Tanzania kuna sheria inayosimamia matumizi ya maji ya mvua?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Wakati ubinafsishaji umepamba moto Bolivia walibinafsisha DAWASCO yao kwa kampuni ya France. Kampuni ikapiga marufuku wananchi wa mji kukinga maji ya mvua. Ilisema hayo ndiyo yanaingia ardhini na kwenye vijito ambako wao hukinga. Wananchi waliandama na kampuni ikafurushwa.

Juzi kati kuna jiji US limemshtaki raia wake aliyekuwa akikinga maji ya mvua. Jaji akawauliza jiji kama maji hayo yalikuwa yao kabla hayajatua chini. Wakajibu hapana. Basi akadai kuwa hawana haki ya kumshtaki jamaa.

Sehemu hii inaeleweka. Maji ya mvua kwa miaka na miaka yamechukuliwa kama hewa. Ni haki ya mtu kutumia bila kuulizwa.

Kwa upande mwingine. Maji ya mvua ni mali ya jamii nzima. Ndiyo yanalisha visima na vijito na mito. Je matumizi yake hayapaswi kuwa regulated? Maana matumizi yake yanaathiri jamii nzima. Kwa nini matumizi ya maji ya visima na mito yako regulated na ya mvua siyo? Vipi, maji ya mvua yanaweza kupatwa na lile janga la Tragedy of the commons? Vipi akitokea Mtu anaweza kukomba maji ya mvua kwa ulafi hadi akaathiri yanayowafikia wengine?
 
Wakati ubinafsishaji umepamba moto Bolivia walibinafsisha DAWASCO yao kwa kampuni ya France. Kampuni ikapiga marufuku wananchi wa mji kukinga maji ya mvua. Ukisema hayo ndiyo yanaingia ardhi na kwenye vijito ambako wao hukinga. Wananchi waliandama na kampuni ikafurushwa.

Juzi kati kuna jiji US limemshtaki raia wake aliyekuwa akikinga maji ya mvua. Jamaa alienda mahakamani. Jaji akawauliza jiji kama maji hayo yalikuwa yao kabla hayajatua chini. Wakajibu hapana. Basi akadai kuwa hawana haki ya kumshtaki jamaa.

Kwa upande mwingine. Maji ya mvua ni mali ya jamii nzima. Ndiyo yanalisha visima na vijito na mito. Je matumizi yake hayapaswi kuwa regulated? Maana matumizi yake yanaathiri jamii nzima. Kwa nini matumizi ya maji ya visima na mito yako regulated na ya mvua siyo? Vipi, maji ya mvua yanaweza kupatwa na lile janga la Tragedy of the commons? Vopi akitokea Mtu anaweza kukomba maji ya mvua kwa ulafi hadi akaathiri yanayowafikia wengine?
Nani mwenye uwezo wa kukomba maji ya mvua kwa ulafi atatumia nyenzo gani🤔

Watu hata wakakinga maji ya mvua bado huko maporini mvua itanyesha na mito itafurika
 
Assume mtu ana ekari kama 100 hivi. Akaamua kujenga mabwawa na matenki. Maji yote yanayonyesha kwenye hizo ekari mia anazuia. Huko downstream mito na visima si vitakauka?
 
Wakati ubinafsishaji umepamba moto Bolivia walibinafsisha DAWASCO yao kwa kampuni ya France. Kampuni ikapiga marufuku wananchi wa mji kukinga maji ya mvua. Ukisema hayo ndiyo yanaingia ardhi na kwenye vijito ambako wao hukinga. Wananchi waliandama na kampuni ikafurushwa.

Juzi kati kuna jiji US limemshtaki raia wake aliyekuwa akikinga maji ya mvua. Jamaa alienda mahakamani. Jaji akawauliza jiji kama maji hayo yalikuwa yao kabla hayajatua chini. Wakajibu hapana. Basi akadai kuwa hawana haki ya kumshtaki jamaa.

