robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 842
- 1,425
Tume ya maridhiano iliyokuwa ya kutolea mfano ni ile ya Afrika ya kusini. Matatizo ya Afrika Kusini yalitokana na siasa za ubaguzi wa rangi. Baada ya siasa hizo kutoweka, Ndo ikaundwa Tume ya maridhiano. ilikuwa salama kwa sababu hakuna jinsi siasa hizo zinaweza kurudi nchini kwao.
Kenya waliuwana kwa sababu ya ukabila. Baada ya uchaguzi wakaweka Tume ya maridhiano wakati ukabila bado uko pale pale! Tume hiyo haijaweza kuondoa matatizo yao. Ni upuuzi tu!
Tanzania tunataka kuletewa upuuzi huo, iwe ni kichaka cha kuficha uovu wa kisiasa. Watu wameuwawa kwa sababu ya umwamba wa CCM kutotaka kuruhusu siasa za wazi kwa watu wote. Bado CCM ina siasa za kuzomea wakoloni. Kwa sasa wanazomea yeyote asiyekuwa mwana CCM.
CCM imekuwa ni biashara ya kupata utajiri. Hazina ya nchi inachotwa na kupelekwa CCM. Miradi ya kitaifa inabuniwa ili iwe sehemu ya kupitishia pesa kuelekea kwenye Chama. CCM wako tayari kuuwa ili wabaki madarakani, ili wizi wao usijulikane.
Kama unauwa watu kwa misingi hiyo unatafuta maridhiano ya aina gani? Huwezi kuridhiana na watu wakati unafahamu huwezi kuachia madaraka kihalali. Una lengo la kuiba na huachi kuiba, kwa nini unaalika watu kwenye maridhiano? Huo ni ujinga na upuuzi ndani yake.