Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Nimeelewa sana mkuu sorry unaweza nisaidia majukumu ya baraza la wafanya kaz na jukumu la members wake katika halmashaur?

Nitacopy na kupaste kutoka ktk slides zangu nnazotumia ktk utoaji wa elimu ya mabaraza hayo mkuu, bahati mbaya zipo kwa kiingereza ila nadhani utaelewa.

1. To advice the management on measure to be taken to ensure that public service is delivering service with efficiency, effectiveness and higher standard in order to develop sustainable national economy.

2. To advise the management on matter relating, to the interest and welfare of public servants.

3. Advise the management on any changes on laws, rules, regulations relating to terms and conditions in the public service.

4. To advise the management of matters relating to promotion and discipline in the public service.

5. To discuss and advise on organizational plans its revenue and expenditure estimate. (mambo ya bajeti za idara, halmashauri n.k)

6. Discuss and give advice, training and staff development and

7. Enhance cooperation between workers and management in carrying out Government business


Members wanaoingia ktk baraza la wafanyakazi (kwa case ya halmashauri) ni;
1. Mkuu wa Taasisi (Mkurugenzi Mtendaji)
2. Wakuu wote wa Idara
3. Wajumbe wa kuchaguliwa mmoja mmoja kutoka kila idara
4. Wajumbe wa Halmashauri ya chama cha wafanyakazi kilichopo eneo la mwajiri.....kama kuna chama zaidi ya kimoja (manake halmashauri kuna walimu wanakuwa CWT, watumishi wa afya unakuta wapo TUGHE, watumishi wengineo unakuta wapo TALGWU) basi maana yake hapa kutakuwa na 'Master Council' na katiba yenu itakuwa imeainisha mgawango wa wajumbe watakaoingia kwenye baraza kwa uwakilishi wa kila chama cha wafanyakazi kilichopo hapo).....a representative from a 'master council'
5. Mwakilishi kutoka makao makuu ya chama cha wafanyakazi.
6. Afisa Kazi (kwa ishu za uchaguzi na uelimishaji)

Na legitimacy ya uwepo wa mabaraza ya wafanyakazi ktk taasisi za umma ni kwa mujibu wa;
  1. Presidential secular No. 1 of 1970 by J.K Nyerere – the genesis of Workers council in Tanzania. The directive to be used with observations.
  2. Public Service(Negotiating Machinery) Act No. 19 of 2003 reading with regulations of 2005
  3. Public Service Act No. 8 of 2002 reading with regulations of 2003
  4. Employment and Labour Relations Act No.6 of 2004 reading together with Rules of Codes of Good Practice GN. 42 of 2007
  5. Labour Institutions Act No. 7 of 2004 reading together with Rules of Codes of Good Practice GN.42 of 2007.
  6. United Republic of Tanzania Constitution of 1977, Article 18 (freedom of expression).
  7. ILO Conventions and Recommendations on Social Dialogues and Collective Bargaining.

  1. In Tanzania workers’ council is implemented in Public Institutions as per Public Service (Negotiating Machinery) Act No. 19 of 2003 reading with regulations of 2005. Rule 24 state that:
There shall be a workers’ council in each of the Ministry, Independent Department, Regions, Local Government Authority, Government Institutions and Executive Agencies formed in accordance with the procedures stipulated under the law providing for establishment of trade unions”. Refer section 73 of ELRA No. 6 of 2004"

NADHANI NITAKUWA NIMEJIBU VEMA SWALI LAKO MTUMISHI.
 
Wadau kuna kitu kinaitwa Gratuity,hii upewa mwajiliwa wa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufikia mwisho wa mkataba kabla ya Ku renew mkataba mpya . hivi hii kitu inastahiri kukatwa kodi?
 
Unapewa Gratuity 25% of total amount you accumulated during entire contract period
 
deonova,

Asante, nimekuelewa mkuu...ikiwa haonyeshi kuridhika na mimi kuondoka katika kampuni je? Na tarifa tayari nimeshatoa
 
Mkuuuu!! Hapo kwenye wages me nmeshindwa kuelewa kidogo hiyo minimum wage wanayoandika 100,000 au 130,000 kwa mwezi ni mshahara wa MTU kweli kwa nyakati hizi au me ndo sielew

 
Asee ishu yako ni ndefuuuu....uko mkoa gani mkuu ili nikuunganishe na mtu/afisa anaweza kupokea nyaraka zako na kuzichambua na kuona namna tunaweza kusaidia mkuu?[/QUO

Nipo Dar, nitashukuru kwa msaada.
 
Asante mkuu kwa ushaur wa kitaalamu Mi naomba kuuliza!

