Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
TANZANIA KUSHIRIKIANA NA IRAN SEKTA YA MICHEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya Michezo.
Makubaliano hayo yameingiwa Oktoba 19, 2024 Jijini Dar es Salaam kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Jamhuri ya Kiislam ya Iran ikiwakilishwa na Mhe. Gholamreza Nouri Waziri wa Kilimo.
Nchi hizo zinatarajia kushirikiana katika Utalii wa michezo, kubadilishana wataalamu pamoja na kupeana uzoefu katika miundombinu ya michezo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmood Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa pamoja na wataalam wengine kutoka wizara hizo.