Tanzania Kushirikiana na Iran Sekta ya Michezo

Tanzania Kushirikiana na Iran Sekta ya Michezo

Mkuu umejuaje mimi ni wa upande ule? Na wakati hakuna sehemu nimesema nipo upande gani?
Hapa issue ni kujadili tunabenefit nini na hizi link ups za middle east, kwa sababu tukideal na china hakuna sehemu tunasema tunakaribisha dini za kichina.
Kuhusiana na teknolojia inategemea na kitu husika mfano hapo middle UAE kule jangwani anarusha helicopter na drones kutengeneza mawingu yatayoleta mvua na analima, pale israel wanafunzi wa SUA wanapelekwaga kupiga kilimo na ufugaji. Zijadili hoja mkuu
Wewe naona huelewi hao watu hakuna wanachojua zaidi ya vita na ugaidi sijui unataka tukajifunze nini kwa waarabu kama hata wao wenyewe wanawategemea wazungu
 
Wewe naona huelewi hao watu hakuna wanachojua zaidi ya vita na ugaidi sijui unataka tukajifunze nini kwa waarabu kama hata wao wenyewe wanawategemea wazungu
Badili mtazamo mkuu. Kila kitu inategemea unakiangalia kwa namna gani. Hata hao wazungu uliowataja wanawategemea hao "wanaojua vita na ugaidi" kwenye oil wameenda mbali hata baadhi ya bandari zikiwemo za huko ulaya wanaoperate wale jamaa wa dp world. (Kikubwa mnasaini mkataba wa makubaliano yapi)
 
TANZANIA KUSHIRIKIANA NA IRAN SEKTA YA MICHEZO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya Michezo.

Makubaliano hayo yameingiwa Oktoba 19, 2024 Jijini Dar es Salaam kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Jamhuri ya Kiislam ya Iran ikiwakilishwa na Mhe. Gholamreza Nouri Waziri wa Kilimo.

Nchi hizo zinatarajia kushirikiana katika Utalii wa michezo, kubadilishana wataalamu pamoja na kupeana uzoefu katika miundombinu ya michezo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmood Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa pamoja na wataalam wengine kutoka wizara hizo.

Mmmh Iran katika Michezo!!!!? Iran, inajua Michezo gani!?? Kwanini hatukwenda Brazil, Mexico, Italy, Ufaransa, UK, Nigeria, Cameroon, tunaenda Iran kuomba msaada wa wataalamu wa Michezo!? Hii nchi kila kitu ni kichwa chini miguu juu!
Inaeleweka kabisa, ukitaka upate utaalamu wa IT, nenda, India, Korea, china,
Sasa hawa kenge wa bongo, utunzaji misitu, unawapa waarab waliopo jangwani! Huko kwao walipanda wapi miti, mpira unaomba msaada Iran! Seriously why not Italy, France, Morroco, Nigeria, Brazil, Argentina! Hapa ni uislam wa Bibi mkora,ndio umeangaliwa
 
Badili mtazamo mkuu. Kila kitu inategemea unakiangalia kwa namna gani. Hata hao wazungu uliowataja wanawategemea hao "wanaojua vita na ugaidi" kwenye oil wameenda mbali hata baadhi ya bandari zikiwemo za huko ulaya wanaoperate wale jamaa wa dp world. (Kikubwa mnasaini mkataba wa makubaliano yapi)
Mkuu tuishie hapa baki unavyoamini
 
Back
Top Bottom