#COVID19 Tanzania kuanza kuzalisha chanjo zake za COVID-19

#COVID19 Tanzania kuanza kuzalisha chanjo zake za COVID-19

Rais Samia amesema Tanzania ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza chanjo za UVIKO-19 ikiwa ni juhudi za kupambana na janga hilo pamoja na magonjwa mengine.

Rais Samia amesema hayo wakati akifanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Ulaya, Bw. Charles Michel, jijini Brussels nchini Ubelgiji ambapo amemwambia Bw. Michel kuwa Tanzania inalenga kuwa mzalishaji na msambazaji wa chanjo hizo katika nchi za EAC pamoja na SADC.

Akielezea umuhimu wa hatua hiyo, Rais Samia amesema kuna uwezekano wa Tanzania kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 216 katika uingizaji wa chanjo ifikapo mwaka 2030.

View attachment 2120326
Sijui ni mimi tu au la... Huyu Mwandishi anaandika kama vile bado yeye sio sehemu ya serikali hiyo, ni kama vile yeye bado ni mwajiliwa wa sehemu fulani na analipoti tu kilichotokea... Kasoro hii irekebishwe haraka
 
sasa anataka kukimaliza kizazi cha watanganyika….
 
Baada ya ugonjwa kuisha wao ndiyo wanaanza kuzalisha? shame on them si walikuwa na tangawizi sijui mapapi ni dawa ya corona vimefia wapi?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha chanjo za UVIKO-19 na maradhi mengine ndani ya Nchi kama njia moja ya kutimiza mipango ya Serikali ya kukabiliana na ugonjwa wa corona na magonjwa mengineyo.

Katika mazungumzo yake na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel Brussels nchini Ubelgiji, Rais Samia amesema Tanzania inataka kuwa muuzaji wa chanjo za kuokoa maisha kwa Jamii ya Afrika Mashiriki (EAC) na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Amesema bajeti ya Serikali ya kununua chanjo inadhaniwa itaongezeka kutoka Tsh Bilioni 26.1 mwaka 2020 hadi Bilioni 216 mwaka 2030 ambayo ni sababu maalum ya kujenga kiwanda hicho.
FB_IMG_1645012820130.jpg
 
View attachment 2121035
mwambie Rais hatuhitaji kiwanda cha chanjo ya uviko 19, tunahitaji kiwanda cha mbolea.

Ova...
 
mwambie Rais hatuhitaji kiwanda cha chanjo ya uviko 19, tunahitaji kiwanda cha mbolea.

Ova...
Mimi sio swahiba wake makamba mkuu nadhani ungemtafuta yeye angefikisha ujumbe vizuri.
 
Back
Top Bottom