Exorcist
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 1,235
- 1,268
Kipaumbele cha awamu hii ni tozo, kukopa na kulipa mariba ya hovyo hadi tupigwe mnada, pamoja na kuuwa endangered species na kujipendekeza kwa waarabu, hilo halina mjadala, hilo la kuwapa wamasai maendeleo ni porojo ulizoota ndotoniHazikufanya hayo sababu haikuwa kipaumbele cha tawala hizo, ila kwa Sasa zitafanya maendeleo za hayo maeneo sababu ni kipaumbele cha utawala wa Sasa.
Hifadhi itakayolindwa kwa kuhamisha watu ni Ngorongoro tu na sio vitalu vya uwindaji, usichanganye mambo.
Vibali vinatolewa kuwinda wanyama kwa ajili ya kitoweo au kama sehemu ya utalii kwenye vitalu vya uwindaji tu na sio kwenye hifadhi za taifa au kwenye mamlaka ya Ngorongoro.
Hilo la waarabu lina taarifa nyingi sana hivyo siwezi kulizungumzia
Hata kama watapewa eneo la kuwinda, haliwezi kuwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro maana mamlaka ya Ngorongoro sio kitalu cha uwindaji.
Hifadhi itakayolindwa ni Ngorongoro? Una maana gani? Sio vitalu vya uwindaji, una maana gani? Hiyo Loliondo waliyopewa OBC kwa ajili ya uwindaji walifukuzwa wamasai, sasa unaongelea nini hasa?
Hilo la waarabu liko wazi, walipewa kipindi cha Mwinyi eneo la Loliondo, na sasa wamasai wanatimuliwa ili Kitalu kingine kipigwe mnada..
Eti sio eneo la Ngorongoro, kumbe hivyo vitalu viko Sinza Mori sio? , aisee.., utaahira ni kipaji , sasa nimeamini..