Tanzania kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji; wawindaji kuruhusiwa kuua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee

We Fala tu huna unalojua
Mwaka juzi tulikuwa tunajenga Hekalu la Mkuu wa Dawoodi Bohra pamoja na Villa zingine kule Ipole kwenye kitalu kinachomilikiwa Na wahindi Wa AFRICAB ADVENTURE (UGUNDA CAMP).
Tulikuwa Mafundi na vibarua zaidi ya 100, jamaa walikuwa wakiwamanua tu nyati, kudu na wanyama wengineo then wanachukua maini na nyama tunapikiwa kama mboga.
miezi 8 tuliyokaa kule tumewala sana hao wanyama pori na jamaa wa mali asili wanakujaga kuzuga zuga tu then wanasepa sosioni jipya hapa

Sema hutaki kuelewa. Ni kwanini wamasai wanafukuzwa kwenye Ardhi yao ya asili?
Hawafukuzwi ila wanahamishwa ili kulinda hifadhi dhidi ya kupungua wanyama sababu ya ongezeko la watu na mifugo kupita uwezo wa hifadhi.
 
Jibu hoja hizo; pia ni kwanini hadi leo hatujapata hayo maendeleo wakati tumekuwa tukiua wanyama tangu uhuru, leo kimebadilika nini kitakachotuletea hayo maendeleo?
Na nchi sihami vilevile
Kupata au kutopata maendeleo hakusababishwi na kuua au kutokuua wanyama,ila inatokana na shughuli za uzalishaji mali na kiuchumi ndani ya nchi husika.

Kuua au kuuza wanyama hai nje ya nchi ni njia moja wapo ya kuongeza kipato kwa serikali husika, Sasa matumizi ya hizo fedha zinazopatikana ni jukumu linalobaki kwa serikali husika.
 
Hawafukuzwi ila wanahamishwa ili kulinda hifadhi dhidi ya kupungua wanyama sababu ya ongezeko la watu na mifugo kupita uwezo wa hifadhi.
😂😂😂😂😂, kwahiyo mnatoa vibali vya kuua wanyama ili waongezeke si ndio? Hakyaaaanani, kweli taahira sio hadi uokote makopo
 
Kupata au kutopata maendeleo hakusababishwi na kuua au kutokuua wanyama,ila inatokana na shughuli za uzalishaji mali na kiuchumi ndani ya nchi husika.

Kuua au kuuza wanyama hai nje ya nchi ni njia moja wapo ya kuongeza kipato kwa serikali husika, Sasa matumizi ya hizo fedha zinazopatikana ni jukumu linalobaki kwa serikali husika.
Sasa kama tumekuwa tukiuwa wanyama na hayo maendeleo mnayosema hatukuyapata, ni vipi tutayapata kwa mauaji ya awamu hii? Nini kimebadilika?

Pia kwanini wamasai wafukuzwe kwenye maeneo yao ya asili ili waje waarabu kuua wanyama, why?!
 
😂😂😂😂😂, kwahiyo mnatoa vibali vya kuua wanyama ili waongezeke si ndio? Hakyaaaanani, kweli taahira sio hadi uokote makopo
Kuwinda wanyama kwa ajili ya kitoweo na fedha za kigeni hufanyika miaka mingi tu hapa Tz....halafu wanyama huwindwa kwenye vitalu tu ( vya uwindaji) na sio hifadhi za taifa.

Huko vitaluni wanyama wakiwa wengi ni vizuri wawindwe ili nchi ipate mapato kuliko wageuke usumbufu kwa wananchi wanaoishi pembeni mwa vitalu.
 
Sasa kama tumekuwa tukiuwa wanyama na hayo maendeleo mnayosema hatukuyapata, ni vipi tutayapata kwa mauaji ya awamu hii? Nini kimebadilika?
Wanyama wanawindwa kama njia ya kupata vitoweo,ngozi na fedha za kigeni (utalii wa uwindaji) hivyo hakuna kosa hapo.

Serikali imesema fedha zitatumika kuboresha maisha ya jamii zilizo pembezoni mwa hayo maeneo ya vitalu.....ni vipi watafanya hilo wanajua wao.

