JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Rais Samia amesema Tanzania ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza chanjo za UVIKO-19 ikiwa ni juhudi za kupambana na janga hilo pamoja na magonjwa mengine.
Rais Samia amesema hayo wakati akifanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Ulaya, Bw. Charles Michel, jijini Brussels nchini Ubelgiji ambapo amemwambia Bw. Michel kuwa Tanzania inalenga kuwa mzalishaji na msambazaji wa chanjo hizo katika nchi za EAC pamoja na SADC.
Akielezea umuhimu wa hatua hiyo, Rais Samia amesema kuna uwezekano wa Tanzania kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 216 katika uingizaji wa chanjo ifikapo mwaka 2030.