kupeana zawadi au kulipana madeni, kwa sababu hakuwa na mandate katika himaya ya wahabeshi at the time of the agreement, waEthiopia wenyewe ndio walipaswa watoe hiyo ridhaa kwa wamisri kuwapa hayo maji, hilo halikutokea, hivyo wamisri walipewa maji toka kwenye makoloni ya Britain (Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan), lakini maji toka Ethiopia hayapaswi kuhusishwa kwenye huo mkataba.

kuhusu mipaka, Ethiopia au taifa lolote lile halikuwepo kabla ya mipaka, kwa kuwa mabishano ni baina ya nchi na nchi zenye mipaka, tuna assume wote tumekubaliana juu ya mipaka na hilo halina mjadala.

(kukushibisha tu zaidi, Hiyo Kenya na Tanzania unayotolea mfano ilikuwa under british rule, hao Egypt na Sudan walikuwa under british rule)
Nakuvutia teke la korodani, subiri hapohapo uone...haha
 
Back
Top Bottom