Pia kwanini wamasai wafukuzwe kwenye maeneo yao ya asili ili waje waarabu kuua wanyama, why?!
Wamasai wanahamishwa tu ili kuilinda hifadhi ya Ngorongoro sio kufukuzwa.

hilo la waarabu kuja kuua wanyama umelipata wapi ?, Kama ni kuwinda hata wazungu na waafrika pia wanawinda.
 
Mama mtawala ni taifa la nje lakini anaitawala TZ hana uchungu wowote na Tanganyika
Kama mnaona mama siyo mtz basi tuvunje muungano tugawane fito maana mmezidi sana ubaguzi wakati nyie ndio mmeukumbatia muungano
 
Kuwinda wanyama kwa ajili ya kitoweo na fedha za kigeni hufanyika miaka mingi tu hapa Tz....halafu wanyama huwindwa kwenye vitalu tu ( vya uwindaji) na sio hifadhi za taifa.

Huko vitaluni wanyama wakiwa wengi ni vizuri wawindwe ili nchi ipate mapato kuliko wageuke usumbufu kwa wananchi wanaoishi pembeni mwa vitalu.
Kwamba kitu kimekuwa kikifayika miaka mingi hata kama ni kiovu tukiache tu kiendelee, kuna jamaa hapo juu katokea mfano wa shoga anaeambiwa aache ushoga, halafu yeye anakazana kwamba ku-f-r ** hajaanza leo, kwahiyo huo ndio utetezi wake, aachwe tu aendelee kisa hajaanza leo?!

Hilo la kusema wanawindwa kwenye vitalu nani kabisha?Regardless ni ndani au nje ya vitalu, wanyama hao wasiuwawe, waachwe kwa ajili ya utalii utakaotuingizia pesa pia.

Wanyama mmeshaambiwa ni endangered species, halafu nyie mnasema wamekuwa wengi, kama sio si kurogwa ni nini hiki mnatetea?!
 
Wanyama wanawindwa kama njia ya kupata vitoweo,ngozi na fedha za kigeni (utalii wa uwindaji) hivyo hakuna kosa hapo.

Serikali imesema fedha zitatumika kuboresha maisha ya jamii zilizo pembezoni mwa hayo maeneo ya vitalu.....ni vipi watafanya hilo wanajua wao.

Wamasai wanahamishwa tu ili kuilinda hifadhi ya Ngorongoro sio kufukuzwa.

hilo la waarabu kuja kuua wanyama umelipata wapi ?, Kama ni kuwinda hata wazungu na waafrika pia wanawinda.
Fedha zilizokuwa zikipatikana kwa mauaji ya Simba tangu uhuru hazikuweza kufanya hayo, Leo nini kimebadilika kwamba mauaji ya awamu hii ndio yafanye hayo?

Wanahamishwa ili kulinda hifadhi?!, yaani mnalinda hifadhi kwa kugawa vibali vya kuua wanyama?! Ama kweli taahira si hadi uokote makopo.

Hilo la waarabu , hujui kampuni inaitwa OBC waliopewa awamu ya pili eneo la Loliondo, na sasa ndio wanataka kupewa lingine? muulize maulid Kitenge hapo chini aliyelipwa ili kuanzisha propaganda dhidi ya wamasai
 
Mama mtawala ni taifa la nje lakini anaitawala TZ hana uchungu wowote na Tanganyika
Ndugai hakukosea kusema tutapigwa mnada, bendera kurushwa Burj khalifa tuliambiwa bure, kumbe ndio wanakuja kutupiga mnada huku tunajiona, wamasai wanafukuzwa kama mbwa kwenye ardhi yao, inauma sana
 
Kama mnaona mama siyo mtz basi tuvunje muungano tugawane fito maana mmezidi sana ubaguzi wakati nyie ndio mmeukumbatia muungano
Sasa kama ni ukweli usisemwe, tunauzwa huku tunajiona, tunyamaze?!!
 
Kwamba kitu kimekuwa kikifayika miaka mingi hata kama ni kiovu tukiache tu kiendelee, kuna jamaa hapo juu katokea mfano wa shoga anaeambiwa aache ushoga, halafu yeye anakazana kwamba ku-f-r ** hajaanza leo, kwahiyo huo ndio utetezi wake, aachwe tu aendelee kisa hajaanza leo?!
Uwindaji wa wanyama haujawahi kuwa uovu.

