Tanzania kuna sheria inayosimamia matumizi ya maji ya mvua?

Tanzania kuna sheria inayosimamia matumizi ya maji ya mvua?

Wakati ubinafsishaji umepamba moto Bolivia walibinafsisha DAWASCO yao kwa kampuni ya France. Kampuni ikapiga marufuku wananchi wa mji kukinga maji ya mvua. Ilisema hayo ndiyo yanaingia ardhini na kwenye vijito ambako wao hukinga. Wananchi waliandama na kampuni ikafurushwa.

Juzi kati kuna jiji US limemshtaki raia wake aliyekuwa akikinga maji ya mvua. Jaji akawauliza jiji kama maji hayo yalikuwa yao kabla hayajatua chini. Wakajibu hapana. Basi akadai kuwa hawana haki ya kumshtaki jamaa.

Sehemu hii inaeleweka. Maji ya mvua kwa miaka na miaka yamechukuliwa kama hewa. Ni haki ya mtu kutumia bila kuulizwa.

Kwa upande mwingine. Maji ya mvua ni mali ya jamii nzima. Ndiyo yanalisha visima na vijito na mito. Je matumizi yake hayapaswi kuwa regulated? Maana matumizi yake yanaathiri jamii nzima. Kwa nini matumizi ya maji ya visima na mito yako regulated na ya mvua siyo? Vipi, maji ya mvua yanaweza kupatwa na lile janga la Tragedy of the commons? Vipi akitokea Mtu anaweza kukomba maji ya mvua kwa ulafi hadi akaathiri yanayowafikia wengine?

Post kama hizi ni matokeo ya kwenda shule kukariri badala ya kwenda shule kusoma!
 
Back
Top Bottom