Nina Ndugu yangu alifukuzwa kazi bila utaratibu akaenda Labour kutafuta msaada,baada ya muda labour wakaandika barua ya kumruhusu arud kazin!Shirika likakataa Barua ya Labour na likampeleka mahakamani Baada ya miaka 6 hukumu ikatoka akahukumiwa miaka 2. kifungo cha nje(Hapa hakimu alimwambia usithubutu kukata rufaa)

Ni miaka 3 imepita kwa sasa yeye ni mgonjwa Anahitaji kupata stahiki zake kwasababu utaratibu haukufuatwa wakati wa kufukuzwa kazi!Je ana uwezo wowote wa kupata stahiki zake?
 
Mkuu "formal probation" ni siku ngapi na je ni sababu zipi zinaweza kupelekea probation kuwa extended..?
 

Habari!

Sheria ya Ajira na mahusiano kazini imetoa utaratibu wa kushughulikia mgogoro wa uachishwaji kazi. Kimsingi kwa suala la Termination of employment Mfanyakazi anapaswa kuwasilisha mgogoro huo mbele ya Tume ya usuluhishi na Uamuzi ndani ya siku 30 tangu alipoachishwa kazi. Ikitokea umechelewa then unatakiwa kuwasilisha mgogoro huo kwa njia ya maombi ya kuomba Tume isikilize mgogoro wako nje ya muda “condonation”. Katika maombi hayo utajaza fomu maalumu ya kuwasilisha mgogoro CMA, pamoja na fomu maalumu ya Condonation, hati kiapo na taarifa ya kufanya maombi.

Katika fomu hiyo utaeleza pamoja na mambo mengine sababu za zilizokufanya uchelewe kufungua mgogoro. (Ifahamike kwamba Tume mpaka ijiridhishe kua sababu zilizokufanya uchelewe ni za msingi ndipo maombi hayo yatakubaliwa na shauri la termination litaanza kusikilizwa)

Kimsingi inatakiwa kila siku uliyochelewa uonyeshe sababu za kuchelewa. Ilitokea kulikua na uzembe Tume itatupilia mbali maombi hayo.

Sasa inapotokea kwa wakati mmoja unashauri mahakama ingine, bado haikuzuii kufungua mgogoro wa kikazi. Mara nyingi ni vyema ufungue ukiwa ndani ya muda then ufanye maombi maalum ya kusimama ukingoja kuisha kwa kesi ingine (zinatakiwa ziwe na uhusiano unaoathiriana)

Nimeona nishare na nyinyi! Kama kuna mahali sijapagusia then Wanahaki wenzangu wataongezea
 
na sheria ikoje kuhusu mfanykazi wa uma kuwa na tattoo!?

Hilo linakuwa kosa la kimaadili mkuu (misconduct)....huyo mrejeshe kwenye ile Kanuni ya Maadili ya Utumishi wa Umma aisome aielewe vizuri. Kama ni Tatoo ambayo iko eneo la wazi la kuonekana inabidi aifute.
 
Ni swali kidogo. Mfano ulipewa mkataba mwenye gratuity baada ya miaka miwili. Ila mkataba huo kila mwaka ukiisha unasaini upya. Mwaka mmoja ukaisha vema. Mwaka wa pili unataka usaini gafla kipengele kimeondolewa. Je kuna haki yoyote muajiriwa anaweza kupata hapa?
 
unajua mkuu,watz wengi hawana muda wakusoma hiyo katiba ya ili wajue sheria na haki yao inasemaje,ndio mana wengi tunaburuzwa ktk makampuni na taasisi za umma,
 
Reactions: sab
Mkuu kuna kundi la wafanyakazi waliopandishwa vyeo mwaka 2016 kwa barua kutoka katibu mkuu lkn mwaka 2018 wamepewa barua ya kusitisha upandishaji wa vyeo uliofanyika mwaka 2016 na badala yake barua imewatambua kwamba wamepanda mwaka 2017 sababu ni kwamba kipindi hicho serikali ilisimamisha upandishwaji wa vyeo kutokana na zoezi la uhakiki! hapo maswali kadhaa yameibuka je wanaweza kupewa ushauri gani wa kisheria?je,waliostaafu kabla ya barua hizi mpya wanakuwa na nafasi gani?

Je, Katibu mkuu anayo mamlaka kufuta barua aliyo itoa yeye mwenyewe na kusogeza mbele wakati watumishi hao walianza kutumikia vyeo vyao vipya mara baada ya kutunukiwa?
 
Nilikuwa nafanya kazi sector binafsi kwenye mradi wa miaka 3,mkataba kwa wafanya kazi ni mwaka mmoja then una-renew.

Mkataba wangu ulikuwa from 1st April 2017 to 31st March2018, mkataba unasema ikitokea hawata renew basi one month notice itatolewa-ila all over sudden Jana tar 29.3...wametangaza haturenew mkataba na siku ya mwisho kuwepo kazini ni tar 31...sijapewa barua...ndio nataka kwenda chukua jmos.

....sijui hii imekaaje wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…