Sehemu hii inaeleweka. Maji ya mvua kwa miaka na miaka yamechukuliwa kama hewa. Ni haki ya mtu kutumia bila kuulizwa.

Kwa upande mwingine. Maji ya mvua ni mali ya jamii nzima. Ndiyo yanalisha visima na vijito na mito. Je matumizi yake hayapaswi kuwa regulated? Maana matumizi yake yanaathiri jamii nzima. Kwa nini matumizi ya maji ya visima na mito yako regulated na ya mvua siyo? Vipi, maji ya mvua yanaweza kupatwa na lile janga la Tragedy of the commons? Vopi akitokea Mtu anaweza kukomba maji ya mvua kwa ulafi hadi akaathiri yanayowafikia wengine?
Waregulate huko juu kabla ya kutufikia. Otherwise ni ngumu sana.
 
Kama kiasi cha maji anayoweza kudraw mtu kutoka mitoni na ardhini kwenye visima kiko regulated, kwa nini anachotoa kwenye mvua kisiwe regulated? Ukizingatia kuwa hayo maji ya ardhini na kwenye mito yanatokana na mvua!
 
Hamna sheria mkuu. RWH ni free kwasababu sio resources ya bonde. Resources zetu sisi ni surface na maji ya ardhini tu, hayo ukitaka uyaguse ndio lazima kibali.
 
Assume mtu ana ekari kama 100 hivi. Akaamua kujenga mabwawa na matenki. Maji yote yanayonyesha kwenye hizo ekari mia anazuia. Huko downstream mito na visima si vitakauka?
Mto haupati maji kutoka mvua ya eneo moja. Kuna concept ya watershed au catchment au basin ndio inayotupatia mvua kwenye mto.

Kuhusu maji ya ardhini/visima, hii habari nyingine. Mvua inaweza ikanyesha Mlandizi maji yakarecharge uko hafu akafaidi mtu wa Ubungo.
 
Sasa watu wa kwenye catchment area ya mto wakianza kuvuna maji ya mvua bila kuwa regulated haiwezi kuathiri mtiririko wa mto? Siku hizi kuna madata centre, yanatumia maji mengi sana na yanataka maji safi. Yakinunua maelfu ya mahekta na kuanza kukinga maji safi ya mvua!!
 
Wakati ubinafsishaji umepamba moto Bolivia walibinafsisha DAWASCO yao kwa kampuni ya France. Kampuni ikapiga marufuku wananchi wa mji kukinga maji ya mvua. Ilisema hayo ndiyo yanaingia ardhini na kwenye vijito ambako wao hukinga. Wananchi waliandama na kampuni ikafurushwa.

Juzi kati kuna jiji US limemshtaki raia wake aliyekuwa akikinga maji ya mvua. Jaji akawauliza jiji kama maji hayo yalikuwa yao kabla hayajatua chini. Wakajibu hapana. Basi akadai kuwa hawana haki ya kumshtaki jamaa.

Sehemu hii inaeleweka. Maji ya mvua kwa miaka na miaka yamechukuliwa kama hewa. Ni haki ya mtu kutumia bila kuulizwa.

Kwa upande mwingine. Maji ya mvua ni mali ya jamii nzima. Ndiyo yanalisha visima na vijito na mito. Je matumizi yake hayapaswi kuwa regulated? Maana matumizi yake yanaathiri jamii nzima. Kwa nini matumizi ya maji ya visima na mito yako regulated na ya mvua siyo? Vipi, maji ya mvua yanaweza kupatwa na lile janga la Tragedy of the commons? Vipi akitokea Mtu anaweza kukomba maji ya mvua kwa ulafi hadi akaathiri yanayowafikia wengine?
Hata tozo za miamalq zilianza hivihivi kama tunyuzi twa kipuuzi.

Huwa mnatumwa kuleta hoja ili mpime mapokeo, huenda mmejiandaa kutuuzia mvua ambayo ni kwa hisani ya mama yenu
 
Back
Top Bottom