Asante deonova kwa hii thread, unastahili pongezi za dhati maana kweli unatusaidia kwenye swala la haki za kazi.
Naomba msaada kwa yafuatayo, sijui sheria inasemaje?
Niliajiriwa na muhindi, sina mkataba na miaka 3 imepita sasa, nimesoma natambulika kisheria kuwa na haki zote kikazi.
Niliahidiwa kuanza na mshahara wa lak8, na baada ya miezi utapanda hadi 1.2m, kumbe zilikuwa story za kunivuta, kazi ni ya ukandarasi.
1. Nilipelekwa kigoma kusini toka dar, nikawa napokea lak8 kwa mwezi na lak1 ya chakula, kulala kambini kazini.
Je, nafaa kulipwa daily allowance? hata kama nilikuwa sijui sheria inasemaje, nilikaa kule miezi 9 mfululizo na kazi kila siku isipokuwa siku za mvua na baadhi ya sikukuu. Bado naweza kudai?, maana kwa siku ni 40,000 x miezi9
2. Niliomba mkopo wakati niko kazini kigoma kipindi hicho, nikapewa 2m, ambayo ilianza kukatwa mwezi huo huo, na nilikatwa lak5 kila mwezi, na nilishaomba deni nianza kulilipa baada ya miezi3 ili kujipa muda wa kutatua shida lakini nikawa sina budi maana pesa zilikatwa juu kwa juu. Je sheria inasemaje kwenye ulipaji deni na kwa asilimia ngapi maana naona ilikuwa ni kiwango cha juu na nikajipata nina shida zaidi kutokana na hilo.
3. Miezi miwili baada tu ya kumaliza miradi na kurudi dar, nikapunguziwa mshahara kiasi cha lak3, nilikataa kitendo hicho na boss mwenyewe akasema kama sikubaliani na mshahara nitafute kazi kwingine. Sababu ya punguzo alidai biashara imekaa vibaya na sababu ni utawala mpya kukaza vyuuma, je bado naweza kudai kiasi nilichopunguziwa kisheria? miaka miwili imeshapita tangu punguzo, na boss alitoa ahadi atalipa biashara ikiwa nzuri, cha ajabu kampuni inaiingiza pesa na yeye kila siku analia njaa, sheria inaweza kunisaidia kulipwa lak3 zangu nilizokatwa kwa miaka 2 sasa?
4. Likizo sijaenda miaka 3 yote ya ajira, na wiki iliyopita baada ya kuona hali mbaya nikaamua kwenda kudai pesa za likizo za nyuma, maana niliona ni bora kuliko kuomba mkopo tena, boss kama mbogo na kusema badala ya kunilipa eti nichukue likizo ya miezi hiyo 3 mfululizo, nikagoma na kwa mara nyingine kuambiwa kama siwezi kazi nitafute nyingine. Je, nina haki ya kupata pesa za likizo hizo?
5. Kazini kwetu, ingawa ni kampuni kubwa, lakini hatulipiwi nssf,wcf,sijui paye wala chochote cha uzeeni, miaka 3 sasa bila mafao, je hii imekaaje? Ninahaki nazo bado?
6. Naona kuuna mazingira yanawekwa kuufanya kazi iwe chungu kwangu nijiachishe, jambo ambalo siwezi bila kupata haki zangu nilizouliza hapo juu, yyaani naingizwa umaskini na boss. Je, naweza kujiachisha kazi kwa msingi wa "constructive dismissal" na bado kulipwa madai yangu?
Samahani kwa uzi mrefu na maswali mingi. Ushahidi ninao wa vitu kibao utokanao na madai yangu, je muda unaruhusu kudai ama siku nyingi tayari zimepita na imekula kwangu?
Pia huyo boss ana kampuni mbili ambazo kazi zinaiingiliani, na huwa nafanya kutokana na shida na majukumu, lakini kama nitaamua kupeleka madai yangu mahakamani, je naweza kushinda, ama nitakuwa napoteza muda tu?
Nashukuru kwa muda wako, nawasilisha.