Tanzania katika mtanziko; Hakuna umeme, sukari wala dola. Serikali inachukua hatua gani?

Tanzania katika mtanziko; Hakuna umeme, sukari wala dola. Serikali inachukua hatua gani?

Tanzania hakuna umeme, sukari wala dola.

Huku tukiambiwa kuwa awamu hii uchumi unakua kuliko awamu yoyote ile, makusanyo ya TRA yakivunja rekodi.

Tatizo la umeme nalo limekua sugu bila kupata ufumbuzi wa kudumu na hali ikizidi kuwa mbaya kila siku.

Sukari nayo kila mtu anauza anavyojisikia.

Uhaba wa dola nao ukishika kasi.

Kama kweli uchumi unakua, itakua ajabu kama dola zitaadimika.

Maana factor moja wapo ya kukua kwa uchumi ni ongezeko la mauzo ya nje , na mauzo ya nje ni fedha za kigeni. Dola inaadimikaje.

Kukua kwa uchumi means ongezeko la uzalishaji.

Uzalishaji unaongezekaje kama hakuna nishati ya uhakika??

Kukua kwa uchumi means bei ya bidhaa kuwa stable, huu uchumi wa kukamiana kwa bei za bidhaa ni kwa baadhi ya wafanyabiashara tu sio wananchi.

Viongozi wetu hatuwaoni wakijihusisha na mambo haya.

Serikali ina mpango gani kuaddress hizi issues.?



Tatizo sio serikali tena ni wananchi. Jiulize wewe umefanya nini? Je umeshiriki maandamano ya kulalamika na kudai katiba mpya. Au unategemea serikali hiyo hiyo ikupe majibu. Wakati mwingine wakulaumu ni wananchi mazuba na sio wanaserikali ambao wenyewe wana jenereta, magari na nyumba kwa pesa yenu. Kama hamlalamiki na kuandamana mnasubiri wawajibu mtasubiri sana
 
Pamoja na shida zote hizo, lakini utakuta majitu majinga yanayoipambania CCM ndio hao hao wanaopigika na shida hizi ziletwazo na ccm.
Unajiuliza hivi hawa wana akili timamu au wamelogwa? Maana haiwezekani ambaye zinamtosha kutenda hivyo

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Leo ni wiki ya pili hakuna maji dar
Umeme hakuna
Bidhaa zinapanda bei
Unamkuta mjinga mmoja anakuambia haoni wanaoandamana wanapoteza muda
Waafrica tuna matatizo sana aisee ndo mana wazungu wanatudharau
 
Back
Top Bottom