Hilo la kusema wanawindwa kwenye vitalu nani kabisha?Regardless ni ndani au nje ya vitalu, wanyama hao wasiuwawe, waachwe kwa ajili ya utalii utakaotuingizia pesa pia.
Hata wanapowindwa wanatuingizia pesa za utalii.

Utalii wa kuangalia tu hautoshi (hata washindani wetu wana wanyama) , lazima tupanue wigo wa utalii ndio maana tuna vitalu vya kuwinda.
Wanyama mmeshaambiwa ni endangered species, halafu nyie mnasema wamekuwa wengi, kama sio si kurogwa ni nini hiki mnatetea?!
Hilo linafahamika ndio maana Faru mweusi huruhusiwi kuwinda ila walio wengi kama Simba, chui, nyumbu, mbogo na hata tembo hamna tatizo wakiwindwa maana wakizidi wanasumbua wakazi wa maeneo karibu na vitalu.
 
Fedha zilizokuwa zikipatikana kwa mauaji ya Simba tangu uhuru hazikuweza kufanya hayo, Leo nini kimebadilika kwamba mauaji ya awamu hii ndio yafanye hayo?
Hazikufanya hayo sababu haikuwa kipaumbele cha tawala hizo, ila kwa Sasa zitafanya maendeleo za hayo maeneo sababu ni kipaumbele cha utawala wa Sasa.

Wanahamishwa ili kulinda hifadhi?!, yaani mnalinda hifadhi kwa kugawa vibali vya kuua wanyama?! Ama kweli taahira si hadi uokote makopo.
Hifadhi itakayolindwa kwa kuhamisha watu ni Ngorongoro tu na sio vitalu vya uwindaji, usichanganye mambo.

Vibali vinatolewa kuwinda wanyama kwa ajili ya kitoweo au kama sehemu ya utalii kwenye vitalu vya uwindaji tu na sio kwenye hifadhi za taifa au kwenye mamlaka ya Ngorongoro.

Hilo la waarabu , hujui kampuni inaitwa OBC waliopewa awamu ya pili eneo la Loliondo, na sasa ndio wanataka kupewa lingine? muulize maulid Kitenge hapo chini aliyelipwa ili kuanzisha propaganda dhidi ya wamasai
Hilo la waarabu lina taarifa nyingi sana hivyo siwezi kulizungumzia

Hata kama watapewa eneo la kuwinda, haliwezi kuwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro maana mamlaka ya Ngorongoro sio kitalu cha uwindaji.
 
Uwindaji wa wanyama haujawahi kuwa uovu.

Hata wanapowindwa wanatuingizia pesa za utalii.

Utalii wa kuangalia tu hautoshi (hata washindani wetu wana wanyama) , lazima tupanue wigo wa utalii ndio maana tuna vitalu vya kuwinda.

Hilo linafahamika ndio maana Faru mweusi huruhusiwi kuwinda ila walio wengi kama Simba, chui, nyumbu, mbogo na hata tembo hamna tatizo wakiwindwa maana wakizidi wanasumbua wakazi wa maeneo karibu na vitalu.
Kufukuza wazawa kwenye ardhi yao ili waarabu waje waue wanyama si uovu? Au unadhani wale wamasai ni wanyama kama ngedere flani hivi, msijisahau hivyo, wale ni binadamu kama wewe na mimi, hata kama wanaishi porini na wanyama. Mnaonaje waZanzibari wote tuwahamishie Mtwara maana lile ni eneo la kitalii, kwamba wamekuwa wengi mno, hiyo imekaaje?

Kuingiza pesa kwa kuwindwa ni kitu cha mara moja, na ndio inakuwa imeisha hiyo, ila utalii wa kutazama hauwawi, ataendelea kuazamwa tena na tana huku tukiingiza pesa tena na tena, ni hesabu rahisi sana, ila sina hakika na uwezo wako wa kupiga hesabu ndogo

Kwamba utalii wa kutazama hautoshi, tukiwaua na wakabaki wachache, huo utalii wa kutazama ndio utatisha au utazidi kupungua, akili za wapi hizi?!

Hao Simba na Tembo umeshaambiwa ni endangered species, kiasi kusema wawindwe unaonekana mvuta ugoro tu mbele ya wenye akili...
 
Back
Top Bottom